Nahitaji ushauri please kabla ya kufanya maamuzi

Chauro

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
2,968
1,476
Naombeni ushauri wenu tafadhali.

Nina binti wa kazi ambae nimekaa nae kwa miaka mitatu,kwakweli ni binti mzuri sana mpaka nilifikia uamuzi wa kumpeleka shule.Lakini ghafla baada ya miezi michache nikamuona amebadilika nilikuwa nikimuuliza anasema yupo sawa na kazi anafanya kama kawaida.
\
kilichotokea jana kamuambia mdogo wangu ana mimba,nikamuomba mdogo wangu aendelee kuongea nae ....hiyo mimba ni ya nani kamueleza ni ya mwanafunzi mwenzake na akimpigia simu hapatikani.Alipomuhoji zaidi kamwambia ameongea na mama yake amemuambia atoe hiyo mimba kwakweli nimepata mshtuko.

nimejiuliza maswali mengi,napata wakati mgumu sana

1.Je nimuondoe nyumbani kwangu? lakini napata huruma ataenda wapi .kusema kweli naifahamu vizuri hali ya familia yake ni duni sana.Kumbuka mama ameshauri atoe

2.Niongee nae nimsaidie niendelee kukaa nae azae mtoto wake maana si support kutoa iyo mimba kwakweli namuona kama mdogo wangu.

Ushauri wenu ni wa muhimu sana, nakumbuka wakati nampeleka shule niliongea nae sana sijui aliona maneno yangu hayana maana huruma iliyoingia moyoni mwangu sijui niilezeje.

NAWATAKIA KAZI NJEMA.
 
Jambo la msingi jaribu pia kuwasiliana na familia ya huyo kijana aliyempa mimba thou inawezekana hauifahamu lakini since huyu kijana anasoma pamoja na huyu binti basi inakuwa rahisi kupajua kwao pamoja na ku-dodge kwa huyu kijana. Ni vizuri ukiendelea kukaa na huyo binti ukimsaidia huku ukiendelea kufanya mawasiliano na upande wa pili.

Kitu kingine kilichonishangaza ni jinsi huyo mama yake alivyomwambia kuwa aitoe hiyo mimba
 
asante,Finest na mimi kuhusu huyo mama ndo limenipa tatizo anamuambia tu mtoto atupilie hiyo mimba huko hajui hata itakuaje na akipata matatizo yatabaki kwa nani.

Sidhani kama huyo binti anaweza kumsingizia huyo kijana mimba kwahiyo ni vizuri zaidi wakati ukiendelea kumsaidia huyu binti, ukajaribu kufanya mawasiliano ya haraka na familia ya huyo kijana maana uki-delay na wao wanaweza kuchomoa wakamtetea kijana wao kwamba sio yeye anayehusika na huo ujauzito kwahiyo ni vizuri ukalichukulia hili suala la kushirikisha upande wa pili kwa uzito wa hali ya juu.

Nina uhakika ukimwambia mdogo wako aendelee kumchunguza basi hata nyumbani kwao huyu kijana anaweza kuwa anapafahamu vizuri tu.
 
asante,Finest na mimi kuhusu huyo mama ndo limenipa tatizo anamuambia tu mtoto atupilie hiyo mimba huko hajui hata itakuaje na akipata matatizo yatabaki kwa nani.
Huyu mama upande wa pili, mentality ambayo iko kichwani kwake ni kuwa wewe unaweza kumfukuza huyu binti halafu mzigo wa kulea mimba ukamuangukia huyo mama ndio maana anaona ili isiwe taabu ni bora kuitoa hiyo mimba mama wa watu anaogopa majukumu ila hawazi upande wa pili leo na kesho huyo mtoto ambaye anasema akatolewe anaweza kuja kuwa msaada mkubwa kwake
 
Nakushauri uendelee kuwa nae msaidie mwanamke mwenzio kufikia malengo yake hiyo mimba imetokea bahati mbaya.

kigezo ni mwanamke mwenzake?
we sema tu amsaidie full stop
io kumention MWANAMKE MWENZAKO T SOUND VBAYA..SO ANGEKUWAQ MWANAUME KAPATA TATIZO LOLOTE ASINGEPASWA KUMSAIDIA CZ SI MWANAMKE MWENZAKE?

ANYWAYS AMSAIDIE KM BNADAMU NA NDGU YAKE FULL STOP.
 
Asante tena ndugu ntafanyia kazi unayoniambia.

Sidhani kama huyo binti anaweza kumsingizia huyo kijana mimba kwahiyo ni vizuri zaidi wakati ukiendelea kumsaidia huyu binti, ukajaribu kufanya mawasiliano ya haraka na familia ya huyo kijana maana uki-delay na wao wanaweza kuchomoa wakamtetea kijana wao kwamba sio yeye anayehusika na huo ujauzito kwahiyo ni vizuri ukalichukulia hili suala la kushirikisha upande wa pili kwa uzito wa hali ya juu.

Nina uhakika ukimwambia mdogo wako aendelee kumchunguza basi hata nyumbani kwao huyu kijana anaweza kuwa anapafahamu vizuri tu.
 
Chauro, Msaidie huyo binti kama unaweza, ajifungue salama, na Mungu atakubariki. Meanwhile, ujaribu kuwasiliana na huyo kijana anayedaiwa kumpa mimba uone kinachowezekana hapo, ila kama hakuna, basi kubali yote tu...huwezi kujua utapata thawabu gani. Mi pia niko against na wazo la kutoa mimba
 
option yako no 2 naona ni njema,usimtoe kwa kuwa amekuwa mwema kwako na zaidi sana umekiri unamchukulia kama mdogo wako,,endelea kumsaidia na umpe nasaha zaidi za maisha,,! Fanya kwa ajili ya Mungu,bariikiwa sana
 
kaa nae,wema wako mungu,ndio ataekulipa.sisi tuna mfanyakazi ambae anaishi na mtoto wake,anaishi na mama etu,ni hodari na kazi zake.alipewa mimba na mlinzi.huyo mlinzi alivyompa mimba alikimbia.anaishi na mama tunamchukulia kama mdogo wetu,yupo kwetu tangu 2005 mpaka leo tupo nae.
 
dhambi siku zote inatendwa kwa mawazo.....maneno....vitnedo...na kwa kutotimiza wajibu...........hilo ulioshikilia la kutota mimba ndo unatakwa kulikumbatia.......mshauri azae....binafsi nimechoshwa kusikia sauti za watoto wachanga kutoka vichakani....im tired of hearing these voices crying from far away.......mwambie ajifungue huyo mtoto.....kaa nae leo jioni umweleze
 
Jamani hawa watoto hawafikiri ,yaani maisha magumu unamsaidia apate elimu ajisaidie yeye anaenda kufanya madudu
Msaidie Chauro .
[FONT=georgia, bookman old style, palatino linotype, book antiqua, palatino, trebuchet ms, helvetica, garamond, sans-serif, arial, verdana, avante garde, century gothic, comic sans ms, times, times new roman, serif]Tena tusichoke kuyatenda Mema kwani tutavuna kwa wakati wake tusipozimia mioyo[/FONT]
 
Mimi ninashauri umsaidie ila kwa njia tofauti!
Kama inawezekana umrudishe kwao, lakini mpe mtaji aweze kufanya biashara na kujitegemea. Kukaa na mtu ambaye naye ni mzazi ni kazi sana, maana utakuwa unalea watu wawili, at the end of the day, lazima utafute helper mwingine!

Akienda kujitegemea, ataanza kuwa responsible, kwani kitendo cha kupata ujauzito is irresponsible kwani nina uhakika ulikuwa ukimuasa kuhusu mambo hayo.
 
Hao watoto akili zao ni kama za panya. Mwache azae ajue nini maana ya kuzaa kwa uchungu. Akilala kwenye kitanda cha nusu futi na kuweka engle ya 360 atatia akili na PhD amemaliza. Naomba uhakikishe analea hiyo mimba na azae, heshima itarudi na ujinga hafanyi tena.

Mungu akutie nguvu huku ukifikiria ni jinsi gani umsaidie bintio.
 
...Kwanza kabisa. Nakuomba kwa hali yeyote ile, USIMUONDOE nyumbani kwako Chauro, amekukosea nini? Kumbuka, hapo ni kazini kwake, ndipo anapojistiri, na vile vile familia yako ndio ndugu zake wa karibu. Kwanini umuondoe kipindi kigumu kama hiki huyu binti ambaye ni Mwanamke mwenzako?
Chauro please, na uhakika unajua yu katika kipindi kigumu sana maishani mwake.

Naombeni ushauri wenu tafadhali.

nimejiuliza maswali mengi,napata wakati mgumu sana

1.Je nimuondoe nyumbani kwangu? lakini napata huruma ataenda wapi .kusema kweli naifahamu vizuri hali ya familia yake ni duni sana.Kumbuka mama ameshauri atoe

...Kwa hali ulivyoielezea, huyo mama simlaumu. Wenyewe wazazi hali zao ni duni sana kiasi cha kumruhusu binti yao wewe umchukue akusaidie kazi za nyumbani. Mama mzazi anahofia athari za huo ujauzito, malezi ya hicho kichanga kitapozaliwa, na maisha ya baadae ya mama na mtoto.

si support kutoa iyo mimba[/COLOR] kwakweli namuona kama mdogo wangu.

Si wazo baya Chauro, ila angalia huruma isije ponza kichwa. Utamsaidia kwa muda gani? Kumbuka, Ujauzito ni miezi tisa, na akijaaliwa kujifungua salama kuna kipindi cha maternity leave anachostahiki kupata.

Kama hiyo haitoshi, kichanga kitastahili matunzo na matibabu katika kipindi cha maisha yake. Je, utam support kwa hali na mali? Kumbuka, kulea mimba si kazi kama kulea mtoto.

...Ushauri wenu ni wa muhimu sana, nakumbuka wakati nampeleka shule niliongea nae sana sijui aliona maneno yangu hayana maana huruma iliyoingia moyoni mwangu sijui niilezeje.

NAWATAKIA KAZI NJEMA.

...Chauro, yaliyopita yamepita. Sidhani kama wakati huu ni busara kuanza kumlaumu hakusikia maneno ya Mkuu. Maisha sio kama Computer, kusema uta 'Click' >> delete files kisha 'Click' >> Restart.

La msingi katika kipindi hiki cha 'mashaka' kwake, kaa nae chini uongee nae ki utu uzima. Wewe ni Mwanamke mwenzake. Mwelezee Ukweli nini unachoona kitafuatia kwenye maisha yake. Mwambie Ukweli unaona athari gani zinazoweza jitokeza iwapoo ataitoa mimba hiyo.

Vile vile, mwambie ukweli athari gani za kimaisha unaona zitamkabili iwapo ataamua kuzaa. Huko ni kumtayarisha kiakili, ili ataapoamua kuzaa, au kuitoa...asijemlaumu yeyote.
 
yani dada ,hata sielewi wakati mwingine unaweza hata kupata mawazo mabaya unamsaidia kwa maisha yake yeye anakwenda kufanya mambo ya ajabu halafu kibaya katika vyote na dhehebu alihama akaenda kusali kanisa jingine ananiambia ameokoka mwe!

Jamani hawa watoto hawafikiri ,yaani maisha magumu unamsaidia apate elimu ajisaidie yeye anaenda kufanya madudu
Msaidie Chauro .
 
Back
Top Bottom