Nahitaji kufika Zanzibar

Raphael gadau

JF-Expert Member
Jan 17, 2017
1,006
306
Jamani naombeni kujua,

Nahitaji kufika Zanzibar sasa anayejua hatua za kuzifahamu ilizinisaidie nifike Zanzibar maana sjui hata hatua moja ya kufanya nataka niende nikakuone kulivyo jamani maana kila siku nasikia kuzuri kuzuri, nataka nikakuone kwa macho yangu mwenyewe.
 
jamani naombeni kujua nahitaji kufika zanzibar sasa anaye jua hatua za kuzifahamu ilizinisaidie nifike zanzibar maana cjui hata hatua moja ya kufanya nataka niende nikakuone kulivyo jamani maana kila siku nasikia kuzuri kuzuri nataka nikakuone kwa macho yangu mwenyewe
Kwa kukusaidia, nenda Posta kapande boti nauli kuanzia 25,000 uwe na kitambulisho tu utafika zenji
 
Dar Kwenda Zanzibar Nauli Tsh 25000/-
Nakurudi Hiyo Hiyo Yaani Jumla 50000/-
Boti Nzuri Azam Muda Wa Masaa Mawili Ama Pungufu Ya Hapo (Kama Saa Moja Na Dakika Arobaini)

Uwe Na Kitambulisho Cha Kupigia Kura/Leseni/Nhif Na Vingine Vinavyoweza Kukutambulisha Wewe
 
unaweza kuondoka saa kumi na mbili alfajir na boti ya kwanza saa mbili unakua znz unazunguka kuanzia asubui hadi usiku mida ya saa mbili unarudi kwenye flying horse inaondoka znz saa nne usiku alfajir unakua dar unaokoa gharama za kulala maana znz hoteli ni bei ghali kidogo
 
Bei Ni Kulingana Na Uwezo
15000/-,18000/-,25000/-
Mdau Kasema Hapo UnaweZa Kupata Kilimanjaro V,VI Ambayo Huondoka Dar Asubuhi Saa Moja Hadi Saa Mbili Uko Zanzibar Unazunguuka Kila Kona Na Usiku Unarudi

Pearl Of Stone Town (Lulu Ya Mji Mkongwe)
 
Naomba kujua bei za vyumba kule/gharama za hoteli na vyakula kwa Zanzibar.
Sijawahi kufika nchi jirani hii
 
Naomba kujua bei za vyumba kule/gharama za hoteli na vyakula kwa Zanzibar.
Sijawahi kufika nchi jirani hii
Vyumba ndio mtihani ndugu, 40,000/- hadi 60,000/- ni chumba cha kwaida kabisa, kwa hapa Dar ndio zile za 15,000/-.
 
Panda basi mpaka ubungo, shuka panda mwendo kasi mpaka posta, chukua ticket pale kwenye ofc za baharesa panda boti, nakusubiri zanzibar mi mwenyeji wako
Mkuu wapi unaweza pata chumba kizuri 20,000/= hadi 40,000/= unacheki DsTV
 
Jamani naombeni kujua,

Nahitaji kufika Zanzibar sasa anayejua hatua za kuzifahamu ilizinisaidie nifike Zanzibar maana sjui hata hatua moja ya kufanya nataka niende nikakuone kulivyo jamani maana kila siku nasikia kuzuri kuzuri, nataka nikakuone kwa macho yangu mwenyewe.
Subiri uchaguzi, sema unakwenda kuipigia kura CCM, serikali itakupatia Kila kitu, akili kichwani mwako
 
Back
Top Bottom