Chakaza
Platinum Member
- Mar 10, 2007
- 41,020
- 74,693
Juliana Shonza Naibu waziri wa Habari na Utamaduni amegeuka kuwa msemaji na mtendaji wa BASATA kama alivyoonekana jana akitangaza "tumemfungia" Roma Mkatoliki miezi sita asifanye kazi yeyote (kinyume na falsafa yao ya hapa kazi tu)
Kazi hiyo aliyoifanya Shonza sio yake kama serikali bali ni ya Baraza la Sanaa ambalo lipo kisheria.
Sasa je huyo aliyefungiwa akitaka kupeleka swala hilo mahakamani kuhusu kuzuiwa kufanya kazi yake halali inayotunza familia yake anamshitaki nani? BASATA au Serikali? Na kama ni serikali je inayo mamlaka ya kumfungia?
Shonza acha kutafuta kiki wakati wizara hiyo ina mambo mengi ambayo yamelala na kama utayasimamia ipasavyo utapata kiki. Tuliza akili, kazi uliyo nayo jiepushe na kutafuta sifa.
Najua wewe Juliana Shonza ni memba humu hivyo waweza kuja na kufunguka mamlaka hayo yako kwa sheria ipi?