Nahitaji Faraja Moyo wangu Unateketea.

Hata mimi sijawahi ona mwanume weak kiasi hiki. Labda kipindi cha shule tena o level

Hata kwenye maisha ya kawaida bado napata ukakasi kama atayamudu vilivyo
 
Pole bro.
Hayo ndiyo maisha ya wanawake na wanaume wote waliomo humu duniani.
Kama huna pesa, jiandae kwa masimangano na dharau hata kama ni mkeo na umezaa nae.
Nachokuusia
Achana na matamanio yasiyo ndani ya uwezo wako. Mwambie Mungu akusaidie kukuepusha na changamoto ya huyo mwanamke. Fanya Ibada iwe faraja kwako. Utapata uhuru wa kufikiri kuhusu maisha yako na muda ukifika Mungu atakupa wa aina yako.
Usidanganywe na rangi ya chai, utamu ni wa sukari. Vipo vingi vilivyo vizuri lkn ndani vimeoza bro!!!!! .
 
Kwanza, kwahiyo sisi wazibue chemba umetudharau,kuwa upate kazi hata ya kuzibua chemba.
Pili; kaza moyo Mkuu wanaume hatuwi weak hivyo,najua kuna kupenda lakini fikiria kwani kabla ya kumjua uliishi vp? Wengi tumepita huko kutoa chozi lakin unapiga moyo konde unaaga,na usigeuke nyuma,mapenzi ni kuheshimiana,afu umependa usipopendwa
Take next step in Jesus name am sure you will win the battle.
 
Ni kwel kk umempa ushaur mzur xana
 
Sasa ndugu yangu huoni hilo tanuru la moto wewe ndo unalikumbatia?
 
Huwa naona ni vigumu kufanya maamuzi hayo kwake maana hata kama nikiyafanya hawezi hata kuumia hata robo ya maumivu yangu, ninahisi kama nitajitesa sana kuliko sasa.
Upo weak sana ndugu yangu na kama utaendelea hivi utasumbuliwa sana.
 
Naomba hela eh
 
Material girl hivi vijana wa siku hizi mmerogwa na nani yani kujua tu huyo ana tamaa na mpenda pesa kazi?
 
Sasa hao wanaompa pesa unafikiri wanampa bure? Simama kama mwanaume, jipange na tafuta mtu wa kupanga naye maisha lakini sio huyo ulo naye, kwa akika hamtafika mbali.
 
Pole sana kijana ILA hapo una ajira mbili. Chamsingi chagua moja kwanza. Chagua maisha wanawake wapo wengi na hawatoisha. Jenga maisha yako na kama hapo ulipo ni pagumu hama nenda kajaribu kwingine mkoani. Tafuta MTU ambaye atakuamini akupe mtaji mfanye biashara pamoja na usipende kulia lia kuhusu wanawake. Kuna watu wana mitaji ILA hawana watu wakusaidiana nao. Hakikisha umekua stable kwenye maisha ndo uangalie wanawake poti. Mwache ahangaike na wanaume we hangaika na kazi.

Ni hayo tu
 
Ndugu samahani, usinielewe vibaya, HUYO SI MKE mke anapaswa awe tayari kuishi na wewe kwa hali yoyote, furaha au huzuni mshikamane, sasa huyo anayekuponda kisa huna kazi hujui hakufai? Leo ukiajiriwa atakupenda na utaishi kwa amani ,je siku umepoteza ghafla ajira si naye atakukimbia, chukua hatua HERI KUVUNJA UCHUMBA KULIKO KUVUNJA NDOA. Tafuta mwanamke mwingine wapo ambao wanahitaji mme na si wanaohitaji ajira yako kama huyo.
 
Natamani iwe hivyo ila...
Ama kweli kuoenda ni upofu!!!
Na vipi mambo yakiharibika baadae tena mkiwa ndoani!!!! Maana ashakuonyesha yeye ni wa jinsi gani wakati ambapo hauna kitu.

Au huyu binti hana tatizo ila wewe ndio unajistukia kwakuwa hauna kitu????!!!!!!
 
NB: Adamu aliumbiwa kila kitu ndio akaumbiwa Hawa. Hope unaelewa ina maana gani hiyo[emoji12]
 
Ukiwa na mahusiano na mwanadada hlf analazimisha umuoe unatakiwa kuwa makini nae sana
 
Kwanza usimuhusishe MUNGU maana huo ni uchumba wa zinaa,
Lkn pole sana sana sana,
Ktk mahusiano makosa ni sehemu ya kuendelea mbele na kujitengeneza,
Lkn makosa ya makusudi ni ishara ya taabu utazopata milele ukiendelea kuwa nae,hyo ni alarm,
Bila kuzunguka zunguka nakusihi achana nae haraka sana hiyo ni sumu unakunywa,mtu siyo mke unahangaika nae wa nini,ukilazimisha itakuumiza sana siku ukimuoa,hebu kaa pembeni kidogo muachie nafasi ya yy kuhanhaikia tamaa zake, wewe hangaikia uchumi na maisha yako ya kiroho,
Usiwe na mahusiano na mwanamke mshari na mwenye makusudi,
 
Mhhh pole but hakuna mahusiano yaliyo fanikiwa bila kupitia ups and downs ni swala la mda tu ajira zipo mda ukifika utaajiriwa kikubwa mvumilie tu mwoneshe upendo wa kweli mjali Mambo yataenda vzuri tu..... Happy nyu year in advance
Makusudi unaiitaje ups an downs,
Visa vya makusudi lengo ni kukuumiza,mke ni msaidizi,Huyo anamsaidia kuumia badala ya kutulia,
 
Pole sana...
Kuna msemo unasema, "To every successful man there is a strong women behind"...

Huyo siyo strong woman, she will never motivate you to success sana sana, ukishapata hiyo kazi atakuburuza, kuku-demand na hata kuku-comand kwa kivuli cha amekuvumilia wakati wa shida zako, kumbe siyo kweli...

Follow your heart but carry your brain with you...


Cc: mahondaw
 
Itakuwa ngumu kwako kupata kazi maana unastress sana and believe me fanya maamuzi magumu usimfuatilie kwa lolote focus kwenye namna ya kujikwamua na hali yako kiuchumi... bila hivyo miaka itakatika utashangaa na roho yako
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…