Ng'azagala
JF-Expert Member
- Jun 7, 2008
- 1,286
- 221
Nilimsikia Naibu Waziri wa Elimu Mh Mwantumu Mahiza akiongea na wanafunzi wa ualimu kule Songea (source TBC Taifa jana jioni).
Aliulizwa kuhusu mishahara midogo wanayolipwa walimu. Alijibu kuwa wale wanafunzi wasioridhika ni mishahara ya ualimu watafute kozi nyingine ili wapate hizo kazi zinazolipa zaidi. Na pia hata wale walimu wasioridhika na mishahara pia watafute kazi nyingine na sio kufanya migomo, kwani hata wao (mawaziri nafikiri) wakigoma itakuwaje?
Nilisikitika mno na kauli ile na nilijiulizi hivi
Serikali na wananchi tunalalamika sana kuhusu uhaba wa waalimu na pia mishahara midogo wanayolipwa hawa wachache ukiacha na haki nyingi wanazonyimwa. Je huyu Naibu Waziri anapata wapi kiburi cha kuwaambia walimu watafute kazi nyingine zitakazo walipa?
Alisema walimu wananzia kulipwa kama laki mbili hivi ambazo hazijakatwa kodi. Je huyu Naibu Waziri ameshafanya kautafiti kuona kuwa hiyo inawatosha kuwafanya wasilalamike?
Huyu ni Naibu Waziri wa ELIMU ambaye tunamtegemea asimamie vizuri Elimu yetu wa Tanzania iliyojaa matatizo. Badala ya kuwapa moyo walimu wanaoumia kwa kulitumikia Taifa kwa kujitolea, angalau kwa kuwaahidi kushughulikia matatizo ya Elimu, sasa anaongea kama mtu wa kijiweni.
Sijui CV ya huyu Naibu lakini nafikiri tunamatatizo makubwa na uwezo wa baadhi ya mawaziri wetu.
Hizi kauli MBOFU MBOFU kutoka kwa viongozi wetu zitakoma lini?