Nakushauri ungeenda kuwasiliana na watu wafanyao kazi katika taasisi kama BAKITA, TATAKI, TUKI, nk. Wangekusaidia zaidi. Mimi pia ninasoma English Linguistics (Bachelor), na hizo kozi ni miongoni mwa kozi ambazo ninazisoma, isipokuwa, tunazisoma kiujumla, na endapo mwanafunzi mwenyewe binafsi atataka kuiva katika upande fulani, basi hana budi kwenda kusoma upya, kiundani zaidi. PIA NENDA KAWAONE "TANZANIA TRANSLATORS ASSOCIATION / CHAMA CHA WAFASILI TANZANIA (CHAWATA/TTA). Watu hao natumaini watakuwa ni msaada mzuri kwako kwa kukupatia maelekezo sahihi yahusuyo taaluma hii.