Naibu Waziri Kigahe Azitaka Taasisi za Wizara Yake Kupanga Mipango Inayotekelezeka

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,908
945

Naibu Waziri Kigahe Azitaka Taasisi za Wizara Yake Kupanga Mipango Inayotekelezeka

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb.) ameiagiza Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake kuhakikisha Mipango yote inayopangwa kila mwaka inaendana na mwelekeo wa Viongozi Wakuu wa Nchi, Mipango ya Kitaifa na Kimataifa, Ilani ya Uchaguzi pamoja na kufanya ufuatiliaji na tathimini ili kujua viwango vya utekelezaji wake.

Kigahe ameyasema hayo Agosti 23, 2023 alipokuwa akifungua Kikao Kazi cha Menejimenti na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara kilichofanyika katika Ukumbi wa CAMARTEC, Arusha kwa lengo la kujadiliana na kuimarisha ushirikiano katika utatuzi wa changamoto na utekelezaji wa jitihada mbalimbali za kuendeleza Sekta ya Viwanda na Biashara.

Aidha, Kigahe amezitaka Taasisi hizo zinazojumuisha TIRDO, TEMDO, NDC , CAMARTEC, TBS, WMA, BRELA, FCC, FCT, TANTRADE na CBE kuhakikisha zinakuwa mstari wa mbele kuweka mazingira bora na wezeshi kwa sekta ya Viwanda na Biashara inayotegemewa na sekta za uzalishaji kama kilimo, mifugo, uvuvi, madini na maliasili.

Vilevile, Amezishauri Taasisi za Kifedha kupanua wigo wa utoaji wa huduma za kifedha ndani na nje ya nchi pamoja na kupunguza masharti ya utoaji wa mikopo ili kuwawezesha wafanyabiashara wengi kianzisha na kuendeleza biashara zao na kukuza uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema lengo kuu la Kikao Kazi hicho ni kutafsiri majukumu na shughuli zote za Wizara na Taasisi zake kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma,kilichofanyika Agosti 19, 2023.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi hizo na Mkuugenzi Mkuu wa TIRDO Prof. Madundo Mtambo pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA Bi Stella Kahwa wamesema Kikao kazi hicho ni muhimu kwa kuwa kinawawezesha kutatua changamoto zinazowakabili na kutekeleza majukumu ya taasisi zao kwa ufanisi.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Taasisi za Serikali na Binafsi Makao Makuu ya Benki ya NMB, Bw William Makoresho amesema NMB iko tayari kushirikiana na Taasisi hizo ili kuwawezesha wafanyabiashara kuanzisha na kuendeleza biashara zao.
WhatsApp Image 2023-08-27 at 17.13.49.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-27 at 17.13.49(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-08-27 at 17.13.50.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-27 at 17.13.50(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-08-27 at 17.13.51.jpeg
 
Back
Top Bottom