Hilo la mzazi kupishana kauli na ofisa halina sana mashiko. Hujasema kinaga ubaga kwa nini mzazi alikwama.
Uraia wako ukoje, first and foremost.
Mzazi akueleze ukweli kama kuna uzembe ulifanyika kuhusu nyaraka zako na zake za uzao, majina, ubini , elimu, kughusi taarifa zozote za nyuma na mmetokea pori gani, liko nchi gani.
La mwisho, wanasema uhamiaji ni wala rushwa, lakini kwa experience yangu, pamoja na ula rushwa wao, wao wako makini sana na kazi zao kuliko NIDA, RITA, NECTA na TRA wanakotoa leseni za kuendeshea. Kwa hiyo ukienda Uhamiaji na makaratasi fyongo kutoka taasisi zingine Uhamiaji wanatambua mara moja uozo wa kilichomo humo. Watakwambia pa kurudi kurekebisha halafu wataomba cha juu kulishughulikia jambo lako utakapowarudia.