Nimegundua mumeo hajakushirikisha c anajua una roho ya korosho.
Yeah...nampa big_up sana jamaa kwa kujitambua mkuu...mtu kama una uwezo wa kumudu familia yako...sion ni kwanini usisaidie ndugu zako.....kamsoma mke wake ana tabia mbaya.
Habari zenu wapendwa, imani yangu ni kuwa mu wazima,
Kuna tatizo hapa, asubuhi ya leo nimekaa najiandaa kutoka kaja binamu wa mume wangu na mabegi kuuliza eti amekuja kukaa nyumbani kwangu asome chuo.
Kumuhoji kawa mkali eti mimi sina ubinadmu na mambo mengi mabaya nikasema tatizo siyo huyo binti kuja tatizo kwa nini hakunijulisha kama walishapanga amlete hapo nyumbani.
Nilichofikiria mimi naondoka niende nyumbani kwetu kidogo nirudi baada ya wiki moja coz haya mambo hata katika familia nilivyokulia baba hawezi fanya kitu kama hicho bila kumjulisha mama.
Hapa nipo sahihi wapendwa?
umeona eeh afu unakuta mtu anakuwa ivo ukiangalia familia aliyotoka unachoka mwili na roho...kila kukicha afazali ya jana
sishangai, manka?!!
binamu kinyama cha hamu, ondoka wenzio wafaidi
Wanaume wote hawawezi kuwa sawa na baba yako, kila mtu anaendesha familia kivyake. Kila familia yaani mme na mke ni unique duniani - hakuna zinazofanana. Kuondoka nyumbani sio ufumbuzi. Ukirudi ukakuta kuna mwingine hapo nyumbani usije kulia tena hapa. Gangangamala nyumbani kwako utafutev ufumbuzi na mumeo!
Hahahaaa, anamsusia fisi bucha...
anatoa nafasi nzuri ya mchepuko ha ha haha ha ha ha uuuuuupsi ondoka wenzio tuhamie loo
acha utot kaa na mumeo muongeee
kumbuka baba ni kichwa cha familia kosa alofanya ni kukutokukushirikisha tu
Mwenzako kafanya kosa kwa kutokushirikisha katka suala kama hilo. Hata hivyo uamuz wa kuondoka uache familia si mzuri nadhani bado mna muda wa kukaa mkazungumza juu ya hilo hata kama kosa la awali lishafanyika. Hiyo ni familia yako na we kama mama una mchango mkubwa kuhakikisha inakaa stable. Kitendo cha kuondoka hata kama ni wiki kinaweza kuwa na madhara makubwa kuliko unavyoweza kufikiria
we kweli strong rula!Wanawake wengine bana ni Viazi, inamaana wewe mtu akitaka kuja kwa mmeo lazima akwambie wewe ndio umpe Visa ama? Nathubutu kusema ni utoto unakusumbua na pili ni kwakuwa hauna watoto bila shaka ndio maana!