Nahitaji msaada wa kisheria naona wema wangu unataka kuniponza

Karot

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
1,159
1,309
Habari za majukumu wakubwa na wadogo.

Kichwa cha habari chahusika.

Ilikua siku ya Jumamosi mnamo saa 11 za jioni nimetoka na familia yangu nyumbani kuelekea kwenye sikukuu adhim.

Kwa bahati nzuri mbele ya safari folen ikasimamishwa ya magari kupisha watoto wanaovushwa barabara. Wakati tunasubiri watoto wale wamalizike kivuka ghafla nilisikia mshindo wa kugongwa na gari aina ya Alphard ikanisukumiza mbele ambako kulikua na gari nyingine aina ya land cruser. Gari yangu ni I.S.T.

Kwa bahati mbaya gari yangu iliumia nyuma na mbele ambako mbele kulisababishwa na ule msukumo uliotokea baada ya kugongwa. Sasa alinigonga akaniomba tusishirikishe polisi twende kwa fundi wake tukamalizane mimi na yeye. Mimi nilikubaliana na ile hali, lakini cha kushangaza jana usiku majira ya saa nne nilipigiwa sim ya kwamba kuna barua yangu ya kunitaka niripoti kituo cha polisi.

Sasa nikawa najiuliza inamaana huyu mtu kaenda kutengeneza mazingira ya kwamba asinitengenezee tena gari yangu? Nilijaribu kumpigia sim alijibu ya kwamba yeye aliongea na bosi wake kwamba asikubali kosa la kutengeneza gari mbele wakati kosa lake kaigonga nyuma.

Sasa na mimi nikajiuliza inamaana mbele niliigonga mimi au yeye ndo kaja kunisababishia kuigonga gari yangu? Hapa nilichowaza ni kwamba keshaenda kutengeneza mazingira na polisi ili nikose haki zangu. Ndo nikaamua kuja jukwaa hili naamini nitapata msaada wa kisheria ili nijue pakuanzia.

Nakaribisha maswali, maoni pia kama una mawazo yoyote ya kujenga nambie kipi nifanye ili nishinde kesi hii...

NB: Shahidi niliekwenda kugonga gari yake baada ya mimi kugongwa namba zake ninazo.
 
Hata huyu naye kama gari yake ingeharibika na akahitaji kufanyiwa matengenezo, aliyestahili kubeba mzigo ni huyo huyo aliyekugonga wewe. Tatizo tu isisje ikawa walikuwa wanajuana waliamua kukuweka katikakati na kukugonga
 
Hapana hawajuani hata kidogo tulikutana kwenye ajali tu... Lakini kwa bahati nzuri yule mzee alikua na machale ndo maana akanipatia namba zake ili jamaa akiruka mtego aje anisaidie. Na tayari nishawasiliana nae aje kituo cha polisi mda niliotakiwa kufika na kakubali.
 
Ulipiga picha hiyo ajali before hamjakubaliana? Hilo lilipaswa kuwa la kwanza. Ila usiwe mnyonge, kama amekubali polisi alikugonga kwa nyuma kutengeneza nyuma na amekubali kutengeneza nyuma, hapo amejimaliza kwani kiushahidi yeye ndio amesababisha ukaharibu pia kwa mbele. iLA KAMA HUKUPIGA PICHA KUNA PROBALITY KUBWA AKAKURUKA KIMANGA.
 
Pole Sana Kwa Hiyo Kadhia
Ndiyo Maana Unakuta Mtu Kichaa Kumbe Kayatafuta Matatizo
Yaani Mlikubaliana Vema Anakugeuka!!!
 
Pole sana ndugu, kama unaushahidi wa picha itakuwa vizuri maana ndio itakusaidia Polisi huyo wa mbele pia anaweza kumruka.
 
Pambana naye kiume acha ugoigoi.

Tena ufanye haraka kabla huyo shahidi wako ajawa na mambo 'mengi' yatakayomfanya ashindwe kuja kutoa ushahidi kituo cha polisi.
 
Ulipiga picha hiyo ajali before hamjakubaliana? Hilo lilipaswa kuwa la kwanza. Ila usiwe mnyonge, kama amekubali polisi alikugonga kwa nyuma kutengeneza nyuma na amekubali kutengeneza nyuma, hapo amejimaliza kwani kiushahidi yeye ndio amesababisha ukaharibu pia kwa mbele. iLA KAMA HUKUPIGA PICHA KUNA PROBALITY KUBWA AKAKURUKA KIMANGA.
Nilipiga picha gari yangu na ya kwake pia kabla ya kuondoka eneo la tukio.
 
Back
Top Bottom