Mkurabitambo
JF-Expert Member
- Feb 3, 2010
- 230
- 57
Naomba kupata mawasiliano ya mashirika mbalimbali ya mapadre ambayo naweza kujiunga nayo,
Kiwango cha elimu nina degree moja na umri nina miaka 24. Natamani kumtumikia Mungu katika utume huo.
Kwa sasa nipo dar es salaam
Kama hujapitia shule za seminary ni ngumu kufanikiwa unachokitaka kutokana na hujalelewa kwenye maadili ya kanisa katoliki,hivyo kupambana na mambo mengineUshahuri mzuri, ila ndo kuanza kujipendekeza wengine hatujazoea ila taratibu mambo yataeleweka. Ila nilitaka nipate connection ya moja kwa moja
Sawa, lkn pia kama kweli una wito huo au umeamua kutafuta Huduma Fulani itolewayo na kanisa.Ngoja niongee naye nione atasemaje
Sidhani kama ni vzr kumkatisha tamaa. Wito mtu huitwa kwa njia tofauti. Mtie moyo ashindwe mwenyewe!Wewe huna wito wowote Wa kipadre! ..utaenda kutuharibia masister wetu bure!...mtu mwenye wito Wa upadri Kwa umri wako huo lazima ungekuwa unajua taratibu!
Kwasababu kanisa katoliki lina mafundisho, mkatoliki mwenye mafunzo yote ya sakrament hawezi shindwa tambua sehemu na namna ya kujiunga upadre;
Sasa wewe unataka kuwa padre utuvuruge
Labda manabii/mitume wa kilokole mkuu, mapadre wanaishi maisha ya kifukara tuAliye kudanganya ni nani huyo? Mapadre wanapiga hela mno na wanalipwa mishahara minono balaa.
We umetoa nondo za ukweli, nafuata nyayo zao hao jamaaSidhani kama ni vzr kumkatisha tamaa. Wito mtu huitwa kwa njia tofauti. Mtie moyo ashindwe mwenyewe!
Kuna mtu alimaliza Medicine na akajiunga na upadre na hakupitia seminari na ni padre mzuri sana.
Waseminari wengi ndio hawana wito na wengi hukimbia wito huu. Useminari si kigezo pekee cha kuwa padre. Wapo wengi hawakupitia seminari ila leo ni mapadre wazuri.
Nashauri: akaonane na paroko mahalia, then atoe duku duku lake na atasaidiwa. My univetsity mate now ni frateli, hope yupo kwa Teolojia now (kamaliza falsafa 3 yrs, now 3nd yr teolojia) while alimaliza degree ya environmental science.
Jamaa ana historia nzuri ni kumtafuta tu anisaidieSawa, lkn pia kama kweli una wito huo au umeamua kutafuta Huduma Fulani itolewayo na kanisa.
Jitahidi uonane na Paroko wa Parokia ya KIZINGA MBAGALA- KILUNGULE yy huyu aliwahi kutoa story yake mpaka kufikia kuwa Padre kwani moja ya kazi alizowahi kufanya ni kuwafundisha madreva taxi kiingereza.
Hivyo ni MTU aliyemaliza chuo kama ww lkn aliamua kuwa Padre sababu anapenda maisha ya ukimya yasiyona vurugu.
Nadhani ukiwa mkweli atakuonesha njia.
Mbona watu wana histotia za tofauti na hizo bado wamefanikiwa kabisaKama hujapitia shule za seminary ni ngumu kufanikiwa unachokitaka kutokana na hujalelewa kwenye maadili ya kanisa katoliki,hivyo kupambana na mambo mengine
Upadre unaanzia nyumba ya malezi, kisha uende seminary. Sasa wewe umeshapigwa na Maisha ndiyo unataka kufata sadaka.Naomba kupata mawasiliano ya mashirika mbalimbali ya mapadre ambayo naweza kujiunga nayo,
Kiwango cha elimu nina degree moja na umri nina miaka 24. Natamani kumtumikia Mungu katika utume huo.
Kwa sasa nipo dar es salaam
Huku yupo padre wake, anajiita padre mcharounataka Kuwa Padre Jamii forums?
Kweli upadre sio ajira mkuu, ni witoUpadre sio ajira dogo
Leseni ipo mkuu, sema nini kumtumikia Mungu ni kila kituUpadre unaanzia nyumba ya malezi, kisha uende seminary. Sasa wewe umeshapigwa na Maisha ndiyo unataka kufata sadaka.
Pambana hukuhuku mtaani.
Umekosa hata leseni uendeshe UBER ???
Anzia kwenye Jumuiya yako, kisha parokiani, then utafikia u padre, tafadhari. Kwa ma sister wetu. Tumewagharamia sana. Chonde chonde.Leseni ipo mkuu, sema nini kumtumikia Mungu ni kila kitu
Pia nenda Parokia ya Kristo Mfalme Tabata niliwahi pia kumsikia Padre mmoja radio Tumaini akialika vijana wenye wito wa kujiunga Upadre wafike pale.Jamaa ana historia nzuri ni kumtafuta tu anisaidie
Pia nenda Parokia ya Kristo Mfalme Tabata niliwahi pia kumsikia Padre mmoja radio Tumaini akialika vijana wenye wito wa kujiunga Upadre wafike pale.Jamaa ana historia nzuri ni kumtafuta tu anisaidie
Inawezekana mkuu ukimaliza elimu ya juu na kama hujajiingiza kwenye ndoa. Ukiwa na wito unaingia baada ya kuhitimu.Usiingie kwenye upadre kwa umri huo. Kwanza hautokubalika, ile ni system fulani sio unajiingiza tu katikati lazima uanzie chini.
Kufanikiwa kivip labda?,Mbona watu wana histotia za tofauti na hizo bado wamefanikiwa kabisa
Labda manabii/mitume wa kilokole mkuu, mapadre wanaishi maisha ya kifukara tu