Naibu waziri anapokuwa msemaji wa BASATA

Naibu waziri anapokuwa msemaji wa BASATA

Hawa viongozi wetu wanazo job descriptions na Key performance areas au kila moja anaamka na tamko lake.
Mawaziri na manaibu wao huwa wana pewa instruments kwa ajili ya kazi zao. Pia wanao washauri wasomi kabisa ili wafanye kazi zao kwa maelekezo ya kitaalamu.
Tatizo ni u much know na kuendekeza siasa majitaka hata kwenye kazi zao. Unakuta waziri au naibu anataka kufanya kazi kama Polepole wakati wako kwenye kada tofauti kabisa. Angalia huyu Naibu, ni member hapa JF na badala ya kuleta mada zinazohusiana na wizara yake apate ushauri kutoka kwa wabobezi lukuki waliomo humu yeye anaachana na hayo anang'ang'ania kuwasemanga kina Mbowe na Lowassa wakati kama anatimiza majukumu yake sawasawa hao hawana impact yeyote kwake.
Zile semina elekezi hata kama zilikuwa zina icost serikali fedha nyingi lakini kumbe ujinga ni mzigo na gharama yake ni kubwa zaidi. Kweli ule usemi kuwa UKIONA ELIMU GHALI JARIBU UJINGA, tumejaribu na kudhibitisha kuwa ni kweli.
 
Ubaya wa awamu hii ni kila mtendaji wa serikali ameaminishwa "kukunja sura" na kukamata kamata au kumsimamisha mtu kazi ndio utendaji bora wa kazi.

Ndio maana unaona watendaji wengi kwa sasa wamejikita katika mambo haya;

  • Kufungia, kufungia
  • Kukamata, kukamata
  • Kusimamisha kazi
Wimbo umetoka umesikilizwa miaka kadhaa,leo anakurupuka mtu anaufungia, dhumuni ni nini kama umeshasikilizwa kwa muda wote huo?

Na ukitaka kujua ujinga wa watanzania hii inaweza kuwa ni kiki inatafutwa hapo. Utasikia mtu mmoja ametengua maamuzi ya kuzifungia hizo nyimbo. Wasanii wote watampost na umpa masifa ya "mtetezi wetu"

Tungoje,
 
Mwakyembe mjanja sana mambo ya kikuda kama haya anamuachia naibu wake Shonza ila mambo matamu matamu na manono kama ya kwenda kumpokea rais wa FIFA duniani hua yuko faster tu hapo Airport akimsubiri,hahah.

Akili kichwani aisee.
 
Kuna viongozi wengi, haswa mawaziri na manaibu wao, kama ingekuwa inafanywa vetting kihalali wasingenusa hata kidogo hizo nyadhifa walizonazo..
 
Katika Wizara zinazoonewa kupewa uongozi ni hiyo.

Watawawala wa karibu awamu zote wanaweka umakini tu kwenye Nishati, fedha n.k.
 
Kuna viongozi wengi, haswa mawaziri na manaibu wao, kama ingekuwa inafanywa vetting kihalali wasingenusa hata kidogo hizo nyadhifa walizonazo..
Na kwa awamu hii usije shangaa siku moja Mlingwa au Lusinde anapewa Uwaziri au unaibu
 
Nafasi yake alipewa ili kuwakomoa watu flan hahaha awamu ya tano ni kiboko, unaweza kupewa cheo ili kumkomoa mtu hata kama hufai
 
Dats true awamu hii kukomoana kwingi na ujuaji mwingi alafu awajui kwamba kuna watu wana IQ kubwa tu wako nje ya System tunawachora
 
Dats true awamu hii kukomoana kwingi na ujuaji mwingi alafu awajui kwamba kuna watu wana IQ kubwa tu wako nje ya System tunawachora
Siku anatajwa kuteuliwa kuna mtu aliniambia uteuzi huo ni kumkomoa Kubenea sikuelewa, ila sasa nadhani alisema kweli. Kwa combination iliyopo pale sasa hivi hata kushinda kombe la challenge kwa timu yetu ni msamiati mgumu.
Wamebaki na nguo fupi na nyimbo za vibamia
 
Juliana Shonza Naibu waziri wa Habari na Utamaduni amegeuka kuwa msemaji na mtendaji wa BASATA kama alivyoonekana Jana akitangaza "tumemfungia" Roma Mkatoliki miezi sita asifanye kazi yeyote (kinyume na falsafa yao ya hapakazituu)
Kazi hiyo aliyoifanya Shonza sio yake kama serikali bali ni ya Baraza LA Sanaa ambalo lipo kisheria.
Sasa jee huyo aliyefungiwa akitaka kupeleka swala hilo mahakamani kuhusu kuzuiwa kufanya kazi yake halali inayotunza familia yake anamshitaki nani? BASATA au Serikali? Na kama ni serikali jee inayo mamlaka ya kumfungia?
Shonza acha kutafuta kiki wakati wizara hiyo INA mambo mengi ambayo yamelala na kama utayasimamia ipasavyo utapata kiki. Tuliza akili, kazi uliyo nayo jiepushe na kutafuta sifa.
Najua wewe Juliana Shonza ni memba humu hivyo waweza kuja na kufunguka mamlaka hayo yako kwa sheria ipi?
Moja kati ya threads zake

Nimekataa kumpongeza Mrisho Gambo
Ni aibu watu wazima kusema Uongo, Mtama ya Nape na CCM
 
kama anaewateua ajitambui unategemea nini kwa hawa wateuliwa wake?
 
Dats true awamu hii kukomoana kwingi na ujuaji mwingi alafu awajui kwamba kuna watu wana IQ kubwa tu wako nje ya System tunawachora
Naona kaingia tena kwa Diamond kakumbana na dhoruba mpaka imebidi Mwakyembe afanye rescue attempt haraka
 
Back
Top Bottom