Nahitaji msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji msaada

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Zion Daughter, Jul 4, 2012.

 1. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Habari zenu ndugu wapendwa,
  Ninafanya utafiti kuhusu biashara ya Vyakula vya nafaka kama mchele,maharage unga n.k
  Kama kuna yeyote mwenye idea na hii biashara nitakushukuru kama nikipata uzoefu.
  Utafiti ni wa kuanzisha duka la vyakula hapa Dar es Salaam na ningependa kujua hasa soko,location nzuri ,manunuzi n.k.
  Asante
   
 2. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  is your research for academic reasons or for a business plan
   
 3. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli umeikurupukia hii habari maana alichokieleza hapo juu kinajibu swali lako embu isome kisha uondoe swali lako!
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwa sehem za uswahilini inalipa sana na ndo shm bidhaa ya chakula inatoka kwa speed kubwa
   
 5. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,957
  Likes Received: 23,631
  Trophy Points: 280
  Mkuu hebu kasome kwenye red pale kwa sauti na urudie mara mbili kama utakuwa bado hujaelewa.

  Bibie Zion Daughter kwanza nikupongeze kwa kuwa na mkakati wa kuwa mjasiriamali. Biashara ya kusubiria vimshahara vya wakoloni samtaimz ni utumwa mwingine. Labda ungeweka wazi hasa unalenga kufanya biashara ya Jumla au rejareja ili wajuzi wamwage mapwenti ya kukusaidia zaidi.

  Mungu akutangulie katika mkakati wako (Siku hizi nimeshakuwa mtu mzima)
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  unaweza kufanya utafiti wa kuanzisha duka la vyakula kwa ajili ya masters degree au hata first degree ..... ukaandika kitabu na kutoa recommendations

  ninachouliza hapa hujaelewa, je utafiti huu ni kwa kukidhi wazo la biashara au kwa ajili ya matakwa ya takwimu za kibiasashara
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Yeye anataka tu kufanya biashara na si vingine kwa nilivyomwelewa ama nae atuweke sawa
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Asante mpendwa wangu..Naona unakumbuka wajibu wako vema....
  Katika hili swali la nyongeza naomba nikujibu kuwa nataka nifanye biashara ya rejareja...Nasubiri mapweinti kwa hamu kubwa...
   
 9. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  mdizi...ninataka kufanya biashara Shine asante kwa uelewa wa haraka na wazo zuri la location...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Pouwa mkuu pamoja
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,957
  Likes Received: 23,631
  Trophy Points: 280
  Pouwa.... wasipokupa mapwenti usisahau kunidipu nikupe mapwenti ya kimangimangi.:spy:
   
 12. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Sawa.Lakn naogopa kuja huko maternity.......Hujambo lakn?
   
 13. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,866
  Trophy Points: 280
  We ni kiazi for sure na sio ndizi tena..:nerd:
   
 14. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  respect mkuu ... crystal clear nashukuru umeelewa point yangu ..... tupo pamoja

  best location ni mahali ambapo pana influx ya residential premises with an average income earners .... pia jitahidi kuangalia eneo lililo na maduka ya reja reja mengi na uuzee bei kama za tandale ...tegeta can be very good
   
 15. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Yaani wewe nahisi ulipomaliza shule waalimu wako walishukuru Mungu!
  Huelewi na haujielewi pia!
   
 16. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  dah ... wewe ni mwerevu sana ... hongera sana ... soma reply ya mleta mada kwa swali langu ... amejibu sawia na yeye ni muelewa kuliko king'asti ... sijui nani hapa hajielewi
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Take a hike,will ya?
   
 18. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  King'asti..... nishauri basi.huna ideas na hivi vitu???
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. M

  Malila JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ktkvitongoji vipya kama Kinyerezi,segerea unaweza kupiga bao, niko mitaa hiyo,mara nyingi naona wengi wanakwenda Tandika kufuata mchele, unaweza fungua duka lako huko na ukavuna sana kabla watu hawaja-kopi na kupesti.
   
 20. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,186
  Likes Received: 672
  Trophy Points: 280
  Nakushauri kuzingatia yafuatayo na utafanikiwa ktk biashara yako. Biashara ya nafaka ni nzuri kwa sababu kila mtu ni lazima apate angalau mlo mmoja kwa siku.
  1. Eneo utakalofantia biashara. Je lina idadi kubwa ya watu ambao unatarajia kuwa watakuwa wateja wako?
  2. Bei. Je bei ya bidhaa zako itakuwa na unafuu kidogo kulinganisha na competitors wengine. Zingatia kuwa uhitaji na upatikanaji wa bidhaa ndio unapanga bei ya bidhaa.., ila jaribu kuweka bei ya chini kidogo ili uuze kwa kasi zaidi.
  3. Ubora wa bidhaa. Inategemea na eneo utakalofanyia biashara yako. Kwa wale wanaojali ubora wa hali ya juu weka bidhaa zenye ubora. Pia ni vizuri kufikiria namna utakayofanya kuongeza ubora kama kuweka vifungashio vinavyovutia.
  4. Masoko. Unaweza kutafuta masoko kwenye mahoteli, hosptitali, mashule, mama ntilie kwa sababu wanaweza kununua kiasi kikubwa cha nafaka kwa wakati mmoja.
  Kwa ushauri zaidi unaweza ukani-PM
   
Loading...