Pole sana mdogo wangu, kikubwa hapo kwanza achana na huo mchezo wa kujichua kabisa kama bado unao Ili kuimarisha afya yako ya uzazi.
Lakini pia kimtazamo tu unaonekana bado kuna chembe chembe za utoto zinakusumbua hivyo kufikia hatua ya kufuata mkumbo, sasa inabidi ufanye yafuatayo ili kuweka mambo sawa..
Hakikisha unachuja katika hao marafiki zako unaowaamini jaribu kutafuta wale ambao unaona wana umuhimu zaidi ndio unapaswa kushirikiana nao zaidi ili kuepusha mambo yasiyo ya lazima ikiwemo la kufuata mkumbo.
Pia jiweke mbali na mambo yatakayo ifanya akili yako iwazie zaidi maswala ya wewe kushindwa kujiongoza kihisia mfano acha stori za kijinga na marafiki wasio kua na maadili mazuri, acha kuangalia video za ngono kama unapendelea.
Pia jitahidi kutafuta marafiki wakike ambao unahisi ni wa rika lako pia wenye upeo ili ujenge nao mazoea ya kupiga story na kua karibu nao kiurafiki zaidi muwe munashauriana mambo mbalimbali,hii itakupa uzoefu pia itakujengea hali ya kujiamini na utajikuta unapata shauku juu yao
Pia hakikisha huyo msichana ulie nae unakua nae karibu na usiwe nae kwa ajili ya sex tuu, bali inabidi awe kama rafiuweujitahidi umtumie kama suluhisho la matatizo yako. Jitahidi kuwa nae karibu zaidi huenda ikasaidia, kua romantic sana kwake huenda ikasaidia.
Asante pole kwa matatizo.