Nahitaji Faraja Moyo wangu Unateketea.

Dah mamaee mwanamke Umeeleza jinsi gani mlivyo wanawake. By the way huo ndo ukweli and I love that being honest.
 
Ishi kulingana na hali uliyo nayo mkuu. Piga chini hizo dharau utavumilia mpaka lini? Wekeza nguvu na akili yako katika kutafuta mkwanja ndio thamani yako ataiona. Maumivu siku mbili tatu mambo yataenda sawa. Hatua ya kwanza kata mawasiliano nae. Wanawake wapo wengi tu kwa nini ujitafutie matatizo ya kiafya kwa sababu ya mtu ambaye hatambui wala athamini juhudi zako?
 
Nashukuru sana kwa nasaha zako, Ila najua milango itafunguka japo sikupenda ifunguke yeye akiwa nje nilitaka wote tuingie ndani. [emoji17] [emoji17] [emoji17] [emoji17]
mhenga kijana inaelekea hukuelewa maana ya zile methali mfano;
1. asiyesikia la mkuu huvunjika guu
2. asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu
3. sikio la kufa halisikii dawa
4. mtaka nyingi nasaba hufikwa mingi misiba

pia kuna misemo kama;
1. mpende akupendaye asiyekupenda achana naye
2. akufukuzae hakwambii toka

tafadhali jaribu kutafuta maana za methali na misemo hapo juu ukiielewa utapata faraja ya moyo unayoitafuta.
 
sikia bro,pambana na maisha kutafuta kipato na huyo mwanamje muage kwa furaha na amani kuwa mmeshindana tabia,mtakiane kila la kheri,kila mmoja afate hamsini zake.Wala usiyumbe mkeo bado hujakutana nae
 
Labda kama ni story ulichokiandika..
Lakini kama ni maisha halisi basi niseme tu kuwa umeamua kujichimbia kaburi mapema sana.
Dalili zote hizo unapambana, unachokitafuta utakipata. Yangu ni hayo
 
We umeamua kumpa makavu..na hata kama ukilizwa na demu lia mara moja tembea mbele.
Anajitafutia magonjwa ya moyo huyu.
 
Ukimuoa ukiwa hela na akaja zizoea hela atatafuta kingine kipya usichokuwa nacho, utajitahid ukipate atatafute kingine ambacho huna tena!

Najua moyo ukipenda huwez ona kibaya....heri ya christmass mkuu
 
E
We je mshikaji ni mara yako ya kwanza

Jiajiri au usubiri ajira lakini huyo si wako achana inawezekana atakuwa kama goli kipa anaakaa golini anasubiri kona zipigwe na penalit zipigwe ni Nouma

Mkaushie huyo tafuta mwingine tofauti na hapo utaumia kinyama

Kama disco cheza sana , cheki movies ndefu ndefu za kininja na nyinginezo zitakufanya ujihisi km hao wanaigiza na kumuona huyo ni wa kawaidaa saaana

Utakuja baadae unaleta mrejesho Mujarabu
 
Unamiaka mitano toka uzaliwe?
 
NB : na hao wachache Mungu hua anawaangalia na kuwabariki
Yesu Kristo alizaliwa kwenye zizi la mbuzi sehem chafu chafu mbaya mbaya sehemu isiyo kua na kiyoyozi wala kitanda lakini pale Mungu alipaona hapa ndipo atazaliwa mwanae mpendwa mfalme wa wafalme duniani
 
Mkuu usiumize kichwa, HAUPENDWI na HUTOPENDWA NAYE HUYO MWANAMKE
kama kuna uwezekano wa kuondoka uende ukatafute maisha sehem ya mbali nenda kapambane na Mungu atakusaidia. mwambie tu kistaarabu kwamba umefikia mwisho kwaio kila mtu aende njia yake mwache na uwe na amani, tena furahia na ushangilie mana utakua umejiokoa.
Muombe Mungu ukiwa na nia ya dhati atakuletea mwanamke anayekustahili.
 
Pole mkuu...ungemuacha kwanza utafute life, then likitick ndo utajua umrudie au ummwage!
 
Wewe naona unajipa mizigo miwili wa kutafuta kazi na wa kumfikiria mtu mwingine.

Mwache tena mueleze mama sina kazi siwezi kukuhudumia na pia naona nakuchelewesha maisha wenzako wanaolewa naona nakupa wakati mgumu...hapo achague kusuka au kunyoa...

Nimeupenda ushauri wako...
UKWELI utamuweka huru.
 
Umemchoma kama pasii, mwenzio ndio kapenda kapitiliza.
 
Kwa maelezo yako hakikisha hupiti karibu na wauza sumu za panya maana huchelewi kununua. Pole sana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…