Nahitaji msaada wa kisheria juu ya hii kesi

Habari JF ,

Mpwa wangu ni Mtumishi wa serikali , katika harakati zake za maisha ,Amekopa taasisi mbili tofauti za ukopeshaji pesa kwa watumishi.

Dhamana ya mkopo wake ni mshahara ambapo kwa maelezo wanaacha kadi ya benk akaunt ya mshahara.

Kampuni moja inamdai 1,600,000 na nyingine 1,400,000 , Kilichotokea alikopa sehemu ya kwanza akaacha kadi , baadae kadi ikawa expired , akaitwa abadilishe , akatumia nafasi hiyo kwenda kukopa taasisi nyingine.

Sasa ya hii ya kwanza wamemshataki polis na aliwekwa lockup na nilienda kumtoa wiki iliyopita , na kukubaliana alipe hiyo pesa ,

Tumeenda taasisi ya pili hawataki kumlipia hili deni , na mshahara wake ni mdogo hauwez kugawanyw kwenda sehem zote.

Polisi anatusumbua sana , na anatak amkamate amweke ndani ,

Ndugu zangu naomba msaada kwenye hili shauri , Anatokaje huyu mwanangu , ukizingatia hana pesa , tumepambana hakuna kitu , Msaada tafadhali wa kisheria hapa. Ukizingatia ni mtumishi , anatokaje salama?
Ila jamaa yako mbona kazingua mwenyewe, maana alichofanya ni sawa na umekopea hati ya nyumba halafu unaenda kutengeneza tena hati nyingine ya nyumba ile ile unakopa kwingine (utapeli), halafu alipokuwa anakopa huko sehemu ya pili alikuwa anategemea nini akijua kuwa mshahara wake hauwezi kuhudumia madeni mawili???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom