Nahitaji ushauri wa haraka, moyo unauma

Nahitaji ushauri wa haraka, moyo unauma

Kaka, MOVE ON, usipende kulazimisha penzi, halaf penzi la upande mmoja linachosha, halaf una moyo kuruhusu akawe na jibaba ukishuhudia lol huyo n pasua kichwa atakusumbua huko mbele
Asante sana Dada yangu
 
Move on with your life Mkuu hizi drama za huyo Malaya hazikusaidii chochote kile sana sana utaishia lupango.

Habari zenu ndugu zangu, matumaini yangu ya wazi kuwa hamjambo na mnaendelea na harakati za kulisukuma gurudumu la Maisha.

Kwa upande wangu weekend ya leo haijakaa sawa, nahisi kuchanganyika, Presha sio presha, kuumwa sio kuumwa, yaani kwa ujumla hali ni mbaya.

Nikianza na mkasa wangu huu wa mapenzi ambao umenitokea kati yangu mimi na mpenzi wangu ambaye kiukweli nilitokea kumpenda sana na kushindwa kujizuia.

Awali nilikuwa naishi Dsm sema nikaamishwa kikazi kwenda Mwanza, kazi yangu ni nzuri na kama kijana nimeweza kumudu kupanga nyumba nzuri na kausafiri ka kutembelea.

Nakumbuka ilikuwa mwezi wa 9 mwaka Jana ndio nilikutana na huyu mwanamke kwenye klabu moja hivi jijini Mwanza. Hakika nilitokea kumpenda. Safari ya mahusiano ikaanzia hapo.

Kumbe historia ya huyu Crush wangu haikuwa nzuri hasa kutokana na background yake ya watu aliotoka nao kipindi cha nyuma, watoto wa mjini wanasema MDANGAJI.

Ama kweli mapenzi upofu ndio naamini, licha ya kufikishiwa habari zake lakini binafsi sikuzitilia maanani sana, nilijisemea moyoni kwamba nitamrekebisha aje kuwa Mama watoto wangu.

Kwa ufupi kwenye mahusiano yetu ya kipindi cha miezi 6 tumepitia katika changamoto nyingi sana, tumewahi kuachana na kurudiana zaidi ya mara tano. Chanzo kikubwa cha kugombana kwetu ni huyu mwanamke kuendekeza sana starehe. Ikifika weekend kama ya leo ni lazima mtoke.

Hata Kama nikimshauri tusitoke basi atatumia mbinu yeyote atoke kisha arudi asubuhi anigongee au arudi Kulala nyumbani kwake, mbaya zaidi kichwa cha pombe hana.

Tatizo lingine ni kuendeleza mawasiliano na ex's zake, nimefumania text za whatsapp na kawaida akichart na ma-ex wake. Nilikuwa nikijaribu kumwambia abadilike anaacha kwa muda kisha anaendelea. Mbaya zaidi kwny simu niliyomnunulia.

Nakumbuka siku moja tulitoka club ukazuka ugomvi baina yetu ambao ulipelekea nimtembezee kipigo cha mbwa koko. Kipindi hicho alikuwa hajapata kazi. Kila kitu nilikuwa najitaidi kumuhudumia ukiacha kodi ya nyumba aliyokuwa akilipa mwenyewe.

Baada ya ugomvi huu uliopelekea akae ndani wiki nzima kutokana na majeraha ulimpelekea aka-abort mimba yangu ya mwezi mmoja. Penzi likavunjika na kila mtu akachukua time zake.

Ukapita mwezi m1 bila mawasiliano, nilichofanya kosa nikaanza kutembea na rafiki zake ambao kwa idadi wanafika wanne. Drama zote hizi alikuwa akizishuhudia na nyingine kupelekewa taarifa.

Baada ya kufanya upumbavu wote huu, nilirudi nyuma na kujitafakari upya na kuamua kumtafuta na mapenzi yakarudi upya. Kipindi hiki alikuwa kwny mahusiano na Mzee mmoja mume wa mtu ambaye alikuwa akimsaidia katika mahitaji yake.

Tukashauriana tukapime afya zetu, bahati nzuri hatukukutwa na maambukizi, lakini kumbe huyu mwenzangu alipanga afanye revenge pasipo mimi kujua.

Kwanza aliweka utaratibu ambao naweza kusema sio sahihi, yaani yeye atakuwa na yule babu kimaslahi na hata nilipokuwa nawakuta sehemu nilijifanya kama siwajui mpk yule Mzee atakapokuwa ameendoka.

Hali hii ilinisumbua sana hasa ukizingatia wivu ulikuwa juu zaidi, kama hiyo haitoshi hivi majuzi katoa kali, alikuwa anakunywa na Mzee wake, baada ya Mzee kusepa akaja ex wake wa zamani ambaye yupo vzr kifedha.

Baada ya kuona picha ile kiukweli nilizidiwa na wivu na kusababisha ugomvi Mkubwa ambao Kama sio mkono wa Mungu huyu mwanamke angekuwa Marehemu.

Nimekaa nikaona hapana kwa hili lilotokea ngoja nije niombe ushauri kwa wakubwa zangu ambao huenda Wakawa wamepitia kwenye changamoto kama hizi waweze kunishauri haya.

Nimtafute nimuombe radhi maana moyo wangu bado unampenda? Au ni-move on na Maisha yangu? Labda huenda haikuwa ridhki aliyoniandikia Mwenyezi Mungu.

Nipo kwenye hali mbaya. Nakaribisha ushauri na wale ndugu zangu wa matusi na kejeli nawakaribisha pia.

Nawasilisha.
 
Kweli kbs watu wengi walishaniambia kwamba huyu sio Mwanamke, amerithi karibu kila kitu kutoka kwa Mama yake.
Sometimes mapenzi yanawablind watu sana,kuna mtu unaweza kuona kapotea kabisa,ukamshari lakini akakuona wewe ndo hupendi mahusiano yao,mkuu hapo huna mtu
 
Mm sikulaumu ndivyo mapenzi yalivyo, hata mm huwa napenda kwa staili yako, even mke nliye naye tulipitia drama kama zako, nikazuiliwa kumwoa. Ila kwa sasa katulia but mm nimekuwa kicheche zaidi ya alivyokuwa.
 
Shida moja ninayoiona kwa vijana wa sasa ni kwamba mmeamua kumpenda zaidi shetani na kazi zake zote na mambo yake yote badala ya Mungu na hapo tu ndipo mtakapojiangamiza wenyewe.

Mwanaume wa kweli mwenye akili timamu kbs na utashi haolei bar hata siku moja. Ukumbuke mke ni zaidi ya ww ufikiriavyo sio kitu cha mzaha mzaha kwani ndio familia yako ya mbeleni hiyo

Seriously kbs unakutana na malaya muuza kumma na unaamua kbs kwa utashi wako kwamba anakufaa kuwa mkeo!!?? seriously!!??

Wanaume huwa tunakosea tu kwenye kufanya uzinzi, lakini linapokuja suala la mwanamke wa kuoa, wa kuishi nae "MILELE", huwa hatufanyi makosa aiseee!, labda kwa ninyi vijana wa kizazi hiki kipya maana mna mbwembwe sio kidogo

Wapo mabinti wazuri tu, wanaojiheshimu, wanaomba kwa Mungu awaoneshe wanaume wa kuwafaa kuolewa nao wakaishi nao na kuanzisha nao familia

Una safari ndefu ndugu
Asante kwa ushauri Mkuu
 
In short mapenzi yenu mlivyoyaanza mliyaanza vibaya sana yaan unatomba hadharan na yy anatombwa hadharan. So kuoana itakuwa ni kazi bure. Nakushauri kimbia kwa speed ya standar gauge. Ukioa huyo atakutesa kuliko anavyokutesa saiz
Asante kaka
 
Pole sana Mkuu... naomba huu msemo uuelewe vizuri kabisa "Malaya ni malaya tu hata umfadhili vipi hawezi badilika kamwe "....

Ushauri wangu kwako ni wewe kumfungia vioo na uanze kujifunza kuyaenjoy maisha ukiwa mwenyewe....

Ni hayo tu kwa leo mkuu...
 
Inshort umefall kwa changu aisee,halafu acha kupenda hovyo mimi kama katibu wa chama cha wanaume nimesema usipende pende hovyo,tutakuja kukuaga pale leaders club,kwa hili ulilofanya nakupa yellow card!
Kweli kabisa Bro, nimefail wala Hakuna ubishi, ndio maan nimekuja kwenu mnisaidie kimawazo
 
Back
Top Bottom