Job Richard
JF-Expert Member
- Feb 8, 2013
- 3,865
- 2,176
Mimi niko kwenye biashara hii kwa miezi kumi sasa machine nzuri na imara zinapatikana sido-arusha au moshi za kichina hazidumu kaka. Kama mtaji wako c mkubwa unaweza kuanza na size 50 ya kusaga ila ya kukoboa usikubali kupewa roller 2 bali wakupe roller 3. Ila usimamizi wa karibu ni lazima
MAKADIRIO YA GHARAMA: (SIDO ARUSHA)
a.) Machine ya kusaga size 50, moter hp 20,frame, starter na mikanda yake mitatu=2500,000/=
Note: Ni vyema wakakupa moter hp 25 au 30 ingawa watakudiscourage na kukuambia ni kubwa sana. Mimi walinipa hp 20 iliungua mara 2 ndani ya miezi 2 maana nilikuwa na kazi nyingi sana. Wazoefu wanishauri ninue hp 30, tangu nimenunua mwezi wa nne haijawahi kuungua na inapiga kazi bila hata ya kuchemka
b.) Mashine ya kukoboa roller 3, frame, mikanda 3, motor hp 25 na starter=3200,000/=
c.) Wiring inategemeana na jengo lenyewe na nguzo ziko umbali gani makadirio 1500,000/= hadi 2,200,000/=
d.) Mifuko (25kg), kuchonga nembo kiwandani 200,000/= na wanaanza na order ya mifuko 400 kwa bei ya 540/= kwa mfuko wanapatikana mwanza
e.) Cherehani ya kushona mifuko, ndogo ni sh. 200,000/= kubwa 500,000/= japo ndogo ni nzuri maana hazitumii mkanda
NAKUTAKIA KILA LA KHERI MKUU
Mashine za kusaga na kukoboa tunazitengeneza ubungo external