Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

wakuu salama huku ndani......
kwa wanaotafuta miche ya mipapai mifupi tafadhal ni PM. nina miche ya SINTA FI(ya njano ndani) na Malkia F1(mekundu)
Unauzaje na uko wapi?

Amini usiamini, ukihitimu shule ndio utaanza masomo.
 
Mtaji ninao ila tatizo ni shamba siwez kukod miaka mitatu itabidi ninunue ila sijajua ninunue wap ila nafikiria karibu na dar

Mkuu kama uko serious na kilimo cha papai niPM maana nina uelewa sahihi wa zao la papai na sehemu muafaka ya kilimo hiki.
 
Naomba ushauri..mipapai yangu inapotoa maua yananyauka au yanazaa ila papai changa zinanyauka na kudondoka
 
Kweli mkuu.. Kwa kuwa ana miche anauza na ni biashara halali, ingefaa aweke hapa namba ake wateja wampate kirahisi. Nimejaribu hio pm in vain!
 
Baada ya kusoma kuhusu kilimo hiki humu ndani nimeamua kujaribu
Nimekodi shamba sehemu za Kilombero Morogoro pembeni ya mto Ruaha.Mto ambao unatoa umeme wa kidatu. nimeshalima na andaa kuchimba kisima au naangalia uwezekano wa kutumia maji ya mto.
Tatizo ni mbegu.Kariakoo zinauzwa 15,000/ kwa pkt moja ya gramu 5 na ktk kuulizia nimeambiwa zipo 50 tu.Sasa kwa eneo nililoandaa kama eka 2 naweza kupanda roughly miche 1000.
Je kuna sehemu ambayo naweza kupata mbegu nzuri Malkia F1 kwa gharama ndogo kdg? au nitengeneze mwenyewe toka mapapai ya kisasa yaliyokomaa?
 
mpapai wangu ulizaa Matunda yakakomaa ilipofikia hatua ya kuanza kuzaa matunda kwa sasa Kila ikizaa Matunda yananyauka na kuwa na rangi ya njano kisha kudondoka chini.
Naomba ushauri nini kifanyike ili Matunda yasiwe yananyauka?....
thanks in advance
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom