Naibu Waziri Kigahe Afanya Ziara Chuo cha CBE & TRIDO

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

NAIBU WAZIRI KIGAHE AFANYA ZIARA CHUO CHA CBE & TRIDO

Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo la Metrology Annex unaoendelea katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika tarehe 26 Septemba, 2023 ambapo ilielezwa kuwa jengo hilo litagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 22.4, litakapokamilika na litakuwa la ghorofa 10.

Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amewataka wakandarasi wanaojenga na kusimamia ujenzi wa jengo la Ofisi la Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda (TIRDO) kuongeza kasi ya ujenzi ili likamilike kwa wakati uliokubalika.

Ameyasema hayo tarehe 26 Septemba,2023 alipofanya ziara kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hizo mkoani Dar es Salaam.

Mhe. Kigahe amesema kuwa Wizara ina fahamu kuna changamoto zinazojitokeza hivyo amewaomba watumie fedha zilizotolewa Kuboresha vitu vinavyowezekana ndani ya bajeti, na Yale yanayoshindikana kuwe na sababu za kujitoshekeza.

Aidha, Mhe. Kigahe amewapongeza kwa hatua iliyofikiwa kwa sasa ikilinganishwa na hatua ailiyoikuta katika ziara yake ya awali aliyoifanya.

WhatsApp Image 2023-09-28 at 00.50.37.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 00.50.38.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 00.50.38(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 00.50.39.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 00.50.39(1).jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-09-28 at 00.50.40.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-28 at 00.50.40.jpeg
    39 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-28 at 00.50.40(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-28 at 00.50.40(2).jpeg
    55 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-28 at 00.50.41.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-28 at 00.50.41.jpeg
    49.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom