Poleni wana JF hasa mlioko kwenye mchakato wa ujenzi na ambao mmetoa ushauri. Kimsingi Ndg yangu Mazingira na Mama Joe ushauri mliopewa ni mzuri sana. Ni kuufanyia kazi kwa umakini na kufanya maamuzi sahihi na usimamizi makini.Kwa suala la nondo kweli KAMAKA ndo muafaka. Pale hakuna uswahili na vibaka hakuna. Utaratibuwao ni mzuri. Nendeni pale. Mahitaji ya nondo kiasi na size ni sensitive kwani ni technical aspect ambayo Engineer vema akakufanyia hesabu. Kuhusiana na na kokoto ushauri mzuri umetolewa. Kwa ghorofa moja kokoto za hapa DSM zinafaa tu. Mimi Nilithubutu, Nikaweza na Nasonga mbele. Mimi nimejenga ghorofa 1 naelekea kuezeka Desemba 2011. Amini usiamini, nilinununu mchanga wa kutosha, nikanunua simenti, nikawa na maji ya uhakika na nikawatafuta wafyatua tofari na kusimamia mfuko 1 tofari 25. Curing nilisimamia mwenyewe. ujenzi ulienda vizuri. Pamoja na Engineer wangu lakini nimejitahidi kuwa karibu na kusimamia kila nilipopata nafasi. Nimejifunza mengi juu ya upatikanaji wa building materials bora na kwa gharama nafuu. Kumbuka construction industry is too complicated like its market. Kuweni makini na mafundi, engineer, suppliers nk. Ndg Mazingira naona unahitaji nondo, kokoto, matofari, n.k. sijui uko wapi hapa DSM nione ninavyoweza kukusaidia. Hali kadhalika mama Joe. Ninaweza kuendelea kutoa ushaui if you think fit. Kila la heri