Nahisi simpendi mke wangu

Nahisi simpendi mke wangu

Pole sana mkuu, kuna swali najiuliza ambalo sijaona jibu lake humu, huyo mwanamke mlifunga ndoa?

Maisha ni yako kaka, hela unatafuta mwenyewe kaka, kama mtu haeleweki ndani ya miaka 10 ataeleweka lini tena? watoto wote watatu bado wadogo ila wa kwanza na wa pili nahisi wanaweza kujihudumia vizur sana

Cha msingi angalia Moyo wako unataka nini, watu wengine wanakuaga wametumwa na shetan kuwaharibia watu, au kukuondolea aman tu, Mwanamke rudisha kwao, tafuta dada wa kazi akusaidie kulea wanao mpaka watakapo kua ndio ufikirie kuoa mwingine, kwa sisi wa kristo dini hairuhusu kuachana ila kuna baadhi ya mazingira inabidi talaka ihusike, na mali za kugawana n mali mlizoshirikiana kutafuta kama kwenye uchumi wa familia hana mchango wowote anataka mali gani?

Utampa kiinua mgongo tu
 
Mimi ni mpenzi wa kusoma vitabu hasahasa vya saikolojia, nimejaribu mbinu mbalimbali zinazoelekeza kumfanya mtu akupende na kuwe na amani ndani lakini wapi. Kwa mfano kuna kipindi nawapeleka kanisani na baada ya hapo nawaambia hakuna kupika leo tunaenda kula hotel. Tukifika huko wengine wanafurahi na watoto wanafurahia ma-burger na vingine lakini yeye naanza kufoka kuwa nachezea hela na vyakula vibaya.
Yaani ni mtu wa tofauti. Siku moja nikasema leo hatulli nyumban tunaenda hotel, nikachukua chumba hotel (Kunduchi) nikijua tutauwa tunahuisha mapenzi lakini nichopata natamani kulia. Unamlazimisha mtu ku-do kama umembaka, hakuna kushikana shikna wala nini.
Maisha yananitesa mimi, inaniuma kwani kuna warembo wanakuwa wanaonyesha interest
vitabu vina sehemu yake ila sehemu uliyofikia wewe unahitaji maombi, jiombee mwenyewe na familia yako, omba Mungu akuonyeshe njia na nini cha kufanya, anasema njooni wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha, kama una mtumishi wa Mungu unayemwamini mshirikishe kama hauna jua Mungu anasikia maombi yako, na mimi nitakuombea.
 
Pole sana mkuu, kuna swali najiuliza ambalo sijaona jibu lake humu, huyo mwanamke mlifunga ndoa?

Maisha ni yako kaka, hela unatafuta mwenyewe kaka, kama mtu haeleweki ndani ya miaka 10 ataeleweka lini tena? watoto wote watatu bado wadogo ila wa kwanza na wa pili nahisi wanaweza kujihudumia vizur sana

Cha msingi angalia Moyo wako unataka nini, watu wengine wanakuaga wametumwa na shetan kuwaharibia watu, au kukuondolea aman tu, Mwanamke rudisha kwao, tafuta dada wa kazi akusaidie kulea wanao mpaka watakapo kua ndio ufikirie kuoa mwingine, kwa sisi wa kristo dini hairuhusu kuachana ila kuna baadhi ya mazingira inabidi talaka ihusike, na mali za kugawana n mali mlizoshirikiana kutafuta kama kwenye uchumi wa familia hana mchango wowote anataka mali gani?

Utampa kiinua mgongo tu

Mimi ni Mkristo na kutokana na mazingira ya maisha ninaoishi nieshindwa kutangaza ndoa. Kwa hiyo naishi maisha ya kujifichaficha kanisani. Natoa sadaka, zaka na michango kwa kadri Mungu alivyonijlia lakini sishiriki meza ya Bwana. Inaniuma sana.
 
Nimeshafikiria kuachana nae na hilo limekuwa wazo linalozunguuka kwenye kichwa changu kwa muda sasa, nimepoteza mapenzi na yeye kabisa. Naona kama tunaishi nyumba mbili tofauti na ninatamani akae mojawapo ya nyumba zetu na mimi nikae nyingine. Ukweli kuna kipindi nilimwambia achukue kila kitu aniache huru tu, kwani najua hana moyo wa kutafuta.

Nimejaribu kumpeleka shule nikijua tatizo litakuwa ujinga akaamua kuacha. Akawa ananilaumu kuwa simpendi kwa kuwa hana kazi nikamwambia afungue biashara nimpe mtaji akakataa. Kuna rafiki yangu amemfungulia duka mke wake aliniomba nimkutanishe mke wake na wangu ili amfundishe biashara, mke wangu akakataa.

Nikajaribu hata kumwambia afungue salon awe anasimamia akakataa. Kila kitu yeye ni mpinzani kwangu na kila ninachofanya yeye anapinga. Nikijaribu ku-support huduma za kijamii anakuja juu kama mbogo. Hakutaka hata nichangie harusi ya ndugu yangu na nilipochanga hakuhudhuria harusi ile. Naishi maisha ya kujitenga na jamii mpaka najiona mpweke. Nimempa hela akafungue akaunti benki ili niwe namuwekea hela ya matumizi huko lakini fomu zina miaka miwili ndani hazijajazwa.

Pole sana...kwani ni lazima uishi nae au kashakuloga ninii...oa mke mwingine na atakaloamua na aamue kwani atakufanya nini na ukishaoa anza kumpotezea taratibu,matumizi unayapunguza mpaka unaacha kumpa kabisaa akienda usttawi wa jamii utaitwa uwe unatoa matumizi ya watoto unasema uwezo wako ni elfu 30 mwisho wa siku watoto watakufuata wenyewew...mwanamke anaheshimiwa lakini hajieshim wawapi uyoo mxfyuuu sana...hakuna kugawana mali mali andikia watoto nukta.anamwanaume ndo anayemtia bichwa tafuta kipotable uzae nae faster ndo atajibeba vizur
 
Mimi ni Mkristo na kutokana na mazingira ya maisha ninaoishi nieshindwa kutangaza ndoa. Kwa hiyo naishi maisha ya kujifichaficha kanisani. Natoa sadaka, zaka na michango kwa kadri Mungu alivyonijlia lakini sishiriki meza ya Bwana. Inaniuma sana.
miaka kumi bila ndoa????
 
miaka kumi bila ndoa????

Ndiyo, hakuna mazingira ya kunishawishi kujifunga nira na mtu mwenye moyo kama huo. Mi natafuta namna ya kufanya kwa ajili ya kunusuru afya yangu na amani ya moyo wangu
 
Kuwa makini inawezekana ana ajenda ya siri ya kutaka kukupumzisha kwa amani.
 
Nilifanikiwa kuoa miaka kumi iliyopita na katika maisha yetu ya wawili tumefanikiwa kupata watoto watatu, wote wa kiume.

Migogoro katika maisha yetu ilianza mara baada ya kuanza kuishi pamoja. Mimi na mke wangu tulianza kuishi pamoja kabla ya kufunga ndoa. Binafsi nilimpenda sana na nilitamani kumfanyia kila ninaloweza ili awe na amani na furaha.

Kiukweli tulianza kuishi kwa amani na furaha mpaka pale mke wangu huyu alipoanza chokochoko dhidi ya mama yangu. Alianza kuniambia kuwa mama yangu hampendi na wala alikuwa hataki aolewe na mimi na kisha akaanza kwashambulia wifi zake. Nilijiuliza maswali mengi na baade nikagundua kuwa ni maneno ya kutunga.

Kilichonifanya niamini ni baada ya kukumbuka kwamba mimi na mke wangu tumechukuana kwa maamuzi yetu binafsi (mimi siwashirikishi wazazi) na pili ni kwamba wazazi wangu wanaishi mbali na anapoishi huyo mwanamke, na tatu hapajawahi kuwa na mahusiano yoyote na wala mawasiliano yoyote baina ya familia hizi mbili.

Hapo nikaanza kumuona mke wangu kama mtu wa shari. Mke wangu nilimtoa bara kuja kuishi naye Dar es Salaam na nilitamani kuja kufunga nae ndoa.

Baada ya kuishi naye kwa mwaka mmoja jijini Dar es Salaam na tukiwa tumefanikiwa kupata mtoto mmoja tulipanga safari ya kwenda kijijini kuwasalimia wazazi pamoja na kujitambulisha kwao. Ilipofika Jumapili nilimwambia tutaenda kanisani na tutajitambulisha tukiwa pamoja ili kanisa litupokee na baadae tuanze mchakato wa ndoa.

Tulikubaliana kwa ajili ya hilo ila tulipofika kanisani kabla ya kuingia kwenye ibada huyu mwanamke akaniambia nisimtambulishe kanisani na wala nisijaribu kumtaja. Nilipatwa na hasira iliyoharibu ibada yangu na tuliporudi nyumbani ikawa ni ugomvi tu.

Mimi ni msomi mwenye digrii na mke wangu ni mama wa nyumbani. Niliamua kuoa mama wa nyumbani kutokana na nature ya kazi yangu inayonihitaji kuwa mbali na nyumbani kwa kipindi kirefu nikiwa kwenye camp.

Maisha yaliendelea hukutukiwa na migogoro isiyoisha kila mara akinituhmu kwa mambo mbalimbali, mara nyingine alinituhumu kuwa nina mke mwingine na nimemjengea nyumba na mara nyingine ananituhumu kuwa namuua kwa UKIMWI.

Sikujisikia vizuri na mara kwa mara nilikuwa naenda kupima ili awe na amani na kuna kipindi nilikuwa namchukua kwenda kupima ila yeye anachukua vipimo vingine na kukataa kupima UKIMWI.

Mimi huwa napima na majibu namuonyesha. Katika hali hizo nilijikuta maisha yangu nyumbani yanakosa furaha na mara kwa mara ni mizozo mara huu mara ule. Hata tendo la ndoa ilikuwa nadra kulipata kwa hiari na wakati mwingine nahisi ana mwanamume mwingine anayemzuzua.

Mbali na kuwa mbali kwa muda mrefu, muda mfupi tunaopata kuwa pamoja unakuwa na majonzi tele. Kuna kipindi nilisafiri kwa wiki sita 6 na niliporudi nikadhani mwenzangu amenikumbuka ila nilichokiona usiku ni kibaya. Tulienda kulala na alipojilaza tu akavunga amesinzia usingiz mzito, nilijaribu kumuamsha ila akavunga kufa. Nilijaribu kulala ila sikuweza kupata usingizi nikaamua kwenda kulala kwenye sofa sebuleni ili nijisikie niko safarini.

Kuna kipindi nilipoteza kazi akaniambia ameonyeshwa kuwa hayo ni mapigo na wala sitakaa nipate kazi tena. Wakati huo nilikuwa nimepata kiwanja hapa Dar es Salaam na nikiwa najipanga kuanza ujenzi.

Nilikaa mtaani miezi miwili na baadae nikapata kazi mpya. Baaada ya kupata nilimwambia nataka kuanza ujenzi, yeye aliniambia ni vema nikaacha kujenga kwani nitapata hasara.

Nilimuuliza hasara gani nitapata akasema hiyo nyumba itakuja kuuzwa ili tugawane hela. Mi nilimambia simsikilii yeye ila naangalia mahitaiji ya watoto wangu kwamba wanatakiwa kuwa na nyumbani kwao.

Nilibahatika pia kupata gari na siku moja nikiwa safarini peke yangu kwenye gari nilipata ajali ya kugongwa na gari nyingine. Bahati nzuri ni gari iliharibika ila mimi nilibaki salama.

Baada ya tukio hilo siku moja tukiwa kwenye mzozo alinitolea neno kali kuwa nilipata ajali kwa maombi yake. Anadai aliomba nikipakia mwanamke kwenye gari yangu nipate ajali. Nilijisikia kumrukia nimle nyama mbichi lakini nikajizuia.

Mizozo imekuwa mingi mpaka najisikia kumtapika, sina amani wala furaha niwapo nyumbani. Watu wanaposema wamewakumbuka watoto hasa hasa mama yao kwangu inakuwa tofauti.

Sijawahi kunywa kilevi chochote na ivyo si mtu wa kurudi usiku niwapo mapumziko.
Kwa sasa nina nyumba mbili na magari mawili ila sina furaha ndani ya nyumba yangu.

Natamani kuwa na mwanamke atakayekuawa mke kwangu, huyu wa sasa najisikia kuachana nae kwani nikingalia miaka iliyoko mbele yetu ni mingi na siwezi kuendelea kuishi kwa mateso kwa kipindi cha utu uzima.

Naomba ushauri wenu wana jamvi

Pole !!!!!!!!!!! Huwezi kupata suluhu kwa kumwacha huyo mke na kutafuta mwingine kwani huyo mpya anaweza kuwa mbaya kuliko uliyemwacha na ukimwacha na huyo atakayekuja atakuwa mbaya kuliko waliotangulia na mwisho kabisa utageuziwa kibao kuwa wewe ndio mbaya kwa kuwa kila unayekutana naye ni mbaya kwako. Na mbaya nyingine wale watoto bwana naona mateso kwao hao ulionao kulelewa na mke wa pili na wa mke wa pili na wa kwanza kulelewa na wa tatu na nk

Ninavyojua mimi wanadamu wote ni wazuri kwa sababu wameumbwa kwa mfano wa MUNGU, ila aliye kinyume na MUNGU amewaharibu ili wafanane na yeye. kwa hiyo kila mtu ni mzuri tu ila aliye ndani yake ndiyo matokeo yake hayo unayoyaona. Na ili aondokane na hayo na wewe uipate amani unayoitamani ni muhimu ukutane na YESU na siyo yesu (usidhani kuwa nakubeza mkuu ila ni kutokana na maelezo yako yamenipelekea kuwa huna YESU bali una yesu)
 
Mimi ni Mkristo na kutokana na mazingira ya maisha ninaoishi nieshindwa kutangaza ndoa. Kwa hiyo naishi maisha ya kujifichaficha kanisani. Natoa sadaka, zaka na michango kwa kadri Mungu alivyonijlia lakini sishiriki meza ya Bwana. Inaniuma sana.

Very easy, huhitaji akili ya PHD kuamua hili, hamjafunga ndoa, ujue sisi wa kristo vile viapo mbele za Mungu, na mbele za waumini ndio hua vinatufunga kama hamjafunga ndoa mbona issue nyepes tu

simama kama mwanaume, kuanzia sasa tengeneza mazingira kwa wanao, hata mbuzi akili hana lakini ukimfundisha anaelewa, kama saa tano n mda wa kunywa maji kila ukifika huo mda utawaona wanaelekea mtoni wenyewe,

Miaka 10 sio midogo, huyo sio sahihi

Fanya mpango urudi kundini hata kimya kimya, mchungaji anaweza kukurudisha ofisini kwake
 
Ndiyo, hakuna mazingira ya kunishawishi kujifunga nira na mtu mwenye moyo kama huo. Mi natafuta namna ya kufanya kwa ajili ya kunusuru afya yangu na amani ya moyo wangu
saa miaka kumi yote unasubiri nini jamani? huoni kama ungekuwa umeshafanya maamuzi mapema na kuepusha yote hayo, mtu humwamini yet unadiriki kukaa naye miaka kumi na kuzaa watoto watatu naye, mmoja tunaweza sema ok hukujua but three? kama mtu unashindwa kuamini kumuoa, na hakushawishi why ten years with her? it doesn't make sense, nakushauri ufanye maamuzi na uanze maisha, hao watoto unawatesa tu kama wazazi ndio kugombana na kuogopana na nani mbaya hamleti mazingira mazuri kulea watoto, wewe ni mwanaume fanya maamuzi ya kiume. Maisha yako yanatilisha huruma but haileti maana. something is not clear.
 
Kaka pole sana mimi najiuliza kitu gani kinachompa jeuri huyo mwanamke kiasi hicho?

Kwasababu unatafuta pesa una-risk maisha yako mabarabarani hii yote kutafuta kwa aajili ya familia na yeye mkeo akiwa mmoja wa mtu anayeunda hiyo familia kama hujamuoa ndoa ya kanisani mwache asiwe mwiba kwenye maisha yako.

Au kama vipi mpumzishe kwanza aende kwao akakae huko kama miezi sita hivi aone joto ya jiwe labda ataona umuhimu wako.
Amuache ili iweje, hujui kama MUNGU hapendi kuachana? hakuna cha kanisani hapo hiyo tayari ni ndoa (10 yrs wanakaa pamoja na watoto 3 halafu uje na ushauri wa kuwaachanisha wewe. Mungu atakuhukumu wewe huyu jamaa akitoroaa majukumu yake hayo na hatimaye watoto kutaabika kwa ushauri wako huo
 
Acha kulalamika na kufeel sorry for yourself, kama unataka kuwa na furaha amua sasa hakuna kikwazo chochote. Kama hauna furaha sasa ni kutokana na uamuzi wako na wala si wa mtu mwingine, huyo Mwanamke ni none factor as far as i'm concern unless umeamua kuwa Jesus kuifia dunia then hauna sababu ya kulialia.
You have 2 options
1. Kaa na huyo Mama mvumilie huku wewe ukiumia na accept your fate quietly
2. Kick her out, tell her to go as far away as possible from you. Claim your life do the things that makes u happy, (usisahau wanao lakini) You do not owe anybody anything! Go on and live! DO IT NOW
 
Pole !!!!!!!!!!! Huwezi kupata suluhu kwa kumwacha huyo mke na kutafuta mwingine kwani huyo mpya anaweza kuwa mbaya kuliko uliyemwacha na ukimwacha na huyo atakayekuja atakuwa mbaya kuliko waliotangulia na mwisho kabisa utageuziwa kibao kuwa wewe ndio mbaya kwa kuwa kila unayekutana naye ni mbaya kwako. Na mbaya nyingine wale watoto bwana naona mateso kwao hao ulionao kulelewa na mke wa pili na wa mke wa pili na wa kwanza kulelewa na wa tatu na nk

Ninavyojua mimi wanadamu wote ni wazuri kwa sababu wameumbwa kwa mfano wa MUNGU, ila aliye kinyume na MUNGU amewaharibu ili wafanane na yeye. kwa hiyo kila mtu ni mzuri tu ila aliye ndani yake ndiyo matokeo yake hayo unayoyaona. Na ili aondokane na hayo na wewe uipate amani unayoitamani ni muhimu ukutane na YESU na siyo yesu (usidhani kuwa nakubeza mkuu ila ni kutokana na maelezo yako yamenipelekea kuwa huna YESU bali una yesu)

Acha kumtisha mwenzio. Amuache kabisa huyo mwanamke na asijichanganye zaidi kwa kuokoka au kuingia kwenye dini kupata suluhisho
 
Kwani kuchat na ex girlfriend wa kaka yao ni kosa...
Unajua wamemjualia wapi...?
Unajua kuna makaka wana date marafiki wa dada zao?

Jamani tujitahidi kuolewa kwetu kusiwe chanzo cha kusambaratisha familia za watu...
Kwani ukifanikiwa kumtenga mumeo na familia yake huwezi kuwa na amani kwenye ndoa yako kama huyu na mkewe...
Kwani mume akiwa hana amani wewe utaitoa wapi...?
kumbuka hao ni nduguze wewe ni mke ...kila mtu ana nafasi yake ...huwezi kuziba nafasi yao....moyoni anasononeka mwisho anakuchoka...

Pole sana mkuu, mke wako yaweza kuwa anatatizo lakini pia utafute chanzo cha hayo matatizo ni nini? familia zetu nazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kucreate tatizo na inapokutana na mke kasirani hali ndio inakuwa mbaya zaidi.

Nakuambia hivo kwasababu na mimi na experience hali ya mawifi wamekuwa hodari sana kuchat na x girlfriend wa kaka yao na ni kwa open ata ktk social networks naona, kwa vile mimi si mshari nanyamaza ila ukikutana na mtu ambae hawezi kuvumilia lazima reaction yake itakuwa kubwa, hivo mtu kama mimi nikimuambia mume wangu siwapendi wifi zangu hawezi kunielewa lakini kama ana busara inabidi anielewe sana tu.

Mara nyingi wanawake tunakuwa na upendo sana ukiona mwanamke anabadilika ghafla ujue kuna sababu inayompelekea kubadilika na once akibadilika kumbadilisha tena kazi sana, sasa kama unampenda tafuta njia ya kutatua na kufaham chanzo cha tatizo, lakini kama unahisi imeshindikana achaneni kwa wema
 
Pole sana mkuu, kuna swali najiuliza ambalo sijaona jibu lake humu, huyo mwanamke mlifunga ndoa?

Maisha ni yako kaka, hela unatafuta mwenyewe kaka, kama mtu haeleweki ndani ya miaka 10 ataeleweka lini tena? watoto wote watatu bado wadogo ila wa kwanza na wa pili nahisi wanaweza kujihudumia vizur sana

Cha msingi angalia Moyo wako unataka nini, watu wengine wanakuaga wametumwa na shetan kuwaharibia watu, au kukuondolea aman tu, Mwanamke rudisha kwao, tafuta dada wa kazi akusaidie kulea wanao mpaka watakapo kua ndio ufikirie kuoa mwingine, kwa sisi wa kristo dini hairuhusu kuachana ila kuna baadhi ya mazingira inabidi talaka ihusike, na mali za kugawana n mali mlizoshirikiana kutafuta kama kwenye uchumi wa familia hana mchango wowote anataka mali gani?

Utampa kiinua mgongo tu

Acha kupotosha au hauijui biblia, talaka ipo kwa Wakristo.
 
Umeona eehh

Life's too short, you only live once!

Acha kulalamika na kufeel sorry for yourself, kama unataka kuwa na furaha amua sasa hakuna kikwazo chochote. Kama hauna furaha sasa ni kutokana na uamuzi wako na wala si wa mtu mwingine, huyo Mwanamke ni none factor as far as i'm concern unless umeamua kuwa Jesus kuifia dunia then hauna sababu ya kulialia.
You have 2 options
1. Kaa na huyo Mama mvumilie huku wewe ukiumia na accept your fate quietly
2. Kick her out, tell her to go as far away as possible from you. Claim your life do the things that makes u happy, (usisahau wanao lakini) You do not owe anybody anything! Go on and live! DO IT NOW
 
pole ndugu jaribu kukaa na mwenzako muongee ai hata utafute mshauri wa mambo ya ndoa anaweza wapa msaada zaidi maana inaonekana kuna mambo mengi sana hapo ili kuyamaliza na kukaa kwa amani lazima kuwe na mazungumzo ya kina.
 
Nilitaka kukazia na miye kwenye elimu...nikaona huruma...

Haya wale wa std 7 ndio mke material njoeni pande hizi mtoe ushauri...

Kuna mengi yanachangia hapo ila kwa ufupi
Pengine ni
Elimu( afu mnasema ooh la saba na f 4 ndo wakuoa on a sasa)
Pengine ni asili yake ya ukorofi mwanzo hakukuonesha
Pengine ushawishi kashikwa akili na anao wajua
Pengine hakupendi kuna kitu alifata kwako keshakipata haoni tena umuhimu wako
Pengine pengine..

Wanasema kosea kujenga lakini si kuoa wala kuolewa

Ushakosea toka mwanzo
Angalia utaratibu was maisha yako na wanao
As long as hamjafunga
Ndoa nenda Naye taratibu MPE anachotaka anza upya
Yanini MTU mmekutana ukubwani akufanye uishi kama mtumwa ? Hiyo siyo definition ya ndoa
Sepa atakuua huyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom