Neek Conqueror
Member
- Sep 10, 2018
- 9
- 12
Nakazia asome huu mstari. 1Yohana 4:4Tatizo linalokusibu ni nini? Je ni uchumi, elimu, ugonjwa? Imani yako ndio itakuponya. Kiukweli kupona ugonjwa kwa njia ya imani sio jambo jepesi inabidi uwe na imani haswaa,
Mama Helen white anasema unapokua kwenye maombi au Mfungo ukiombea jambo Fulani ona ilo jambo limeshaisha, usifikirie kuhusu ukubwa wa tatizo fikiria ukubwa wa Mungu juu ya ilo tatizo, usisubiri upone completely ndio ujue umefunguka anza kupiga hatua na kua na furaha (tatizo hujasema shida ni nini yaweza kua ni personal).
Lakini inahitaji uwe na imani haswaa au nenda kwa Mwamposa maana kwenye imani tunasema ukiona jambo linakua gumu kwako na wewe unganisha nguvu za watu wengine.
Habari za muda huu?
Nahitaji msaada wa maombi ili Mungu anisaidie, napitia kipindi ambacho sielewi nifanye nini.
Nimeomba nimefunga lakini sioni badiliko lolote nahitaji msaada sana katika hili maana sina option nyingine kabisa.
Nikipata msaada wa mtu mwenyewe moja kwa moja ntashukuru sana awe mchungaji, mtume, nabii au muumini wa kawaida tu maana naamini Mungu anaweza kumtumia yeyote. Anaewiwa kunisaidia mzigo huu karibu.
Tafadhali msinielekeze namna ya kusali ama vipi maana nimeomba usiku na mchana inawezekana sijaomba vizuri kiasi cha kufikia kiwango cha kupata msaada nnaohitaji lakini nilipofikia nimechoka sasa siwezi tena mwenyewe nahisi/naamini nahitaji msaada wa watu wengine ili kuinuka hapa.
Asantee natanguliza shukurani.
Kweli kabisa. Tumempuuza sanaHuyo alitaka kuharibu mjadala. Mwenzie ana shida yeye analeta mizaha akitegemea ataungwa mkono na baadhi ya wanachama humu badala yake wamempuuza.
Unakosea unaposema umeomba lakini huoni badiliko lolote. Ukisema hivyo maana yake ni kuwa unampangia Mungu kutoa majibu! Ukiomba, subiri, Mungu anajua muda wa kukujibu. Lakini pia yawezekana ameshakujibu, ila wewe hujaona kwa macho ya kibinadamu.Habari za muda huu?