Mimi ni wakala wa Mpesa vodacom nahitaj msaada wa kisheria wa kuishtaki kampuni ya Vodacom kwa kuniibia Tsh. 300,000/=. Kesi yenyewe ipo hivi; Kuna mteja amekuja kwangu kutoa fedha kupitia mtandao wa Vodacom Mpesa nami kama wakala nimemuhudumia bila shida.
Katika kuhakikisha muamala ni sahihi nimehakikisha nimepokea msg ya kupata float kutoka kwa mteja na mteja amenionyesha msg ya kuthibitisha kwamba muamala wa yeye kutoa fedha kupitia namba yangu wa wakala umekamilika.
Sasa kila nikiangalia balance ile fedha haijafika katika akaunti yangu ya wakala na nikiwauliza Vodacom customer care wanasema muhamala uliofanyika haujasoma katika system yao na wala haupo lkn cha ajabu mihamala mingine yote liyofanyika imeonekana kwenye system yao.
Msg niliyopata ya kuuthibitisha muhamala ninaoudai ni kutoka Mpesa na wala si kutoka private namba na zaidi msg hiyo imetaja mpaka ongezeko la kiasi cha fedha katika akaunti yangu ya wakala ambayo ni sahihi ijapokuwa ongezeko hilo halisomi kwenye akaunti yangu ya biashara ya uwakala.
Kuna uwezekano mkubwa wahudumu wa Vodacom Mpesa wamehack muhamala huu na kuzuia usisome kwenye system hivyo naomba msaada wa kisheria ili niweze kuishtaki kampuni hii.
Ahsanteni