Nahitaji maombi!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji maombi!!!!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mvaa Tai, May 10, 2011.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Jamani kwa watu wa imani zote naombeni msaada wa maombi yenu. Miaka ya hivi karibuni kuna roho ya chuki mbaya imeibuka moyoni mwangu dhidi ya binaadamu mwenzangu.
  Kabla ya Mkapa na kikwete kuingia madarakani nilikuwa na tabia ya kupenda kufuatilia hotuba za Rais Ali Hasan Mwinyi kila anapohutubia taifa na wakati mwingine nilikuwa nasitisha shughuli zangu ili nimsikilize rais, baada ya kumaliza mda wake akaingia Mkapa, huyu mtu alijiwekea utaratibu wa kulihutubia taifa kila mwisho wa mwezi ni katika kipindi hiki iliibuka shauku kubwa zaidi ya kufuatilia hotuba za viongozi wa nchi kiasi kwamba hata mimi nililazimika kuweka katika ratiba zangu ilimradi tuu nisiikose hotuba ya rais hata moja, siyo kila alichohutubia Mkapa nilikipenda lakini nilikuwa nafurahishwa sana na namna alivyokuwa anapangilia vizuri hotuba zake na kuzi-address hoja kisomi.
  Alipoingia Kikwete madarakani niliendelea kufuatilia kwa karibu hotuba zake za kila mwezi, tofauti na miaka ya nyuma taratibu nikawa sivutiwi kuendelea kusikiliza mpaka hotuba yake iishe, baadaye nikawa simsikilizi hata kama nipo karibu na TV au redio, hii hali iliendelea kwa mda kidogo, mbaya zaidi katika kipindi hiki cha kuanzia 2011 tatizo limekuwa kubwa zaidi kila nimsikiapo rais aidha nitazima Tv au nitalazimika kubadiri stesheni, na mahala nisipo na mamlaka ya kufanya hivyo nimekuwa nalazimika kuondoka eneo hilo. Hili tatizo linazidi kuwa baya zaidi kwasasa hata nikimsikia mtu anazungumzia habari zake huwa nakasirika, najua tatizo kubwa laweza kuwa ni uwongo wake alio ufanya katika kampeni akiwa anawania kuingia madarakani kwa mara ya kwanza, pale aliponidanganya “maisha bora kwa kila mtanzania” nikajikuta nampatia kura yangu bila kujua kwamba huyu mtu ni wa mzahamzaha”. Naombeni msaada wa maombi roho yangu ijirudi kidogo kwa huyu mtu
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :happy:

  God will honor your request....he bestows to the humble and fill them with His delights......
   
 3. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana.
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  kilicho kuingia wewe ni roho ya utambuzi wala si ya chuki
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Bora wewew unamchukia tu, wengine wanatamani kuvomit!
   
 6. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #6
  May 10, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora uache kumsikiliza hadi hapo ukijihs furaha.
   
 7. x

  xman Senior Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu pole sana, jitaidi kukwepa kusikiliza hotuba zake na mabo yote yanayomwusu ikiwa haitakusidia msikilize lakini mchukulie kama kiongozi wa kawaida sana ambaye ufanya mambo kwa mazoea so chochote atachoongelea do not take it seriously na sio wewe tu mwenye hilo tatizo wapo wengi ambao wamemchoka wanaomba ata hiyo miaka minne iliyobaki ihishe kesho, uchaguzi mkuu mpya uje!!!!
   
 8. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Nadhani hii itanisaidia
   
 9. w

  warea JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unahitaji kubadilika,
  1. Badili "SIMTAMBUI JK KAMA NI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA" kuwa "Namtambua JK KAMA NI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA"

  2. Huwezi kubadili moyo wako, ila unaweza kubadili nia (mind) yako. Mungu hawezi kubadili nia yako ila ukiibadili ataugeuza moyo wako umpende Mungu na JK


  3. utakuwa mwanakondoo
   
 10. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu
  usiangalie wakati anahutubia kila mwezi
  usisome magazeti yenye taarifa zake
  kama ............me

   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ni wazo zuri sana, ngoja nisifanye haraka kwanza, nalifanyia kazi
   
 12. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #12
  May 10, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ishindwe na ilegee hiyo roho maana nimegundua inaambukiza kwa njia ya Hewa. Cha kunisikitisha zaidi ni kuwa sijui lini na wapi lakini ushaniambukiza zamani tatizo lako. Tena kwangu ni baya zaidi. AGHRRRRR...
   
 13. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  nadhani unisamehe kwani ntakuwa ni mimi nimekuambukiza! Mimi nilikuwa na hasira tangu alipopitishwa 2005. nilijitahidi kuwaeleza nilioweza kuwa hapa tumekula wa chuya. hamna kitu hapa. sikusikilizwa na nilipuuzwa kwa sababu ya propaganda zake alizokuwa kajipanga nazo. lkn i could see kwenye macho yake kuwa hakukuwa na heri yoyote mbele kwa nchi hii. hata walipokuwa wakisema ni chaguo la mungu nilishika kichwa. kwamba hivi watu wote hawa hawawezi kuuona ukweli, mbona unaonekana kwenye macho yake kwa wazi kabisa.

  sikuwahi na sijawahi kumpa kura yangu. nashukuru 2010 wengi walikuwa wamegundua ukweli ambao nilishauona enzi na enzi. na kweli legitimately sio rais halali wa nchi hii, ingawa constitutionally he is (pity...!)
   
 14. A

  Anyambilile Member

  #14
  May 10, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo mengine falsafa yako nimeeipata mkuu,Kwa kifiupi ni kuwa blabla zimekuwa nyigi sana kinachoongelewa si ndicho kinaccchotendwa pole sana ndiyo yaliyofanywa na wananchi na kuchakachua .
   
 15. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Pole sana ndugu, hili tatizo lipo kwa Watanzania wengi lakini mimi ninahitaji maombi ya haraka, haiwezekani kumchukia binadamu mwenzangu kiasi hiki kwani yeye alipenda awe muongo? si ni maumbile tuu
   
 16. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  At least sasa nahisi ugonjwa wangu ni common, hivyo matibabu yaweza patikana. duu nilianza kuchanganyikiwa
   
 17. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pole sana mkuu. Ulisoma seminary? Unaimba kwaya kanisani?
  Huo ugonjwa ulianza kuambukiza mwaka jana mara baada ya Padri Slaa kutangaza kugombea urais!
  Ila ni wa msimu utaisha taratibu!
   
 18. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ahsante ndugu yangu, binafsi nilikuwa sifahamu kama " Padri Slaa kutangaza kugombea urais!" ingeweza kuniletea matatizo kiasi hiki maana akiwa alhaji Ali hasan mwinyi madarakani sikuwa na matatizo naye na nilikuwa namsikiliza vizuri tuu kama rais wa nchi, iweje ustaadhi Kikwete nimchukie?, nadhani hii ni serious case kuna haja ya kujikita zaidi katika maombi.
   
 19. Mwana CCM.

  Mwana CCM. Member

  #19
  May 10, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeifuatilia vizuri thread ya mtoa mada nimejizuia kuchangia haraka maana inahitaji uwezo mkubwa kuitafakari kabla hujachangia lolote, kwanza imekaa kama utani. Naomba nisichangie lolote
   
 20. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  WAKUU!
  kama ni maombi basi mimi nahitaji maombi zaidi yako mkuu!
  mpaka wanaovaa tshet za pic ya jk namchukia!
  NAMCHUKIA YEYOTE ANAYEMFAGILIA HUYU JAMAA!
  NIOMBEENI PIA NDUGU ZANGU!
   
Loading...