Naibu Spika, Tulia Ackson aanza rasmi harakati Jimbo la Mbeya Mjini

Janken jr

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,125
1,178
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu ameanza rasm harakati za kuomba nafasi ya Ubunge Mbeya Mjini ambalo ni Jimbo linaongozwa mtu wa watu, Rais wa mioyo ya watu wa Mbeya, Joseph Mbilinyi.

Tarehe 18/07/18 alikuwa mtaa wa Sae kufanya kikao na umoja wa waendesha bodaboda ukanda wa Sae kwa lengo la kuwajulisha juu ya nia yake ya kuwania nafasi ya Ubunge na kuomba vijana hao nao kumthamini.

Tulia alitumia nafasi hiyo pia kutambulisha taasisi yake ya Tulia Trust pamoja na shughuli zake za kusaidia jamii mikopo yenye riba nafuu ambayo kiukweli ni sawa na sifuri kwani ni 5%. Aliahidi kutunisha mfuko wao bodaboda.

Tulia karibu Mbeya lakini jipime na ujipange. Imani yetu tulio wengi ni juu ya Sugu.

Ukweli ni kwamba mchawi wa CHADEMA(SUGI) mbeya ni CHADEMA(SUGU) wenyewe wajivuruga watawavuraga wananchi mwishowe kupoteza jimbo.ADUI anatafta kila namna apate nafasi kma zile za Arusha na kwingineko watu hasa wawakilishi na wenye nafasi ndani ya chama wamuuunge mkono mh.Magufuli wanashindwa.ile biashara iliyinawira mikoa mingine mbeya imekwama.wakistawisha migogoro basi watakuwa wanaipa nafasi biashara ya kumuunga mkono JPM na kupoteza nafasi walizokuwa nazo kama madiwan na wabunge.Tulia anataman nafasi hiyo.
 
Si tumesikia wale kina Dada wa Chadema wamekamatwa wakifanya vikao vya ndani kule Kigamboni?

Yeye kapataje ruksa kufanya mikutano ya ndani tena kwenye jimbo lisilo lake??

Hii double standard mnayofanya Polisi mtakuja kuleta umwagikaji wa damu hapa nchini!
 
Huyu mama anataka kucheza bongo freva na muasisi MR II ataweza??

Bongooo eeeeee
Bongo dar es salaaammm
Utalialialia
Ndani ya daresalaaam
Kaa chonjo eeeeee........
 
Hivi kumbe ubunge ni biashara inayolipa sana!!
Mana mtu kuanza kampeni mapema hivi tena kwa kutumia fedha (rushwa ) ni jambo LA kusikitisha sana.
Kiongozi anayetafuta madaraka kwa rushwa ni hatari sana.

Hizo fedha atazirudisha vipi?
Ni akina nani wanatoa fedha zao kwa ajili ya kumsapoti mtu kutangaza nia tu tena wakati huu ambao 2020 bado?

Kama tunapambana na rushwa basi tusiwe na urafiki kwenye rushwa.

Mtu huyo ameanza kampeni mapema 2020 ni vizuri akakatwa ili kusafisha chama na kukiweka mbali na wagombea wanaotumia ushawishi wa fedha kupata nafasi.

Hivi kila jimbo watu wakianza kujitokeza na kuanza kutangaza nia tena kwa kutumia mgongo wa misaada ambayo ina harufu ya ushawishi si itakua ni vurugu na kampeni zisizoisha.

Kwanza huyo mtangaza nia amepuuza maelekezo ya Mwenyekiti wake na mkuu wa nchi kuwa mikutano ya hadhara iachwe mpaka 2020 .
Alipaswa awe mfano wa kuunga mkono tamko na amri ya kuzuia mikutano ya kampeni isiyoisha kila Siku.

Kama kampeni zimeanza kwa nini ziwe ni dhidi ya majimbo ya wapinzani tu.

Kwa nini tunajenga taifa lisolo na haki sawa kwa wananchi wenye asili moja na ndugu moja.

Tulipowaondoa Wakoloni tulitegemea kujenga taifa lenye Uhuru na haki kwa wote mana tulibaki waafrika ambao kwa wakati Fulani wote tulikua watumwa .
Sasa cha ajabu tunajenge taifa lenye madaraja japo kuwa wote ni waafrika tuliokua tumeuchukia utumwa. Sasa tunawaweka wengine kuwa huru zaidi na wengine kuwa watumwa wasio na Uhuru.

Namshauri Mtu yeyote anayetaka kutangaza nia asubiri 2020 bunge likivunjwa. Kwa sasa ni kufanya vurugu na kujiona ni bora na jeuri na imara zaidi kuliko wengine hata ndani ya chama chake ambacho pia hakijaanza mchakato wa kugombea ubunge.
 
Jinsi huyu mama alivyo bize kujipenyezapenyeza nilijua kuna kitu anakitafuta, ngoja tuone kama atafanikiwa kuwa mbunge wa kwanza mwanamke Mbeya.

Vv
 
Msitetemeke huyo ni Mbunge tayari Tukuyu kwa Sauli kishaambiwa tayari yeye hatogombea
Kuhusu mikutano kumbuka yeye ndiye Spika ajaye ni Mhimili unaojitegemea.
 
Back
Top Bottom