Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
- Akumbusha wajibu wa viongozi kwa wananchi
Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha amewataka wana CCM kuacha kujidanganya kwamba chama chao kitaendelea kutawala milele.
Nahodha, mmoja wa viongozi wa juu wa CCM na serikali alitoa kauli hiyo jana wakati akiwahutubia wananchi wa Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Ninatofautiana kimtazamo na watu wanaosema kwamba CCM itaendelea kutawala milele na milele, hapa kama hatutajipanga vizuri ipo siku chama chetu kitangolewa madarakani tusibweteke, alisema Nahodha.
Akitoa mfano, Nahodha aliwataka wana CCM kujifunza kutoka katika nchi jirani ambako baadhi ya vyama vilivyopigania uhuru kama ilivyo CCM vimengolewa madarakani. Alikitaja chama cha Kenya African National Union (KANU) ambacho kilipigania uhuru wa Kenya kuwa mmoja wa vyama vilivyopata kungolewa madarakani.
Kumbukeni namna ambavyo KANU ilisambaratika kule Kenya leo hii imesahaulika kabisa. Lakini si huko tu, kule Zambia (UNIP) na Malawi (MCP) vyama tawala vilibwagwa vibaya na sasa vimesahaulika masikioni mwa wananchi, alionya Nahodha.
Akiendelea, alisema ni wazi ipo siku wananchi wanaweza kukichoka CCM na kukibwaga iwapo viongozi watashindwa kutimiza ndoto za wananchi za kuwaletea maendeleo.
My take:
Sasa ni ukweli uliowazi kwamba hata viongozi wakuu wameanza kusema ukweli tofauti na zamani ambapo ilikuwa ni nadra sana kusikia maneno kama haya ukimtoa Baba wa taifa aliyekuwa akiwaambia ukweli.