Bluray
JF-Expert Member
- Mar 25, 2008
- 3,449
- 127
Mkuu heshima mbele, sijakupata sawa hapo kwenye bold..kwa maana angewadanganya au angewapiga siasa na kukwepesha ukweli ama...?
Huwezi kumwambia mwalimu, anayefanya kazi ngumu na kulipwa mshahara mdogo, katika nchi ambayo unemployment haipimiki kwa ukubwa, kwamba atafute kazi nyingine kama hataki mshahara mdogo.
Hii ni sawa na kumwambia "pika pilau" mtu anayekufa na njaa kwa sababu hana hata unga wa kupika ugali.
Naibu Waziri alitakiwa kuona hili kama challenge na kulifanyia kazi.Hata kama si kwa kuongeza mshahara, serikali inaweza kuanzisha program nyingi tu na nzuri tu za kuwajali walimu na kuwapunguzia ugumu wa maisha.Nchi nyingi zina program kama hizi wa watumishi wa serikali na walimu, ambao traditionaly hawalipwi mishahara minono lakini wanakuwa comensated otherwise.Sisi kwetu tatizo mishahara si mizuri, haiji kwa wakati, halafu hamna hata perks zozote za maana za kuwafuta jasho walimu.Naibu Waziri, kwa sababu yeye alishawahi kuwa mwalimu, angewaeleza amefanya nini kuboresha hali ya walimu, the fact kwamba hajakuwa na chochote cha kusema inaonyesha hakufanya kitu na yeye ni kama robot tu anayesubiri amri za handlers wake waliomuweka pale.
Naibu Waziri anashindwa kuelewa kwamba walimu wana haki ya kulipwa mishahara inayokidhi mahitaji, na kwamba mtu mwenye mapenzi na ualimu, kimsingi halazimiki kuacha ualimu ati kwa sababu tu ualimu haulipi, hili ni kosa, ni utovu wa haki za binadamu zinazompa kila mtu kuwa na uhakika wa kuendesha maisha yake kwa ujuzi wake, ilimradi asivunje sheria.Sasa naibu waziri anasema hawa walimu wanafunzi waende kutafuta kazi nyingine, vipi kama mtu wito wake katika maisha ni ualimu?
This is typical of our leaders -or should I say misleaders- kuacha interesting problems zikae bila kupewa solutions na badala yake kuwa bulldoze watu kwa decrees za kisultani zinazoonyesha kutojali, kutotaka kutoa suluhu, kutoelewa kwamba uongozi ni dhamana na utumwa kwa wananchi -wakiwamo hao walimu wanafunzi- na umangimeza uliokubuhu ulimbukeni wa ubwanyenye ghafi.
Kauli hii imekaa kimtaani taani na kwa watu wote wenye kufuatilia maswala ya elimu kwa makini, naibu waziri alitakiwa kuwaomba msamaha walimu wanafunzi hawa.