Nahitaji kupanda mlima Kilimanjaro - this November

just-imagine

JF-Expert Member
Aug 18, 2015
374
448
Habari wakuu,

Nahitaji kupanda mlima Kilimanjaro mwezi wa 11 mwaka huu, kama kuna mtu anaweza kuniunganisha na tour company/mountain climbing company ambayo ina gharama nafuu nitashukuru sana. Natanguliza shukrani.

NB: Nipo peke yangu.
 
Kuna uzi hunu mtu alipanda mlima Kilimanjaro, utafute utakusaidia.
 
Nilipanda mwaka jana wakati naishi Maji ya Chai Arusha. Nilitaka kufa. Niliishia Kibo stop. Nikarudi chini.
 
1. Atmospheric pressure kule juu ipo chini sana. Oxygen unaitafuta kwa tochi.
2. Baridi damu inaganda mikononi.
3. Chakula mnashindia mikate na maji.
4. Sikuona raha yoyote zaidi ya tabu
Nimepanda mwaka jana mwishoni, nilipita njia ya marangu. Changamoto nilianza kupata baada ya kufika kibo hut, kwanza sikuwa na hamu ya chakula pili kila nikijilazimisha kula natapika na usiku natakiwa kwenda summit. Nashukuru Mungu nilikomaa na mlima huku nikiwa na njaa hadi nikatoboa. Laiti kama ningemwambia guide tatizo langu wasingeruhusu kupanda ila niliwaficha, nikaja kuwàjulisha wakati nashuka
 
Back
Top Bottom