Nahitaji kufahamu kuhusu MBA ya chuo cha AMUCTA-Tabora

Nahitaji kufahamu kuhusu MBA ya chuo cha AMUCTA-Tabora

muuza ubuyu

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
3,543
Reaction score
3,599
Habari za majukumu jamani.

Napenda kuuliza kuhusu ubora wa MBA itolewayo na chuo cha Archbishop Mihayo University College of Tabora ambayo ni tawi la SAUT.

Mimi nimegraduate bachelor yangu kutoka SUA miaka 10 iliyopita na tangu muda huo nimekuwa nikifanya kazi katika remote areas kiasi kwamba nimeshindwa kujiendeleza kielimu.
Kwa sasa natarajia kuhamia kikazi Tabora mjini hivyo naona pia kuna nafasi ya kujiendeleza. Je, chuo hiki kinatoa elimu bora inayoweza kumjenga mwanafunzi mpaka akawa na uwezo wa kumfanya awe mweledi katika tasnia yake ama hapana? (Bila kujali uwezo binafsi na altitude ya mwanafunzi). Please share experience yako kuhusu hili.

NB: Nilishawahi kusoma OUT MPM semester moja sikuridhishwa na namna nzima ya utoaji wa elimu yao hivyo niliacha.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndugu yangu achana na hivi vyuo vya wasi wasi. ukitaka MBA ambayo niya uhakika nenda vyuo vya serikali tuuu . full stop
 
ndugu yangu achana na hivi vyuo vya wasi wasi. ukitaka MBA ambayo niya uhakika nenda vyuo vya serikali tuuu . full stop
We jamaaa bado unamawazo mgando sana ya miaka 1990's nani alikwambia elimu bora inatolewa na vyuo serikali?
Nchi nyingi zilizokwisha endelea elimu ya chuo imeachiwa private sector..serikali imekuwa msimamizi tu.Mbona hausemi elimu ya primary au secondary ukitaka bora uende serikalini ambako ndiko foundation ya elimu ilipo.Kwa nini wazazi wanakimbiza watoto wao private school? Hata chuo ndio hivyo hivyo..
 
We jamaaa bado unamawazo mgando sana ya miaka 1990's nani alikwambia elimu bora inatolewa na vyuo serikali?
Katika suala la masters degree mambo ni tofauti sana na hicho unachosema. Vyuo vingi (sio Vyote) vya private havina uwezo wakuajiri na kulipa wahadhiri wenye level ya senior lecturers( ndio wanatakiwa kufundisha postgraduate), hivyo basi wanachuo wa masters wamekua wakifundishwa na assitant lectuers na lecturers wenye masters ushahidi upo. aidha vyuo bora duniani ni vile vya umma na si private kama unavyo sema.
 
ndugu yangu achana na hivi vyuo vya wasi wasi. ukitaka MBA ambayo niya uhakika nenda vyuo vya serikali tuuu . full stop
Tatizo mkuu nahitaji kusoma huku naendelea na kazi kwani tayari nina majukumu yangu ya kifamilia yanayohitaji pesa hivyo nikiacha kazi (nipo private sector) ili niende shule that means my family and my long terms plans will shake.

Pili naomba utoe mawazo yako kuhusu ubora wa AMUCTA tu. Na-opt hawa jamaa kwa sababu wanatoa MBA evening class.

OUT hapana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah, ina maana humu hakuna mliosoma AMUCTA (consituent university college of SAUT, Tabora)? Wadau tiririkeni basi!
 
kunavitu waliambiwa na TCU wavirekebishe lkn wakakaidi ndipo TCU wakawazuia kudahili,lkn wenyewe ukiwauliza wanakwambia tunasubiria majibu kutoka kwa Waziri wa elimu,yaan hawataki kuonyesha na kukubali km wamezuiliwa kudahili,lkn km mtu mzima unajua tu nn kinachoendlea
 
Duh, shukrani sana bro kwa taarifa.
 
Back
Top Bottom