Msaada wa kisheria tafadhali

jangala22

Senior Member
May 20, 2021
140
108
Habari za humu jukwaani wakuu
Niende mojakwamoja katika mada ipo hivi Mimi ni mtumishi wa serikali ,ilikuwa mwaka 2021 mwezi wa tatu nilihitaji kwenda kukopa katika bank Y bas nikipigiwa hesabu nikakubaliwa kukopa na kipindi sijakopa walikuwa wananidai Bado kiasi Cha milioni kama nne na laki kadhaa bas wao wakaja kunipa cash Kama milioni Moja na laki nne hivi maisha yakaendelea Sasa picha ikaanza sijui Nini kilitokea kwenye salary slip deni baada ya kukopa likawa linasoma hiyo bank Y wananidai milioni Moja na laki nne tukaenda hivyo hivyo Hadi mwaka 2022 mwezi wa nne deni hilo likaisha na Mimi nikasema mbona deni limeisha na Nina shida ya Hela nikaenda bank tofauti tena ilikuwa inatoa kias kikubwa na muda mzuri wa marejesho bas nikaenda pale wakanipigia hesabu kwenye hiyo bank nyingine X Kwa vile tayari Ile bank Y walikuwa hawanidai amount ikawa kubwa bas baadae mwezi wa 6 baada ya Mimi kupata mkopo kwenye bank X na Sasa mshahara ukawa unapitia bank hiyo X ghafla bank Y wakaja kujua walifanya makosa wakaingiza makato upya wakaanza tena kukata mshahara wangu na tayari kiasi walichokuwa Wanakata hapo awali nilikiunganisha kwenye makato nilipoomba mkopo bank X maana wao ndio walifanya makosa na Mimi nilikuwa sifaham mambo yao ya bank .
Nachoomba msaada wa kisheria je hii bank iliyofanya makosa yenyewe Kisha baadae kuja kuniingizia makato pasi na Mimi kujua na mshahara wangu unakuwa hautoshi naweza kuwashitaki Ili tukae mezani Ili Kila mmoja awe salama sio Ile kwangu tu ?
Naomba kuwasilisha
 
Umekipa hela unapaswa kulipa maana unasema "mlipiga hesabu" bila shaka ulijua principal loan+interest jumla deni ni shilingi ngapi na makato kwa mwezi ni kiasi gani. Kama walifanya makosa na take home ipo chini ya 1/3 ongea na HR wako maana ndiye anayeingiza makato
 
Umekipa hela unapaswa kulipa maana unasema "mlipiga hesabu" bila shaka ulijua principal loan+interest jumla deni ni shilingi ngapi na makato kwa mwezi ni kiasi gani. Kama walifanya makosa na take home ipo chini ya 1/3 ongea na HR wako maana ndiye anayeingiza makato
Ndio baada ya hiyo bank Y kuanza makato upya mshahara ukawa chini ya Moja ya tatu
 
Mkuu jifunze kuwa sensitive kwenye masuala yanayohusu pesa yako kwa maelezo yako tu uliyakanyaga tokea mwanzo pale bank Y ilipoendelea kukata hicho kiasi cha 1.4M ch marejesho kilichobaki, maana swali la msingi ni je, ulienda ofisini kwao mkpiga hesabu na loan officer wako na kijiridhisha kiasi wanachokidai au ulipiga kimya tu wajichotee wanavyotaka
 
Jamaa anataka bank y waipotezee Hio milioni 4? Sio kizembe hivo!
Bongo nyoso sana, benki wamepotezea kukata kimakosa, jamaa kapiga kimya, anajifanya hajui nini kimetokea
benki wamestuka jamaa anataka kuwashitaki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom