Nahitaji ushauri wa haraka, moyo unauma

Nahitaji ushauri wa haraka, moyo unauma

Habari zenu ndugu zangu, matumaini yangu ya wazi kuwa hamjambo na mnaendelea na harakati za kulisukuma gurudumu la Maisha.

Kwa upande wangu weekend ya leo haijakaa sawa, nahisi kuchanganyika, Presha sio presha, kuumwa sio kuumwa, yaani kwa ujumla hali ni mbaya.

Nikianza na mkasa wangu huu wa mapenzi ambao umenitokea kati yangu mimi na mpenzi wangu ambaye kiukweli nilitokea kumpenda sana na kushindwa kujizuia.

Awali nilikuwa naishi Dsm sema nikaamishwa kikazi kwenda Mwanza, kazi yangu ni nzuri na kama kijana nimeweza kumudu kupanga nyumba nzuri na kausafiri ka kutembelea.

Nakumbuka ilikuwa mwezi wa 9 mwaka Jana ndio nilikutana na huyu mwanamke kwenye klabu moja hivi jijini Mwanza. Hakika nilitokea kumpenda. Safari ya mahusiano ikaanzia hapo.

Kumbe historia ya huyu Crush wangu haikuwa nzuri hasa kutokana na background yake ya watu aliotoka nao kipindi cha nyuma, watoto wa mjini wanasema MDANGAJI.

Ama kweli mapenzi upofu ndio naamini, licha ya kufikishiwa habari zake lakini binafsi sikuzitilia maanani sana, nilijisemea moyoni kwamba nitamrekebisha aje kuwa Mama watoto wangu.

Kwa ufupi kwenye mahusiano yetu ya kipindi cha miezi 6 tumepitia katika changamoto nyingi sana, tumewahi kuachana na kurudiana zaidi ya mara tano. Chanzo kikubwa cha kugombana kwetu ni huyu mwanamke kuendekeza sana starehe. Ikifika weekend kama ya leo ni lazima mtoke.

Hata Kama nikimshauri tusitoke basi atatumia mbinu yeyote atoke kisha arudi asubuhi anigongee au arudi Kulala nyumbani kwake, mbaya zaidi kichwa cha pombe hana.

Tatizo lingine ni kuendeleza mawasiliano na ex's zake, nimefumania text za whatsapp na kawaida akichart na ma-ex wake. Nilikuwa nikijaribu kumwambia abadilike anaacha kwa muda kisha anaendelea. Mbaya zaidi kwny simu niliyomnunulia.

Nakumbuka siku moja tulitoka club ukazuka ugomvi baina yetu ambao ulipelekea nimtembezee kipigo cha mbwa koko. Kipindi hicho alikuwa hajapata kazi. Kila kitu nilikuwa najitaidi kumuhudumia ukiacha kodi ya nyumba aliyokuwa akilipa mwenyewe.

Baada ya ugomvi huu uliopelekea akae ndani wiki nzima kutokana na majeraha ulimpelekea aka-abort mimba yangu ya mwezi mmoja. Penzi likavunjika na kila mtu akachukua time zake.

Ukapita mwezi m1 bila mawasiliano, nilichofanya kosa nikaanza kutembea na rafiki zake ambao kwa idadi wanafika wanne. Drama zote hizi alikuwa akizishuhudia na nyingine kupelekewa taarifa.

Baada ya kufanya upumbavu wote huu, nilirudi nyuma na kujitafakari upya na kuamua kumtafuta na mapenzi yakarudi upya. Kipindi hiki alikuwa kwny mahusiano na Mzee mmoja mume wa mtu ambaye alikuwa akimsaidia katika mahitaji yake.

Tukashauriana tukapime afya zetu, bahati nzuri hatukukutwa na maambukizi, lakini kumbe huyu mwenzangu alipanga afanye revenge pasipo mimi kujua.

Kwanza aliweka utaratibu ambao naweza kusema sio sahihi, yaani yeye atakuwa na yule babu kimaslahi na hata nilipokuwa nawakuta sehemu nilijifanya kama siwajui mpk yule Mzee atakapokuwa ameendoka.

Hali hii ilinisumbua sana hasa ukizingatia wivu ulikuwa juu zaidi, kama hiyo haitoshi hivi majuzi katoa kali, alikuwa anakunywa na Mzee wake, baada ya Mzee kusepa akaja ex wake wa zamani ambaye yupo vzr kifedha.

Baada ya kuona picha ile kiukweli nilizidiwa na wivu na kusababisha ugomvi Mkubwa ambao Kama sio mkono wa Mungu huyu mwanamke angekuwa Marehemu.

Nimekaa nikaona hapana kwa hili lilotokea ngoja nije niombe ushauri kwa wakubwa zangu ambao huenda Wakawa wamepitia kwenye changamoto kama hizi waweze kunishauri haya.

Nimtafute nimuombe radhi maana moyo wangu bado unampenda? Au ni-move on na Maisha yangu? Labda huenda haikuwa ridhki aliyoniandikia Mwenyezi Mungu.

Nipo kwenye hali mbaya. Nakaribisha ushauri na wale ndugu zangu wa matusi na kejeli nawakaribisha pia.

Nawasilisha.
Wewe ni Pimbi.Kama ulikubaliana naye awe na huyo mzee huku ukijua basi wewe ni kiazi huhitaji ushauri wowote zaidi ya kutukanwa
 
Mmmh mbona kama leo Wanaume zamu yetu kuzalilishana!!! Like seriously kabisa nakaa pembeni demu wangu yule pale namuona na Kizeee.
Jamani jamani Uuuuuuuwwiiiiiii. .Mola aniepushe mana kitakacho tokea report ya Ma Dr's ndio itaeleza huyo marehem amekufaje.
 
Brother,.kwanza Pole na Majanga..

Huyo mwanamke sio tu moto wa kuotea mbali ila ni moto usio oteka, mkimbie kama ukoma.
Ni nyoka na hawez badilika leo wala kesho.

Na usikute hao EXs wake nao wanampenda huyo mdada kama ww unavyompenda, so jinsi anavyowapanga wao na ww huko mbelen utapangwa hivyo hivyo.

GET RID OF HER, and her friends, sehem anazoenda usiende, wala sehem ambazo mlikuwa mnaenda usiende maana zitarudisha kumbukumbu.

MOVE ON Brother, na take it easy wakat unatafuta msichana mwingine.

Br
Asante Kaka kwa ushauri. Safari hii nitajitaidi kuukabili huu mtihani
 
watoto walivyo wengi mkuu unahangaika na mmoja mzee?......ila unachokosea kimoja unampigaje mwanamke??? assume mshua wako angekua anampiga mama yako ungejisikiaje? mwanamke ni kama mama yako mmeshindwana move on acha ubondia unaweza kuja kuua
Nimekuelewa Bro. Nashukuru sana kwa ushauri
 
At average mmeachana na kuriadiana Mara moja kila moja kwa kila mwezi
 
Mkuu unatafuta kifo tu... Songa mbele piga moyo konde mwezi tu unamsahau na usiwe unapasha kiporo...
Nitajitaidi japo kipindi kile ulipita mwezi lakini hisia zikarudi za kumkumbuka, nitajitaidi kipindi hiki mkuu
 
Back
Top Bottom