Naibu Waziri wa Afya Dkt Ndugulile: Ni marufuku Hospitali kushikilia maiti kwa kile kinachotajwa hadi pale gharama za matibabu yake zitakapolipwa

Hivi haya malalamiko ya watu kudaiwa mpaka kufikia kushindwa kukomboa miili ya wapendwa wao mahospitalini wakaishia kufanya ibada nyumbani na kumshukuru Mungu hayakusikika miaka yote yamesikika mwaka wa uchaguzi?
Hili jambo lipo sana tena kwa miaka mingi kabisa. Mimi mwili wa ndugu yangu umewahi shikiliwa hospitali moja kubwa hapa jijini Dar private. Hakika tulipata taabu sanaaa kulipa lile deni na baada ya wiki kadhaaa tukatoa mwili.

Nafikiri jambo la msingi ni kuwe na utaratibu including ndugu wa karibu kusign form maalum zikiambatanishwa na vitambulisho vya kitaifa na taratibu za wapi msiba unafanyika hivyo madai ya gharama za matibabu kulipwa baadae. Naiunga mkono serikali
 
da hapo chadema watasema sanaaaaaaaaaa kuwa bila wao serikali isingetoa hiyo tozo mbona ni hoja ya muda mrefu sana hiyo ilikuwa haijatolewa maamuzi tu

Hapo Chadema imetoka wapi Kaka? Lakini huu uamuzi umekaa ki siasa Zaidi.Utekelezajiwake ni mgumu na unawaweka watendaji kwenye mtego mbaya sana katika kutekeleza majukumu yao.

Kabla ya kusifia inabidi kuona muongozo wote wa utekelezaji wa hii makitu. Kwa sababu principle ya kuchangia bado iko pale pale na haijafutwa. Tulisha sikia mara nyingi mgonjwakushiliwa wodini akitakiwa kulipa billyake ya matibabu ndio aruhusiwe kutoka.
 
Ila mambo mengine siasa hazitakiwi hospitali ni sehemu yenye ubinadamu kuliko mahala popote kwenye huduma za jamii wapo watu wanaoshindwa kulipia matibabu baada ya kupona au wakati wa matibabu na kwa kupitia ofisi ya ustawi wa jamii hugawana gharama au kulipiwa gharama zote hili nimeliona mara nyingi likifanyika tena kwa watu wa hali za chini lakini pia kwenye swala la maiti kuna ubinadamu sana tatizo watu hupenda shortcuts na kulalamika.

Utaratibu uliopo unazingatia utu na misingi ya huduma nzuri kwa wananchi sasa hawa wanasiasa na matamko huku wengine wakija na story za vijiweni wanaharibu sana .

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sugu ataweka historia kuwa mwaka wake wa mwisho kuwa bungeni alitoa hoja hii maana hana ubavu wa kurudi bungeni mwakani labda abadirishe jimbo.
 
Hivi karibuni Mh. waziri mwenye dhamana na mabo ya afya Mh. Ummy Mwaimu alitoa maelekezo ya kuzuia hospital za serikali na zile zinazo pewa ruzuku na serikali kuacha tabia ya kuzuia maiti.

Hii ni baada ya wabunge wa upinzani kueta hoja bungeni kikao cha 18. Lakini jambo hili lililetwa kwanza na Mh. Kishimba na amekuwa akilisema kwa muda sasa.

Hata hapa JF hoja hii imejadiliwa. Ingawa siupingi upinzani, kilichinisikitisha ni kwa nini Mh. UMMY amempuuza kishimba na kuzima KICK yake?
 
jamani kila jambo na wakati wake huu ndiyo ulikuwa wakati wa kutoa hizo tozo za lazima maiti wapinzani wasije wakaanza kuleta sifa zao kuwa wameilazimisha serikali kuitoa hiyo lazima ya tozo.
 
jamani kila jambo na wakati wake huu ndiyo ulikuwa wakati wa kutoa hizo tozo za lazima maiti wapinzani wasije wakaanza kuleta sifa zao kuwa wameilazimisha serikali kuitoa hiyo lazima ya tozo
iboyamwaka2020, ndo hivyo tena wapinzani wameshapewa POINTI za bure na Mh. Ummy
 
jamani kila jambo na wakati wake huu ndiyo ulikuwa wakati wa kutoa hizo tozo za lazima maiti wapinzani wasije wakaanza kuleta sifa zao kuwa wameilazimisha serikali kuitoa hiyo lazima ya tozo
Bila upinzani ccm isingefanya chochote, ccm inatekeleza Sera za upinzani,
 
Ndugu wadau wa JF. Salamu.

Kuna jambo linaumiza vichwa vya wananchi wengi.

Hivi inakuwaje mgonjwa anaipigania afya yake kwa gharama kubwa lakini kwa bahati mbaya anapoteza maisha. Jina lake limebadilika, sasa anaitwa maiti (marehemu).

Jambo la kushangaza serikali kupitia hospitali inamdai huyo marehemu alipe pesa, asipolipa hatolewi hospitali. Hata maiti anadaiwa?

Wizara ya afya ifikirie kwa kina kadhia hii inayotupata sisi wananchi. Viongozi kumbukeni bila wananchi viongozi msingekuwepo.

Nawasilisha.
 
hapo ndio utajua kazi ya madactari ni kutibu,ila swala la kupona ni majaaliwa ya mwenyezi Mungu.
 
Ndugu wadau wa JF. Salamu.

Kuna jambo linaumiza vichwa vya wananchi wengi.

Hivi inakuwaje mgonjwa anaipigania afya yake kwa gharama kubwa lakini kwa bahati mbaya anapoteza maisha. Jina lake limebadilika, sasa anaitwa maiti (marehemu).

Jambo la kushangaza serikali kupitia hospitali inamdai huyo marehemu alipe pesa, asipolipa hatolewi hospitali. Hata maiti anadaiwa?

Wizara ya afya ifikirie kwa kina kadhia hii inayotupata sisi wananchi. Viongozi kumbukeni bila wananchi viongozi msingekuwepo.

Nawasilisha.
Hili swala ni gumu sana hata mimi linaniumiza ila kuna namna inabidi ifanyike, naomba tujadiliane kwa mtindo wa swali?? Mimi na ww ikiwa tuna hospital na tukapata wagonjwa 20, ndani ya mwezi bahati mbaya wakafariki na wamehudumiwa na madaktari wetu na huduma zetu, na dawa ambazo tumezilipia, haitokua hasara?? Kama jibu ni ndio, serikali ifanyaje kwa waliofark???
 
Mkuu wewe ni Master wa maswali nmeamimia fact yako Kuna raia watauwa ndugu zao ili kukwepa gharama heb just imagine mtu anadaiwa 5 mil at hospital nae ndg zake wasilipe achen hzo
 
Back
Top Bottom