Nahitaji kupata cheti cha kunitambulisha kama (IT)

ashomile

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,622
2,428
Mimi nahitaji msaada kama inawezekana , Najua kutumia vema kompyuta, mpaka kufanya matengenezo upande wa software pekee, najua kutumia vizuri Microsoft office, kupiga window na kurepair kompyuta kama inashida kwa upande wa software hakuna tatizo lakunishinda yapata miaka mitatu.

Nachoomba ni namna gani naweza pata cheti cha kunitambulisha maana nina taaluma tofauti na hii ila na hii nayo ni sifa inayoweza kunipa kipaumbele nikiwa na cheti.

Maana kuna sehemu nahitaji kuomba kazi nikiwa nimeambatanisha na cheti cha taalum ya IT nipo tayari kwa gharama au kama kuna chuo nawezapata ushauri na msaada wakutunukiwa cheti kwa kupewa mtihani nipo tayari .

Naombeni Ushauri Wenu.
 
Labda ufoji, ni chuo ulichosomea pekee kinachoweza kukupa cheti
 
Hakuna taasisi itakayo kupa cheti kma haijakufundisha. Unatakiwa uchukue course yao kisha ufanyie mtihani ndio upate cheti. DIT, UCC na vyuo vingine vyenye masomo ya ICT na CS zinatoa short courses.

Kama pale UCC unaweza chukua short course ya Micro computer applications (ms office, email, internet, nk.) mwezi mmoja au miwili unapewa cheti.

Pia wana course ya Computer Maintenance in Software and hardware hzo nazo unaweza chukua utapewa cheti ukimaliza. Hvyo ndio unavyopata cheti
 
Hakuna taasisi itakayo kupa cheti kma haijakufundisha. Unatakiwa uchukue course yao kisha ufanyie mtihani ndio upate cheti. DIT, UCC na vyuo vingine vyenye masomo ya ICT na CS zinatoa short courses. Kma pale UCC unaweza chukua short course ya Micro computer applications (ms office, email, internet, nk.) mwezi mmoja au miwili unapewa cheti. Pia wana course ya Computer Maintenance in Software and hardware hzo nazo unaweza chukua utapewa cheti ukimaliza. Hvyo ndio unavyopata cheti
Ushauri mzuri sana na nitaufanyia kazi
 
Umedanganya.
Nikikufanyia interview mimi kwenye category ya software wewe as a beginner unafeli mapema sana.

Hujasoma IT wala CS huwezi tuambia hushindwi chochote kuhusu software hii kitu ni mtambuka balaaa
Wewe umeingia darasa lakini mimi ambaye sijaingia naweza kukuzidi mbali sana .
Kwanza kabisa nina kipaji asilia .
Pili mimi najifunza kila kuitwa leo .

Unachonizidi ni cheti maana kuna watu wamesomea Arusha College ila mpaka leo huwa wanakuja nakusema kwamba kuna mambo wameyasahau nawasaidia .
Na wanashukuru .
 
Wewe umeingia darasa lakini mimi ambaye sijaingia naweza kukuzidi mbali sana .
Jesus Christ! Labda ni kweli 😅
Kwanza kabisa nina kipaji asilia .
Cha computer?
Pili mimi najifunza kila kuitwa leo .
Machine learning? 😄
Unachonizidi ni cheti maana kuna watu wamesomea Arusha College ila mpaka leo huwa wanakuja nakusema kwamba kuna mambo wameyasahau nawasaidia .
Na wanashukuru .
Unaona sasa yani nashindwa hata niandike nini nabaki nacheka tu.
Hivi umehisi kabisa level yangu huenda ikawa sawa na hao watoto aiseee hii ni dharau hata ungelitaja UCC baaado ingekuwa ni dharau
 
Mimi nahitaji msaada kama inawezekana , Najua kutumia vema kompyuta, mpaka kufanya matengenezo upande wa software pekee, najua kutumia vizuri Microsoft office, kupiga window na kurepair kompyuta kama inashida kwa upande wa software hakuna tatizo lakunishinda yapata miaka mitatu.

Nachoomba ni namna gani naweza pata cheti cha kunitambulisha maana nina taaluma tofauti na hii ila na hii nayo ni sifa inayoweza kunipa kipaumbele nikiwa na cheti.

Maana kuna sehemu nahitaji kuomba kazi nikiwa nimeambatanisha na cheti cha taalum ya IT nipo tayari kwa gharama au kama kuna chuo nawezapata ushauri na msaada wakutunukiwa cheti kwa kupewa mtihani nipo tayari .

Naombeni Ushauri Wenu.

Hakuna elimu rahisi kiasi cha utakavyo wewe
Ilete kwanza hiyo 1.5 tuitafune umezeshwe slides ndio tukupatie cheti
 
Jesus Christ! Labda ni kweli

Cha computer?

Machine learning?

Unaona sasa yani nashindwa hata niandike nini nabaki nacheka tu.
Hivi umehisi kabisa level yangu huenda ikawa sawa na hao watoto aiseee hii ni dharau hata ungelitaja UCC baaado ingekuwa ni dharau
Mkuu, msamehe bure!! Nikimsoma between lines naona haelewi ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya juu ya kile anacho kizungumza.

Kwa mtu ambaye anajieleza mwenyewe kuwa anajua 'kupiga Windows' na vichangamoto vidogo vya computer anahitaji cheti cha IT, kwa IT expert akimsikia atamhurumia tu.

Hivi huyu anasema anajua software related issues, ukimpa network related issue anaweza hata kufanya troubleshooting achilia mbali kulitatua tatizo husika?

Ushauri:
Kijana, kwa unachokijua nenda kasome short courses za Software applications na PC Maintainance ili upate cheti kinachoendana na matamanio yako.
 
nilijua tu soon dogo atajua hajui, pale anapojaribu ku-under estimate professions za watu.
Ngoja tukuulize kaswali kadogo.
Badilisha base 2 namba 10001111 kwenda
a)base 16(hexadecimal)
b)base 8(Octal)
c)base 10(Decimal)

Mkuu, Nikiwa kama IT expert namuombea radhi, naamini hajui akisemacho.
really ? nipe steps za ku configure MQTT itumie port nyingine zaidi ya 8883 kwa secured channels
 
Back
Top Bottom