Nahitaji kujua vigezo na masharti vya kujiunga Indriver

Nahitaji kujua vigezo na masharti vya kujiunga Indriver

Tape measure

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2015
Posts
1,989
Reaction score
3,692
Mwaka 2018 ilianzishwa kampuni ya usafiri ya tax kwa mkoa wa Mwanza Taxify baadae wakajiita BOLT, Madereva walihitajika kuhudhuria mafunzo ya siku moja, karibu na Rocky City Mall, waliohudhuria kipindi cha mwanzo walipata commission nzuri kila mtu alitamani kuwa tax driver mjini.

Kwa Dar es Salaam Uber nayo ilivuma sana, mpaka wahuni walipoivamia inafika pahali unafanya booking ya Tax, App inakuelekeza bei mfano itakua 4,000-6,000 lakini dereva anakuambia atakuja kama utamlipa 8,000. Hawa ni madereva wahuni na kama mtu una haraka inakulazimu kukubali au kujadiliana bei ipungue kitu ambacho sio sawa.

Kwa sasa kuna kampuni nyingine inayofanya kazi katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Dar Es Salaam wao nasikia wanajiita Indriver na application yao ni IndriverApp. Dereva ambaye amefanya kazi ya Tax na kutumia Indriver App kupata wateja katika mikoa hii nahitaji kujua vigezo na masharti vya kujiunga nao.

Wanahitaji gari za kuanzia mwaka gani, commission zao zinalipwaje, kuna maboresho yeyote kama mteja kuweza kumpata dereva wa gari akiwa offline!! ikiwezekana kupata namba za ofisi tuweze kuwasiliana nao kiurahisi itakuwa msaada na kwa wengine wachangamkie hii fursa ikiwa ya moto.

Aluta continua
 
Kama wewe unamiliki gari na unataka kuwa masikini ingiza gari yako indrive.

Utaelewa ninachoongea.

Kwenye miji midogo kama Arusha uendeshe gari mfano;
Mteja anattaka kwenda Kwa Morombo au njiro km 9 ana 4000 alafu uende kule ukifika usubiri atokee mwingine atakayehitaji kurudi mjini tufanye labda Kwa 5000 mfano jumla itakuwa 9000.

Hii 9000 ni Lita 3 ya petrol na distance ni 18kms.Na hii unaweza kwenda usipate request ya abiria anayerudi kwenye kituo Chako je utalala huko?

Nilimpatia uncle angu gari Carina wakati hii app imeingia nikamwekea fulltank.

Baada ya mda mchache nikaona Dogo anazidi kukonda tu nikamuuliza kulikoni?

Kaniambia hii sio kazi ni shughuli.

Alivyonielezea nikamuelewa sana. In short Kuna miji Haina movement kubwa so hata mzunguko wake wa pesa uko pale katikati ya mji tu zaidi
In short sikushauri
Kumbuka gari haihitaji petrol peke yake
Gari inapaswa
Kwanza: ijihudumie,
Pili: imhudumie anayeiendesha
Tatu: imhudumie mmiliki
Nne: Ijiwekee akiba
Tano: Ijilipie Kodi Serikalini
 
Kama wewe unamiliki gari na unataka kuwa masikini ingiza gari yako indrive
Utaelewa ninachoongea...
Umefanya upotoshaji mkubwa sana,Biashara ya Indrive haimlazimu dereva kwenda mahali ambapo yeye hajakubaliana na nauli husika.

Indrive wao wanampa mteja wao nafasi ya kukata ofa yake na dereva ndio unaamua kukubali kwamba itakulipa au haitakulipa tofaut na kampuni nyingine kama Bolt na Uber wao nauli inakuja automatic..
 
Unataka kuniambia wateja wa indrive wanatoa nauli halisi ya Mahali?
Au anakata liofa lake tu la ajabu ajabu Ile taximan njaa ajitoe mhanga?
Ninaweza nikakufanyia screenshot hapa kama evidence ya ule utopolo
 
Kama wewe unamiliki gari na unataka kuwa masikini ingiza gari yako indrive
Utaelewa ninachoongea
Mkuu sipo Arusha naomba kujua wanahitaji vitu gani kukubaliwa kufanya nao kazi, nilifikiria kuweka tax kati ya maeneo ya sanawari, ngarinaro na kijiwe kimoja katika barabara inayoelekea Klub ya Tripple A.

Najua biashara kila siku kuna watu wanaziacha sababu haziwalipi na kuna wengine wanafikiria kuzifanya biashara hizo hizo.
 
Mkuu sipo Arusha naomba kujua wanahitaji vitu gani kukubaliwa kufanya nao kazi, nilifikiria kuweka tax kati ya maeneo ya sanawari, ngarinaro na kijiwe kimoja katika barabara inayoelekea Klub ya Tripple A. Najua biashara kila siku kuna watu wanaziacha sababu haziwalipi na kuna wengine wanafikiria kuzifanya biashara hizo hizo.
Driving license, bima ya gari, picha yako, picha ya gari yako inayoonyesha Plate namba yake
Alafu upambane
 
Driving license, bima ya gari, picha yako, picha ya gari yako inayoonyesha Plate namba yake
Alafu upambane
Vipi kuhusu makato, hamna asilimia ya pesa utakayopata kutoka kwa hawa Indriver? Dereva hawalipi chochote hawa Indriver? Nauliza kutokana na uzoefu wa bolt mwanza walikuwa wanatoa commission 40% kwanza hii pesa sijui wao walikuwa wanaitoa wapi kile kipindi cha mwanzo au ilikuwa promotion tu kuvutia madereva
 
Inaweka record ya routes zako zote so utapaswa kulipia commission
Sijajua ni ngapi Kwa Sasa but ndio hivyo
 
Back
Top Bottom