Nahitaji logo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji logo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Tabutupu, Dec 31, 2011.

 1. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  Wakuu nahitaji logo ya kampuni .
  Naomba wenye ujuzi huu wanipe quatation;
  thanks
   
 2. Buggy

  Buggy JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mie na-design kwa laki 2.
   
 3. Ibang

  Ibang Senior Member

  #3
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu habari yako...
  wasiliana nasi tutakufanyia design ya logo uipendayo kwa gharama nafuu kabisa
  tucheck kupitia
  Ibang Net
  tuwasiliane kupitia

  info@ibangnet.com
  +919980047826
  +255754382711
   
 4. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu usipoteze muda wako kutafuta Madesigner wa kuchora papa na nguru... No offence lakini sikushauri uwasiliane na hao Ibang hapo juu... (Siwajui hawanijui) na wala siko hapa kumuharibia mtu biashara yake, naongea professionally... Nimevisit Website yao, ni pure copy and paste ya templete ambayo nilishawahi kuifanyia modifications miaka minne iliyopita wakati najifunza neating codes...
  Hawa jamaa logo wao wenyewe hawana (wameweka text ndani ya duara la blue)... Wakuu hebu fungueni link yao hapo juu muone...page zao zote zinafanana, pembeni kuna testimonial chini, mission/vision juu... Come on guys... Hebu umizeni vichwa kabla hamjaanza kuwaza pesa... And this Is what I said in my previous posts kwenye thread ya biashara ya webdesigning and development...
  Kuna mambo mengi sana watanzania tunayakurupukia na kujifanya tunayajua kiasi cha kujiita experts, lakini ukweli ni kwamba hatujui na wavivu wa kufanya kazi kwa bidii (baadhi yetu)... Inakera sana kuona watu wanatumia templates for business use... Au kwakuwa wazee wa copy right hawatuangalii huku africa???

  Well, back to the logo design... Nakushauri uwasiliane na Homepage : Spearhead Branding huyu jamaa ni proper expert na kazi zake zipo kwenye website yake hapo juu... Ila nikutanabahishe tu... He is not cheap...
  Kumbuka a logo is your representation of your company... It should be done right... Hizi logo za laki mbili au elf 50 ni so cheap kwa taswira ya kampuni...kumbuka you are buying ART na hata siku moja any artistic work is never cheap...
  Kama utahitaji designers kutoka nje ya tz, ingia 99designs | Logo Design, Web Design and More. Design Done Differently. au search google... Kwa bahati mbaya brabdstack imefungwa, ningekulink na proper designers...
  NB: wakuu wa ibang, take this as a positive criticism... Msione nimekupeperushieni mteja, by the way, its up to him to work with whoevr he/she likes...I just had to get this crap out of my chest...
  Mimi ni Designer pia, ila sina muda kwa sasa so I'm out.
  Kama unataka inspiration kwenye logo designs, tembelea Logoholik - Logo and Corporate Identity Creation uone kazi za ukweli hapo...
   
 5. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  mkuu kwa hiyo unataka kuniambia makampuni kama sony, panasonic, hitachi, google hayana logo?? Kisa yameandika tu maandishi au wewe unajua logo uone symbol ndio unaiita logo??
   
 6. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Sasa kama vipi ........ni PM nipe kazi ya kampuni na details nyingine muhimu then ntakupa quatation, halafu siku nyingine tuma kule jukwaa letu la Technology.
   
 7. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuhusu madai yako juu ya hawa jamaa wa Ibangnet sina cha kusema. Ila kuhusu wa-Tz kuwa wavivu na kutumia templates za watu then wakajiita experts nakubaliana nawe. Hii tabia imesambaa sana. Kuna mtandao wa videocopilot.net unaofundisha motion graphics na visual effects, basi wabongo wanacopy na kupaste (bahati mbaya/nzuri) jamaa huweka na templates kabisa. Matokeo yakje kazi zinakuwa zinafanana sana. Aaaah, haya.
   
 8. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ja!! thats right Sony dont have a logo!! they have a brand Name!! Upo hapo, Get the definition of Logo then ask!! ( siku offend ndugu tunaelimishana tu!!) and check it well if you happen to pass Sony head quaters you will find a Flag outside! I hope you dont need explanations for that!
   
 9. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  thanks kwa kunielimisha
   
 10. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wakati napost nilitaka nikupe mifano ya logo hizo ambazo ni brand names kama sony, samsung microsoft, dell, hp, toshiba nk...(Hizi si logo par se) kama alivyoeleza mkuu hapo juu, a logo is not a brand name, but it can be part of it...
  Katika sanaa ya uandishi kuna kitu kinaitwa font design and development... Makampuni tajwa hapo juu yamelipa hela nyingi sana tena sana kwa watu wanaotengeneza font ili za kwao ziwe tofauti kabisa na font yeyote ile, wanaporepresent their brands, ndio maana zinastand kama taswira mama ya kampuni zao... Hautokuja kuona kampuni yeyote kubwa inatumia arial, verdana, comic sans, calibri etc kama fornt watakayoandika just a simple text ili iwe brand name yao....pitia hapa utaelewa http://www.leawoodward.com/whats-difference-between-logo-brand/
  Hii ni elimu nyingine mkuu inapaswa iresearch, sasa kama mtu unataka logo yako iwe simple and neat in a text format, jiandae kutafuta type designers wakutengenezee font yako uitumie kama logo in an artistic way, na utahitaji consultants wa maana kukupa ushauri...
  Lakini kikwetu afrika, tunaenda tu ile bora liende... Professionalism ni muhimu sana kwenye hii sekta inayokua haraka na kwa kasi kubwa...hebu angalia logo ya Jamii Forums utoe japo credits kidogo...it stands very well na ina coordinate visually na what's in the forums...kama unataka kufahamu zaidi ingia www.fontsquirrel.com uone tofauti ya font za bure na za kuuzwa... Soma na makala mbali mbali za madeveloper online using google search...
  Nb: by the way, google's logo sio just text mkuu, ile ni art, jinsi rangi zilivyochanganywa pale ni heshima kubwa sana kwa aliyehusika na kazi...also, google wana logo yao yenye letter g ndani ya box na imezungukwa na rangi zao...
  Nb2: colours in your logo should be your house colours, yaani rangi utakazokuwa unatumia kikampuni, from ur office, documentation, letters, b.cards etc, sio una logo ya blue, halaf website yako nyekundu, letter heads zako kijani, business card pink...angalia sites kama littlewoods.com, asda, tesco, jpmorgan, vividiti, themeforest etc... Zitakupa mwangaza.
   
 11. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Ndio maana siku zote ninasema naipenda sana jamii forum hapa ni zaidi ya chuo kikuu
   
 12. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #12
  Jan 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  MKUU HESHIMA SANA.
  UNACHO SEMA NI KWELIKABISA, NA KAMA KUNA MTU ATAKUJA KUPINGA BASI ATAKUWA KICHAA.

  - Cheki hata mfano waLOGO ya UN ni ya blue na kila kitu chao ni cha blue, ukiingia ofisini utakutakuanzia masofa ni ya blue, kalamu, trey na kazalia

  -Kwa Sisi ni kwelikabisa, utakuta mtu ana logo ya Njano lakini ukiingia Ofisini mwake unakutanana mapazia ja Kijani, viti vya Blue na kazalika
   
 13. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #13
  Jan 1, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mkuu Doltyne,

  Katika post zako kwenye thread hii nakubaliana na wewe kwa point ulizotoa. Hapa bongo kitu kinachoitwa professionalism bado sana. Watu wengi wanaingia katika fani kwa lengo la kutafuta kitu cha kuweka tumboni, na sio kutoa ujuzi katika eneo husika. Kwa kifupi, katika utendaji kazi bado kuna blah blah nyingi na watu wetu wanaaojiita "wataalam" wengi hawajui kwa kina kuhusu fani zao.

  Nazungumza kama mtu ambaye nafanya logo design na website development, so nina uzoefu mzuri katika hili. Jambo moja ambalo ningependa kulizungumzia, ambalo umeligusiia katika post zako, ni palle ulipozungumzia matumizi ya template. Kwa mara kadhaa mimi pia nimeshawahi kutumia template katika baadhi ya kazi za wateja - lakini hata wateja wenyewe walikua na ufaham kwamba website yao ilikua ni customized template.

  Wakati mwingine si tatizo kutumia template, ila ni kwa nini unatumia template hapo ndipo kunamtofautisha professional and non-professional designer.

  Mwamko wa website na logo development, au kwa ujumla corporate branding hapa bongo ni mdogo sana, na watanzania wengi (wateja) hawaoni umuhimu wa kutafuta professional consultation kwenye eneo hili. Hili linaweza kuchangiwa na mambo mengi ikiwa ni uelewa mdogo wa elimu ya biashara na marketing na sababu nyingine nyingi za msingi ambazo nisingependa kuzizungumzia kwa kiundani kwa sasa.

  Hivyo basi utakutana na wateja wengi wanaopenda kazi zenye "professional grade" lakini wana budget ndogo sana. Kwa mfano, mteja anataka website ambayo budget yake roughly ni USD 2,500, lakini yeye ana USD 500. Katika mazingira kama haya, ili mteja apate anachokitaka bila wewe kuumia, unaweza kumshauri ku customize template ambayo inarandana kwa ukaribu na kitu anachohitaji. Vinginevyo ni vigumu kufanya kazi kwa budget hiyo alafu uumple professional output.

  Cha msingi, kutumia template haimaanishi kutokuwa professional. Unaweza kutumia template kama inalazimu, au ni njia nzuri zaidi baada ya kufikia makubaliano kati yako na mteja.

  Mwisho kabisa isingependa kulalumu upande mmoja bila kuangalia matatizo katika upande mwingine. Kufikia hadhi ya kuwa professional sio kazi ndogo. Inahitaji dedication, time na gharama za kifedha pia - kama kununua vitabu, kwenda shule na kadhalika. Kuwa "professional" ni investment na hakuna mtu ambaye yupo tayari ku invest kwenye biashara isiyokuwa na soko, au yenye soko dogo lisilovutia.

  Kutokuwa na "market" au kwa lugha nyingine "kutokuwa wateja wa kutosha (hapa nazungumzia makampuni ya kati) ambao wanahitaji professional consultancy)" inachangia kutokuwa na professionals kwenye fani mbalimbali hapa TZ, na sio kwenye website development au corporate branding peke yake, bali hata kwenye software development and upande mwingine wa ICT. Hata kwenye movie production, tatizo ni hili hili.

  Ni watu wangapi wapo tayari kununua muvy yenye hadhi kwa TZS 30,000+? Je, soko la muvy lipo la kutosha?

  Ni watanzania wangapi nawaotazama "quality" na sio "price"? Watanzania wengi tupo tayari kuchukua kazi/kitu cha bei rahisi hata kama hakina quality, na hili linachangia sana kukosa watu ambao unaweza kuwaita "professionals" kwenye fani zao ambao wataangalia sana kutoa quality output na sio low price na blah blah nyingi.

  Watanzania wenye uwezo wapo wengi, ila hali halisi ya mazingira kwa namna fulani inachangia kupoteza vipaji vingi hapa nyumbani.

  Ram
   
 14. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #14
  Jan 1, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  am breathless and speechless too, yote yaliyosemwa ni UKWELI MTUPU na ni ELIMU TOSHA kwa sisi wengine
   
 15. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ndugu umeelezea vema sana upande ambao mimi sikuweza kuuzungumzia kwa sababu maalumu...
  Tukiangalia matumizi ya template tanzania, yamekithiri mno... Ndio maana nina wasiwasi na ukuaji wa tasnia hii na athari zake hapo mbeleni... Sababu zote zikitiliwa maanani, ukweli ni kwamba, Watz tunapenda vya gharama ndogo au bure kabisa... Tuna sifa mbaya ya kutoheshimu taaluma za watu na kufikiria muda watu hao wanaotumia ili kufikia malengo ya kazi husika... Kuhusu gharama ya kazi, kweli bei za wateja ni ndogo sana, tena zinakatisha tamaa... Mimi ushauri wangu, badala ya kutumia template za watu online, kwanini developer/designer usikae miezi mitatu ukatengeneza zako from scratch ukaziweka kwenye stock yako wateja wakija ukawapa hizo na kuwaambia ulichofanya???
  Tatizo hapa si kutumie template, bali ni za nani zinatumika na kwa haki ipi miliki? Kumwambia mteja kuwa hii nimechukua sehemu labda kwenye torrent akakubali, hakumaanishi kuwa aliyetengeneza karidhia kazi yake iibiwe... Hizi ni zile za kuiba, lakini za bure hakuna tatizo...
  Tukitaka tufike kwenye level ya south africa, inabidi tukubali kuendana na mabadiliko ya tasnia nzima ya www, pia wateja waelimishwe na ikiwezekana waambiwe kwa gharama hii sitoweza kufanya kazi yako kwa sasa kwa sababu kadha wa kadha...
  NB: Kucopy kazi za watu Kunaua uwezo wako wa kufikiri na kubuni. Matumizi mazuri ya kazi za watu ni kusoma codes na kujifunza arrangements...
  Nb: kama mtu unataka kipato cha kueleweka, post kazi zako halisi kwenye online marketplace kama themeforest ,envato au 99 designs, fungua ac nbc au crdb au upate debit mastercard na jiunge na paypal uweze kupokea malipo na kuyaingiza kwenye ac zako kwa kutumia electronic cards...
  Kuna watu wanajua wanamake up to 100,000 usd per year kwa kuuza template online...template inauzwa dola 35 lakini inakuwa downloaded mara elf6... You make the maths...sio lazima uwe na mteja physical uweze kupata pesa... Cha muhimu ni competency.
   
 16. DullyM

  DullyM Member

  #16
  Jan 1, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mbaya zaidi sisi watanzania pia tuna mtindo wa kudharau kazi za watanzania wenzetu!! hata zikiwa proffesionnal vipi! mtu akitajiwa bei ya kutengeneza logo atasema jamaa wezi wanataka pesa nyingi!! lakini mtu huyo huyo atalipa double eti kwa sababu kuna mzungu katoka #&"*#*# katengeneza!! Tutafika kweli!?!?!
   
 17. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #17
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nakuunga mkono ndugu yangu, tena sometimes hata sio mzungu, kampuni za nchi jirani tu hapo zinacharge pesa za ajabu kwa kazi ambazo hapahapa zingefanyika kiweledi kabisa...
   
 18. +255

  +255 JF-Expert Member

  #18
  Jan 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Mi sina ujuzi kabisa wa hz web designing, ila nimeipenda sana web ya "kipanya.co.tz" sidhani ka itakuwa designer alii copy maana nimeona art ya mwandiko wake kbs kipanya kwny hz template
   
 19. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #19
  Jan 1, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Doltyne,

  Thanks mkuu kwa nyongeza.

  Kwa suala la ubora, hususani katika fani ya website development, nadhani taasisi za serikali zingejaribu kuwa mfano katika kuzingatia ubora wa tovuti zao, pengine hii ingechangia kwa kiasi fulani kujenga soko ambalo linazingatia zaidi ubora wa kazi.

  Lakini cha kusikitisha, tovuti za taasisi za serikali ndio zinazoongoza kwa viwango vya chini huku zikiwa zimegharimu fedha nyingi. Nakumbuka tovuti ya wizara ya mambo ya ndani ilitengenezwa kwa bajeti ya 80Mil kama sijakosea. Ingawa utashangaa kwamba tovuti yenyewe inaonekana kama ya bajeti ya 1.5M hivi.

  Watu wa "longolongo" ndio watu wanaokumbatiwa na kupewa vipaumbele hapa kwetu. Watu wanaojifanya kuwa "professional" ndio wanaoganga njaa hapa mjini. Mwishoni hata wale wenye vipaji wanaamua kuwa longolongo alimradi waende na jinsi mfumo mzima unavyotaka.

  Tunaweza sema mengi kwenye hili, ila ukweli utabaki kwamba, katika malezi tuliyopewa, wengi hatukufundishwa kuweka kipaumbele katika ubora. Na hili litabakia hivi kwa kipindi kirefu sana kabla ya watu kubadilika.

  Ram
   
 20. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  Laki mbili?? Ni kampuni kubwa sana, kwa hiyo tunahitaji logo ya ukweli.
   
Loading...