Naibu Waziri Gekul Awahimiza Wazazi Kufuatilia Mienendo ya Watoto

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini mkoani Manyara Pauline Gekul amewataka wazazi na walezi kufuatilia mienendo ya watoto wao pindi wakiwa mashuleni pamoja na kushirikiana na walimu ili kuboresha mazingira ya Shule pindi inapohitajika mchango wao

Ameyasema hayo wakati Akiongea na wananchi wa Kata ya Himiti na Bonga kwenye Ziara yake ambapo amesema kuwa hivi karibuni kumekuwa na tabia ya viongozi kutelekeza Shule huku wanafunzi wakiwa wamekaa chini kwenye vumbi ili Hali wazazi wapo na hawafuatilii mazingira wanayopitia watoto wao na suala Hilo kuwaachia walimu pekee jambo ambalo Sio sahihi

Ameendelea kusema wazazi wanatakiwa wajitoe kwa hali na Mali ili kuhakikisha watoto wao wanapata Elimu Bora katika mazingira mazuri yasiyo na bughudhi ili watoto hao wafikie malengo Yao

Pia amewashauri walimu kuwapa wanafunzi kifungua kinywa na isiwe mlo mmoja tu kwa siki bali wapate Milo angalau miwili kwa siku huku akishauri asubuhi wanafunzi wapewe uji asubuhi kwani ni mzuri kwa Afya zao.

1-71.jpg
 
Huyu mnyanyasaji. Mzaririshaji. Waziri una pesa unahangaika wananchi wadogo
 
Back
Top Bottom