Nahitaji msaada wa mawazo gharama za kununua mashine ya kukoboa na kusaga nafaka

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Asalaam wanaJf, muda mrefu nimekuwa na wazo la kuanzisha mradi unaohusiana na nafaka. Kwa sasa wazo lililotawala kichwa changu ni kununua mashine inayotumia umeme ya kukoboa na kusaga nafaka. Nimejaribu kuuliza huku na kule wengine wananikatisha tamaa lakini wazo langu liko palepale.

Tafadhali kwa mwenye kuelewa gharama halisi na namna ya kuanzisha biashara hii naomba msaada wako! Daima Jf ni kisima cha maarifa! karibuni sana.
 
upo uzi maalum wa suala lako ebu Google utauona hapa hapa jf

Habari za leo, sijui unataka kufunga ktk eneo gani, na ulipenda kuzalisha kwa kiasi gani, hicho ni kitu muhimu kabla ya kuuliza, waweza waisliana nami ktk inbox yangu ntakupen details zaidi sir
 
Hbr za leo, sijui unataka kufunga ktk eneo gani, na ulipenda kuzalisha kwa kiasi gani, hicho ni kitu muhimu kabla ya kuuliza, waweza waisliana nami ktk inbox yangu ntakupen details zaidi sir

Nashukuru mkuu, natakamani kufunga morogoro mjini na uzalishaji nao lenga ni kuhudumia wateja wa kawaida wenye nafaka zao pamoja na kusaga zangu na kufunga kwenye mifuko maalum kisha kuuza kulingana na ukubwa wa soko kwa kipindi husika
 
Wazo zuri hilo,lifanyie kazi.Mm nimefunga mashine za mafuta huko Namtumbo songea na wakati wa msimu wa kiangazi zinaingiza pesa ya kutosha.Sahiv najipanga nifunge mashine za umeme songea mjini.Nitasaga na kukoboa nafaka za wakulima na pia mzigo wangu.Nitaajiri vijana na watafanya kazi ucku na mchana kwa shift.
 
Ok fine, nina imani kubwa sana kwa Morogoro utafanya kazi hata hivyo jipange kukoboa mpunga na kusaga mahindi, nakuomba sasa uanze mchakato kwa ushahuri huu, sijui umeweza ku accumulate kiasi gani cha pesa isipokuwa unahitaji upate Mashine moja inaitwa SN machini 180 series hii ni multpurpose inakoboa mpunga na pia inakoboa mahindi, capacity yake ni 10tons yaani kukoboa gunia 100 is just a flaction of minutes mashine hii inapatikana China, mtambo huu upo wa aina mbili kuna complete set ambayo bei yake ni mkasi kidogo na pia kuna kuchukua processing unit tu kama utapenda, nipe mail yako ntakurushia pics na pia ntakupa contact person in china ambae ni sales manager wa kampuni hiyo inayotegeneza mitambo hiyo, thanks
 
Nunua motar 2 za Hp kuanzia 25-35,na vinu nunua toka sido.Ahsante.

nashukuru kwa ushauri, lakin umeandika kwa kifupi sana! hizo motor zinagharimu sh. ngapi na hivyo vinu vyake? tafadhali mkuu naomba uzoefu wako kamili
 
Nunua mashine ya kusaga mahindi yani dona ndio lishe inayotakiwa sasa ivi, hatuli sembe tena, pia pakia vizur ktk mifuko lete mjini.
 
Ok fine, nina imani kubwa sana kwa Morogoro utafanya kazi hata hivyo jipange kukoboa mpunga na kusaga mahindi, nakuomba sasa uanze mchakato kwa ushahuri huu, sijui umeweza ku accumulate kiasi gani cha pesa isipokuwa unahitaji upate Mashine moja inaitwa SN machini 180 series hii ni multpurpose inakoboa mpunga na pia inakoboa mahindi, capacity yake ni 10tons yaani kukoboa gunia 100 is just a flaction of minutes mashine hii inapatikana China, mtambo huu upo wa aina mbili kuna complete set ambayo bei yake ni mkasi kidogo na pia kuna kuchukua processing unit tu kama utapenda, nipe mail yako ntakurushia pics na pia ntakupa contact person in china ambae ni sales manager wa kampuni hiyo inayotegeneza mitambo hiyo, thanks

mkuu naitaji msaada wako weka mawasiliano tafadhali
 
Asalaam wanaJf, muda mrefu nimekuwa na wazo la kuanzisha mradi unaohusiana na nafaka. Kwa sasa wazo lililotawala kichwa changu ni kununua mashine inayotumia umeme ya kukoboa na kusaga nafaka. Nimejaribu kuuliza huku na kule wengine wananikatisha tamaa lakini wazo langu liko palepale. Tafadhali kwa mwenye kuelewa gharama halisi na namna ya kuanzisha biashara hii naomba msaada wako! Daima Jf ni kisima cha maarifa! karibuni sana

Nilishatoa maelezo humu kuhusu swali lako na wachingiaji wengine pia walitoa michango mingi nilitafutwa na wengi na tuliweza kubadilishana mawazo mod kama wataweza tusaidia wangeunganisha,Mimi nipo huko muda kidogo mkuu na hata hivyo nina mashine niliichukua na sijaitumia naomba ni pm ili tufanye mawasiliano ya kina,na pia naamini nitakushibisha kwa kila utakachohitaji kufaham.
 
Ndio mkuu, karibu sana

Mimi niko kwenye biashara hii kwa miezi kumi sasa machine nzuri na imara zinapatikana sido-arusha au moshi za kichina hazidumu kaka. Kama mtaji wako c mkubwa unaweza kuanza na size 50 ya kusaga ila ya kukoboa usikubali kupewa roller 2 bali wakupe roller 3. Ila usimamizi wa karibu ni lazima

MAKADIRIO YA GHARAMA: (SIDO ARUSHA)
a.) Machine ya kusaga size 50, moter hp 20,frame, starter na mikanda yake mitatu=2500,000/=
Note: Ni vyema wakakupa moter hp 25 au 30 ingawa watakudiscourage na kukuambia ni kubwa sana. Mimi walinipa hp 20 iliungua mara 2 ndani ya miezi 2 maana nilikuwa na kazi nyingi sana. Wazoefu wanishauri ninue hp 30, tangu nimenunua mwezi wa nne haijawahi kuungua na inapiga kazi bila hata ya kuchemka
b.) Mashine ya kukoboa roller 3, frame, mikanda 3, motor hp 25 na starter=3200,000/=
c.) Wiring inategemeana na jengo lenyewe na nguzo ziko umbali gani makadirio 1500,000/= hadi 2,200,000/=
d.) Mifuko (25kg), kuchonga nembo kiwandani 200,000/= na wanaanza na order ya mifuko 400 kwa bei ya 540/= kwa mfuko wanapatikana mwanza
e.) Cherehani ya kushona mifuko, ndogo ni sh. 200,000/= kubwa 500,000/= japo ndogo ni nzuri maana hazitumii mkanda

NAKUTAKIA KILA LA KHERI MKUU
 
Back
Top Bottom