Nahitaji busara za Mshana jr na Faizafoxy

Mbona hao ndiyo majority? Wafuatilia siasa,wapiga kura na mashabiki wa vyama ni wachache mno ukilinganisha na wasiojihusisha wala kufuatilia yote hayo.
 
Samahani Aunt Faiza, hii ya pili (kwa ufahamu wangu) inahitaji darasa la kutosha sana ili ieleweke inawezekana vipi??!!.
Hiyo ya pili ni uchawi.

Waislam tunafundishwa kuwa mashetani hufundisha watu uchawi. Kumbuka kuwa "shetani" ni sifa.

Huna haja ya kuujuwa uchawi bali kujuwa kujikinga na kuuvunja vunja uchawi ni jambo jema .

Soma zaidi: Je Uchawi Upo? Na Vipi Kujitibu? | Alhidaaya.com
 
Naam, ndiyo maana nikasema suala hilo linahitaji Darsa, kwa njia ya "uchawi" (sihr) hapo hakuna shaka, lakini siyo kwa njia ya "dhahir" kwamba mtu abadilike na awe kiumbe mwingine.

Uchawi unakuwa "sihr" kiini macho au mazingaombwe pale unapotumika kuficha uhalisia wa kitu, na hii tunaiona ndani ya Qur'an pale wale wachawi wa Musa (as) walipobadilisha kamba zao na kuwa nyoka, tukio lile halikuwa tukio la dhahiri kwamba kamba zikawa nyoka bali ni macho ya watu yalifanywa na uchawi yaone kamba zimegeuka kuwa nyoka. Hiyo ndiyo "Sihr" (uchawi), na jambo hilo linaweza kuelezwa kisayansi.
 
Asante kwa kunialika kwenye mada hii pamoja na mtalaka wangu...
Kila kitu kinawezekena katika maisha... Ni utashi na maamuzi tu ila ishu za ushirikina ni dhana ngumu kuweza kukushauri kwakuwa wengi hawajui kutenganisha kati ya ushirikina na mazingaombwe
 
Babu yetu huu uwanja ni wako kwa ajili ya kutufundisha namna ya kutofautisha baina ya ushirikina na mazingaombwee.

Karibu sana.
 
Babu yetu huu uwanja ni wako kwa ajili ya kutufundisha namna ya kutofautisha baina ya ushirikina na mazingaombwee.

Karibu sana.
Ushirikina ni halisi mazingaombwe ni kiini macho.. Yani unaona ni halisi kumbe ni ujanja ujanja tuu
 
Ushirikina ni halisi mazingaombwe ni kiini macho.. Yani unaona ni halisi kumbe ni ujanja ujanja tuu
Sasa tutajuaje kwamba hiki ni kiini macho na hiki ni kitu halisi?

Mfano akaja mtu akaifanya karatasi kuwa hela hapa tutatumia kigezo gani kujua kwamba ni kiini macho au ushirikina?
 
Sasa tutajuaje kwamba hiki ni kiini macho na hiki ni kitu halisi?

Mfano akaja mtu akaifanya karatasi kuwa hela hapa tutatumia kigezo gani kujua kwamba ni kiini macho au ushirikina?
Muulize lifespan takes hiyo hela
Ikiwa na mipaka ya karibu na kikomo cha muda mfupi cha matumizi hayo ni mazingaombwe
 
Muulize lifespan takes hiyo hela
Ikiwa na mipaka ya karibu na kikomo cha muda mfupi cha matumizi hayo ni mazingaombwe
Anhaaaaaaaa sasa hapo nimepata jambo.
Nakumbuka miaka ya 2000 wakati nipo primary ilikuwa mtu anapitishwa spoko kichwani na damu damu lakini baada ya muda mchache anarudihswa kawaida
 
Anhaaaaaaaa sasa hapo nimepata jambo.
Nakumbuka miaka ya 2000 wakati nipo primary ilikuwa mtu anapitishwa spoko kichwani na damu damu lakini baada ya muda mchache anarudihswa kawaida
Yeah huo sio uchawi wala ushirikina ni viinimacho na mazingaombwe
 
Huyo faiza...hawezagi kuandika hata.. aya moja...anajua kukosoa tu tuneno twa kiswahili...
Huo ni uonezi wa waziwazi. Nimeshaona michango mingi sana ya Faizafoxy yenye maana japo kuna wakati sikubaliani naye lakini ni mchangiaji mzuri na mwenye ufahamu wa juu pengine kukuzidi wewe.

Usipende akubali kila kituunachokipenda wewe sababu ni Faizafoxy na wewe ni ras Jeff
 
Exactly na imeelezewa fimbo ya Musa ikageuka nyoka mkubwa zaidi na kuwala wale wengine wote, kama sikosei.

Uchawi pia una kitu kinaitwa "illusion". Hii ni art ya ku kufanya wewe unaetakiwa kuona uone kitu ambacho sicho. Au kitu ndicho ukakiona kipo lakini hakipo pale.

Kwa hiyo namba 2 inawezekana lakini ukitaka kufahamu vipi inawezekana hapo inabidi tumuombe LIKUD aje kutoa ufafanuzi zaidi.

Binafsi kuhusu swali namba 2 nasema kiuchawi inawezekana. Physically.
 
Naam, "0ptical illusion" na hata "mirage" (mazigazi ?) nazo pia zimo katika "Sihr" ya viini macho.
 
Anilipe consultation fee nimfafanulie A to Z
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…