mkuu NM.... kokoto nyeusi zinajulikana kama granite aggregates na kokoto nyeupe zinajulikana kama coral agreggates ..... concrete (zege) huwa designed kutokana na uzito au uimara strength katika matumizi (concrete grade) ...... grade nyingi za structural concrete huhitaji kokoto nyeusi ... kama vile concrete grade 30 C30 AU GRADE 28 hii ni kwa ajili ya slabs, columns, beams and foundation pads and strips ...kokoto nyeupe kama inavyoitwa ubuyu mtaani ni kokoto ambayo haina nguvu na hutokana na mwamba uliokaribu na uwanda wa bahari yaani coral reef na mara nyingi huwa na composition ya chunvi hivyo kutokuwa na mahusiano mazuri sana na cement .... cement ndiyo kiungo kikubwa cha structural concrete members hivyo basi kama cement haitaungana vilivyo pamoja na kokoto, mchanga na nondo hilo jengo halitakuwa imara .... kukoto nyeupe hutumika kama zege chafu (blinding) na zege ambalo halihitaji reinforcement (nondo) yaani plain concrete
@mazingira ... kwa ujumla tofali unalouliza ni vibrated concrete block .... hili utalipata kwa supplier anayetengeneza tofali 25 mpaka 28 kwa kutumia mfuko mmoja wa kilo 50 za cement lililofanyiwa curing ( kumwagiwa maji ) kwa siku saba ... hivyo basi kuwa na TBS ya kiwango cha 3.5-5KN (kilo newtons)