Nahitaji mawazo yenu wakuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji mawazo yenu wakuu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Manyanza, Feb 22, 2012.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Heshima zenu wakuu?
  nilipata dili katika kampuni hii
  Perdue Farms, hawa jamaa walikuja hapa Tanzania kutaka ku invest lakini mpaka leo ni zengwe kutoka wizara ya Mifugo..
  nimeamua kuja na wazo jingine wakuu nahitaji ushauri wenu na mawazo yenu....

  Kwa kipindi hiki nimekua nikiishi Zanzibar, katika pita pita zangu niliamua kufanya utafiti karibu miezi minne kuhusu sekta ya Utalii... Utalii ni moja ya tegemeo kubwa sana la mapato katika serikali ya Zanzibar.

  Watalii wanakuja hapa kwa ajili ya mapumziko na kutembelea baadhi ya sehemu za kihistoria, nilichojifunza ni kwamba hawafurahii kabisa shughuli za kitalii zinavyoendeshwa hapa Zanzibar, kwa sababu hata wale tour guide wakati mwingine anakua anamtembeza na kumwelekeza mgeni baadhi ya mambo lakini moja kwa moja anaonekana anadanganywa na anakua hana jinsi inabidi akubali matokeo, nimeona wageni wakienda kwenye visiwa kam Prison Island yaani nothing special kabisa kwa mgeni kwa sababu kuna baadhi ya wageni wanaijua historia ya Zanziba lakini hawajawahi shuhudia tu yale maeneo.. lakini ukweli na Historia ya hayo maeneo anakua anaijua vizuri lakini hao Tour guides huwa wanawapiga kamba..
  na vilevile hakuna kitu kipya anachokipata mtalii hapa Zanzibar zaidi ya Kutembezwa kwenye maduka ya vinyago, Ngome Kongwe na Bustani ya Forodhani .
  Lengo langu: nime plan kuanzisha Gallery hata kama sio kubwa sana lakini ni sehemu ambayo itakua tofauti kabisa na Gallery nyingine kama Makumbusho ya Taifa na nyinginezo..
  nilichopanga ni kutafuta Picha za maeneo na sehemu mbalimbali zinazoonyesha maajabu ya Tanzania, najua kuna maeneo mbalimbali ambayo wageni wanapofika inakua ni ngumu kuyafikia au kupata taarifa lakini mimi nimeamua kuanzisha hiyo Gallery ili kufanya hiyo kitu...
  Naomba ushauri wenu wadau:-

  1. Eneo la Kufanyia hiyo kazi nimeshapata ni sehemu moja nzuri sana hapa Stone Town ni ina eneo la kutosha kabisa
  2. Naomba mnisaidie kunifahamisha baadhi ya maeneo ambayo yana vivutio ili niweze kufika pale kupata na kupiga Picha na maelezo husika ya eneo.( nahitaji sana msaada wenu wakuu maana najua hapa JF kila mmoja yupo sehemu mbalimbali ya nchi na kila sehemu kuna vivutio au kuna kitu ambacho ni tofauti kinachoweza kuwavutia wageni hata watanzania pia..
  3. vile vile naomba kama kuna ushauri mawazo na michango yenu naihitaji sana wakuu

  NB: kuhusu mbinu na mikakati ya kuendesha hii shughuli nitazieleza baada ya kufanikiwa kufika baadhi ya sehemu ambazo mtakua mmenitajia..

  Asanteni sana wakuu, Idumu JF..

  its me Manyanza..
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  ,Mkuu Aidia yako ni nzuri sana, il mimi nitakupa adivice kidogo,

  Mkuu sekta ya utalii ni kweli unavyo sema imevamiwa sana utakuta kampuni in tour guide mzungu, hapa ndo ninapo choka mkuu, ni kama uemde kufanya kazi za kutembeza watalii china, wakati wewe ni mzaliwa na umekulia bongo,

  - KUHUSU WAZO LAKO
  1- Mkuu wageni wengi hasa watalii wanapenda kuona kitu in reality mkuu, mfano picha ya mlima kilimanjaro waisha iona huko kwao na kwenye mitandao but wao hutaka kuona mlima live kwa macho yao,

  - Na hata watalii wengi wano kuja huku unakuta simba wameisha muona kwenye zoo but wao wanahitaji kumuona katika maizingira yake ya asili na si kwenye zoo.

  WANAPENDA SANA VITU LIVE KATIKA UHALISIA WAO, KWA SABABU PICHA ZA MIT, WANYAMA WOTE WA TANZANI ZIKO HUKO KWAO ZINAUZWA NA KWENYE MITANDAO ZIPI SANA BUT WAO WANATAKA KUONA UHALISIA WA JAMBO LENYEWE TENA KWA MACHO,

  NA NDO MAANA WANAVYO PANGA KUJA KUTEMBELEA TANZANIA WANAKUWA NA LATIBA YA SEHEMU WATAKAZO ENDA,
  Swala la maduka ya Vinyago, huwa kwanza halipo kwenye latiba zao na pale huenda kufanya GIFT SHOPING ZA KUWAPELEKEA WALIO WAACHA HUKO KWAO

  Ila mkuu unaweza try tu si vibaya kwa sababu hata mfumbuzi wa balbu alijaribu mara 10,000 kwa nini sisi tusijaribu
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Thanks mkuu, najua mimi ninachotaka kufanya ni kitu tofauti kabisa, nataka kua na Gallery inayojumuisha picha ya vitu mbalimbali na Historia ya vitu husika, lets say vyura wa Kihansi, nikipata picha nzuri ikawa na maelezo ya kutosha itamfanya mgeni awe na shauku ya kufika pale na kama atakua tayari kwenda pale nita organize kila kitu kwake, ikiwemo Usafiri,Chakula na malazi.
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mimi nisha kuelewa but ninacho sema, hawa watalii kabla ya kuja huku wana information za kutosha wao wana kuja kudhibitisha tu,

  Chukulia mfano wa Mapiramid ya Misir yale ukiingia kwenye miatandao kuna picha zake na maelezo ya kutosha kabisa kuhusu hayo mapilamid, but still yale mapilamidi yanavutia watu wengi kwa sababu wanataka kuja kuona real Pilamid,

  Kuhusu kuwa unaarenge safari za hao watalii, hapo labuda uniambie unataka kufanya kazi za Tour Operater nitakuelewa au Tour agent,

  Mkuu kumbuka kwamba wageni wanapokuja Tanzania unakuta wameisha panga ratiba yao ya wapi waende na kwa siku ipi, kwa kushirikiana na tour operater wanakuwa tiyali wana ratiba, Ratiba hawaji kuipangia huku kwamba sasa twende Zanzibar kesho sijui twende wapi,

  Na kingine ni kwamba kampuni husika ndo huwa inajukumu la kuwapeleka huko kote, Mfano kama wageni ni wa Leopard tours , Leopard ndo atakuwa na jukumu la kumsafirisha kwenda Hifadh zote anazo taka kwenda, ukiacha Zanzibar ambapo mara nyingi lazima kupanda Meli au Ndege,

  Mkuu labuda fanya hivi uwe na website yako na ujitangaze vya kutosha kwamba wewe unaprovide Picha na ikibidi unakuwa unawauzi baadhi ya picha hizo
   
 5. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu Komandoo,
  najua mwanzo utakua ni mgumu, labda lets say Makumbusho ya taifa mgeni anapoingia analipa dola 3, na anachokipata ndani ya yale makumbusho ni kitu cha kawaida saana, na kama tunavyojua Historia iliandikwa na Wageni na wageni wanaijua historia kuliko sisi tunavyoijua...
  Labda lets say nikipata Information za kutosha kuhusu Mapango ya Amboni na picha halafu mgeni akaja kwenye Gallery yangu akaona ile kitu anaweza akawa na interest nayo akapanga kuona pale na mimi nitakua naratibu kila kitu na sitataka kufanya kazi ya Tour Agents lakini nitakua nadili nao mimi nitakua nachukua Commission yangu..

  na kuhusu ishu ya Kuwauzia hizo Picha ndio nitakua nauza Pia, nina mpango wa kutafuta Kamera ambazo ni hii Quality kwa ajili ya kuchukulia hizo Picha na nitakua tayari kujifunza jinsi ya Kupiga Picha kiustadi zaidi, najua humu kuna watu
  kama Ndida na Eqilypiz, watanisaidia sana katika hili la kupiga na kupata picha zilizo bora...
  Mpango wakua na WebSite pia ninao, na ninachokiongea hapa mkuu nimeshakifanyia utafiti na ninaelewa japo sio sana kuhusu shughuli za utalii zinavyofanyika hapa Zanzibar.

  All I want for this time, ni yale maeneo na Sehemu ninazoweza pata Information na picha kwa ajili ya kazi yangu..
   
Loading...