Nahitaji kufanya kazi na M-PESSA, tiGO PESSA, Zan PESSA na Zap PESSA

Mkillindy

Member
Sep 14, 2011
37
4
Wadau ni njia zipi nifuate ili kufanya kazi na haya makampuni???
Pls kwa anayejua na aliyefanya nao naomba anaeleze.
N:B Pia mapungufu ya kazi hiyo mniambie wadau.
Kwa urahisi waweza ni sms a.rashid@jigambe.com
 
uko mbali sana?? wapi huko??
hii business inataka uwaone wahusika na utakamilisha taratibu zote, huwezi kamilisha hukohuko ulipo. pia kila mkoa kuna shops zao(vodashop, tigo, zap ect) uende ukawatembelee.

kama ni kuhusu biashara, ipo safi. tafuta sehemu yenye mzunguko wa watu eg stand, sokoni, etc. inalipa ndugu.
 


Asante ndg yangu, itabidi nitoke huku nilipo niwafuate huko.
 
Mkuu angalia hii kutoka kwenye site ya vodacom procedure za kujiunga nadhani na wengine watakuwa kama voda..


Pia kuhusu tigo cheki hapa ::: Tigo :::Kuhusu
 
Wadau ni njia zipi nifuate ili kufanya kazi na haya makampuni???
Pls kwa anayejua na aliyefanya nao naomba anaeleze.
N:B Pia mapungufu ya kazi hiyo mniambie wadau.
Kwa urahisi waweza ni sms a.rashid@jigambe.com

Inamaanisha unawebsite au unawebmail tu peke hiyo site ya jigambe haipo maanake nahitaji system ambayo itanisidia kwenye biashara zangu.
 
Thanks kaka, umenifungua macho nikakutana na website kibao za tanzania.
Ila hiyo site ya JigambeAds nimeipenda sana. Hv inafanyaje kazi ?

Mkuu sidhani kama hii itakusaidia hususan kwenye issue yako..., hawa jamaa hiyo site yao ni platform ya kuwakutanisha watu wanaotangaza biashara zao na watu ambao wanaweza kuwatangazia (yaani watu wenye websites au blogs)

Mfano kama wewe una website unajisajili pale alafu wenyewe wanakuunganisha na watu wenye matangazo ambao wanawalipa wenyewe alafu wewe wanakupa commission...

Sounds easy ila bila traffic kwenye website yako au blog huwezi kupata pesa (sababu matangazo mengi huwa ni Pay Per Click) hivyo basi kama unayo website tayari na ina traffic ya nguvu ndio unaweza kupata pesa tena hapo nadhani unaweza hata kuwafata watangazaji direct na kutumia hata google adwords n.k.
 
labda mimi nipo nyuma sana kimaendeleo, kwani
[h=2]M-PESSA, tiGO PESSA, Zan PESSA na Zap PESSA ni nini?[/h]
 
Lakini kama ni biashara ambazo zipo chini ya mamlaka ya watu au shirika fulani, ni lazima na ni busara zaidi kuwaona hao watu ili ufanye biashara ya halali na yenye uhuru
 
hongera saharavoice kwa ushauri makini na wenye tija kubwa
 
labda mimi nipo nyuma sana kimaendeleo, kwani
M-PESSA, tiGO PESSA, Zan PESSA na Zap PESSA ni nini?
Kutuma na Kupokea pesa kwa kutumia simu za mitandao ya Vodacom; Tigo; Airtel na Zantel.....

Inabidi ujiunge na hii service; ambapo mtu yoyote anaweza akakutumia na wewe kwenda kuchukua hizo pesa kwa mawakala (kwahiyo kutuma na kupokea ni kupitia hawa mawakala..) Kwahiyo Mkilindy anataka kuwa wakala wa hii huduma kupitia hayo makampuni
 
nenda ukapige pesa, zipo za brerere kimsingi uwe na mtaji tu wa kuanzia kama milion 4 hivi kwa makampuni yote yaani TIGO, voda na zain
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…