Nahodha: Sitta lete ushahidi wa Mwakyembe

1800

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
2,215
603
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amemtaka Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta kuwasilisha ushahidi wa madai aliyoyatoa juzi kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe alilishwa sumu. Juzi akiwa na kundi la makada wenzake wa CCM wanaojipambanua kuwa wapambanaji wa ufisadi, katika uzinduzi wa Programu ya Neno la Hekima kutoka kwa Kiongozi iliyoanzishwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima, Sitta alirejea kauli yake ya awali kuwa Dk Mwakyembe ambaye pia Mbunge wa Kyela, alilishwa sumu. "Nasema Dk Mwakyembe kapewa sumu. Kama vyombo vya uchunguzi vinasema siyo, basi watueleze ukweli, tena haraka," alisema Sitta na kushangiliwa na maelfu ya waumini wa kanisa hilo na kuongeza: "Vipi uone binadamu ambaye ukimshika katika ngozi unga unamwagika chini, mhudumu anakuja kuufagia lakini baada ya saa moja unarudi tena, kitu hicho siyo cha kawaida. Wamejaribu, wameshindwa kwa kuwa Dk Mwakyembe analindwa kwa jina la Yesu ambalo ni kubwa kuliko yote. Kwa hiyo nuksi, kurogwa kuwekewa sumu ni kama maji katika mgongo wa bata, yanatiririka tu na kwenda zake." Alisema mafisadi wapo kwa ajili ya kuangamiza taifa na kuwaangamiza viongozi wanaotetea maslahi ya wananchi akidai kwamba sasa siku zao zina hesabika.

Akizungumza jana, Vuai alisema ushahidi ukija suala hilo linaweza kuchunguzwa huku akihoji: "Ulimwuliza Sitta kama ana uhakika." Hata hivyo, Vuai alisema masuala yote yanayohusu uchunguzi hayawezi kuzungumzwa katika vyombo vya habari na kwamba ni mambo ambayo hufanyika kwa umakini mkubwa... "Labda nikueleze kitu... hilo suala unalolisema mimi sijalisikia ila kama amezungumza hivyo basi alete ushahidi." "Kwanza hilo jambo la Sitta kusema Mwakyembe kalishwa sumu unaniuliza mimi? Kwa nini usimtafute huyo Sitta ili akueleze vizuri ili ujiridhishe?" Alisema suala kama hilo linapotokea na mhusika akawa na ushahidi anatakiwa kuuwasilisha sehemu husika na kwamba kuzungumza kitu bila kuwa na ushahidi haisaidii huku akisisitiza kuwa mpaka sasa hakuna mtu yoyote aliyejitokeza kutoa madai hayo.

Dk Mwakyembe aliondoka nchini Desemba 9, mwaka jana kwenda katika Hospitali ya Appolo, India kwa matibabu baada ya kuugua maradhi yaliyosababisha ngozi yake kuharibika na tangu arejee nchini juzi ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuonekana katika hadhara ya watu. Wengine waliohudhuria uzinduzi huo ni Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Kahama, James Lembeli, Mbunge wa Viti Maalumu Mbeya, Hilda Ngoye, aliyekuwa Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro na Mjumbe wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Kilimanjaro , Paul Makonda. Mbali ya kuapa kuendeleza mapambano dhidi ya mafisadi, Dk Mwakyembe pia alisema: "Nilifika hospitalini Oktoba 10 (mwaka jana), na tangu wakati huo sikuweza kuvaa viatu lakini leo hii naweza kuvaa viatu, kwa hiyo shetani ameshindwa." Alisema atatumia siku za Jumapili kuzunguka katika makanisa mbalimbali kwa lengo kumkemea shetani.
 
Daily News: 30 January
Kyela (CCM) Member of Parliamentary and Deputy Minister for Works, Dr Harrison Mwakyembe on Sunday confirmed that he had been poisoned by unknown people bent on harming him.

Mwananchi: 30 January
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amemtaka Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta kuwasilisha ushahidi wa madai aliyoyatoa juzi kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe alilishwa sumu.

Huyu Nahodha kama hana la kusema akae kimya au arudi Zanzibar akalime karafuu. Kwa nini asimwambie Mwakyembe alete ushahidi anamn'gang'ania Sitta?
 
Akalime karafuu unataka kuseme pension ya Uwaziri kiongozi na mazaga zaga mengine hayamtoshelezi kuishi "peponi" mpaka mwisho? achane nae kwanza uwezo kuongoza Wizara ile hana sema basi mambo ya kupeana haya cjui ndo kuleta balance ya Muungano
 
Lakini si walishamuhoji sita? Mwenyewe mwakyembe kakiri sasa huyu muendesha boti za uvuvi jambiani na mchambawima mbona anamkomalia sita?
 
itafika sehemu mwenyewe (mwakyembe) atafunguka tu,tuwe na subira,make mpaka sasa hakuna taarifa rasmi toka kwake.
 
Kila chombo kinachohusika na ilo sakata la sumu vina taarifa na wanajua walichofanya.
Unless Mwakyembe mwenyewe afanye uchunguzi na aweke mambo hadharani ila asitegemee msaada wa serikali!
Sina mengi ni hayo tuu!
 
Yaani nimecheka mpaka basi....du hapa JF mwisho wa mchezo.. nchi hii bwana... Haya Nahodha, jibu hizo hoja !!
 
Nahodha= Captain of jahazis from zanzibar to Tanzania mainland. Tehe
 
Daily News: 30 January
Kyela (CCM) Member of Parliamentary and Deputy Minister for Works, Dr Harrison Mwakyembe on Sunday confirmed that he had been poisoned by unknown people bent on harming him.

Mwananchi: 30 January
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amemtaka Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta kuwasilisha ushahidi wa madai aliyoyatoa juzi kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe alilishwa sumu.

Huyu Nahodha kama hana la kusema akae kimya au arudi Zanzibar akalime karafuu. Kwa nini asimwambie Mwakyembe alete ushahidi anamn'gang'ania Sitta?

Nahodha anataka ushahidi gani zaidi ya ripoti ya madaktari! hawa viongozi wa kuokotwa darajani na kupewa uwaziri kazi!!!
 
RIPOTI YA UCHUNGUZI BINAFSI JUU YA UGONJWA WA MWAKYEMBE
JASON BOURNR
TEL:*********
ID************
Hatua ya kwanza:
Niliamua kujua kama ni kweli kalishwa sumu. Na watu nilio wahusisha katika kujua huko ni TISS.
 
Nahodha anataka ushahidi gani zaidi ya ripoti ya madaktari! hawa viongozi wa kuokotwa darajani na kupewa uwaziri kazi!!!
mwacheni Nahodha naye agombee hiyo nafasi ya juu wamkolimbe au awasute mafisadi km hawajmpeleka India, hapo yeye kawekwa baada ya kuukosa Urais Zanzibar, huku kuna watu wameuvizia Urais hata kwa siku moja tu ndo wanaomtuma atamke
yote iko siku MUNGU atayaanika
 
Mwakyembe hana jipya.

Unamaanisha nini unaposema hana Jipya?????
Alipowaandikia wanausalama kuwa wanataka kumuua ....... si ndiyo yenyewe tunayaona????? si unaona sasa uhai/uzima wake ulivyo???? kwani hawaja muua......
 
Njia ya kumaliza huu mzozo mbona ni rahisi sana. Serikali itoe report ya madaktari na ikugundulika kwamba Mwakyembe hakulishwa sumu basi Mzee Sitta aitwe kwa mahojiano. Vingenevyo hata mtu akisema Mwakyembe aling'atwa na paka ni sawa tu. hakuna report!
 
Daily News: 30 January
Kyela (CCM) Member of Parliamentary and Deputy Minister for Works, Dr Harrison Mwakyembe on Sunday confirmed that he had been poisoned by unknown people bent on harming him.

Mwananchi: 30 January
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amemtaka Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta kuwasilisha ushahidi wa madai aliyoyatoa juzi kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe alilishwa sumu.

Huyu Nahodha kama hana la kusema akae kimya au arudi Zanzibar akalime karafuu. Kwa nini asimwambie Mwakyembe alete ushahidi anamn'gang'ania Sitta?

unajua sitta anawashwa sana..s=umu kalishwa mwingine yeye inamhusu nini??hili zee hili ndo maana lilipigwa chini uspika kwa ajili ya kukurupuka kurupuka na chuki zake zisizo na maana
 
Daily News: 30 January
Kyela (CCM) Member of Parliamentary and Deputy Minister for Works, Dr Harrison Mwakyembe on Sunday confirmed that he had been poisoned by unknown people bent on harming him.

Mwananchi: 30 January
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amemtaka Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta kuwasilisha ushahidi wa madai aliyoyatoa juzi kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe alilishwa sumu.

Huyu Nahodha kama hana la kusema akae kimya au arudi Zanzibar akalime karafuu. Kwa nini asimwambie Mwakyembe alete ushahidi anamn'gang'ania Sitta?

Yakhe Nafodha , hii ligi huiwezi maalim.
Ligi ya kikubwa hii, weye kaa pembeni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom