Nahisi naonekana kama mwizi

Wazima wandugu...hili tatizo ni mimi tu au kuna mwingine linamtokea. Nikienda kwa vibanda vya mpesa mara nyingi wanataka Waone sms ilyorudi kwangu ndio wanipatie pesa, nikienda office za watu utaona mdada anahamisha pochi yake na simu , Bank teller anachukua mda mwingi kunihudumia.. saa ingine anaenda kupata ushauri kwa mwenzake au manager..... hii hali inanifedhehesha sana.
Ahahah, mkuu hiyo hata Mimi inanitokeaga sababu ya mwili na sura yangu ya kazikazi, ila mwisho wa siku niki-withdraw kiasi kikubwa cha pesa huwa wanaanza kujichekesha.

Halafu mi sina time nao mikausho mikali, nakushauri wapuuze tu boss, wajinga wengi wanahisi kuwa mwizi ni mtu mwenye sura iliyokaza au ambae yupo rafurafu, kumbe siku hizi wezi na matapeli wanakuwa smart kupita maelezo.
 
Nakuelewa sana, kuna wakati ilikuwa inanitokea hata mimi katika maofisi makubwa ilihali pesa ninayo ila nilikuja kugundua kuwa ni muonekano nikaweka mambo sawa.
 
Nakuelewa sana, kuna wakati ilikuwa inanitokea hata mimi katika maofisi makubwa ilihali pesa ninayo ila nilikuja kugundua kuwa ni muonekano nikaweka mambo sawa.
Inasumbua sana
 
Sasa mambo kama hayo ndio yananizidishia
Itabidi ujiweke sawa Mkuu, pia usijiaminishe sana kua watu wanakuona wewe ni Mwizi coz mtu anaweza akawa anahamisha simu yake au mkoba wake kwa lengo lingine kabisa ila wewe ukawaza anakuogopa wewe utaiba, unatakiwa uiondoe hiyo dhana uliyojijengea.
 
Umenikumbusha mi nlienda kwenye mpesa nimening'iniza funguo ya gar kiunon alaf Niko smart nikamkuta dada mmoja mkali balaa alaf nkaomba namba yake ili nitoe pesa akanipa nikatoa buku tu ,,
Daah yule sista aliniangalia Mara mbili mbili huku ananiuliza umetoa shingap? Nikamjibu buku akauliza "eeeeh?" Nikamjibu "buku" (ki gangster) huku nanyoosha mkono anipe hela yangu nlivyoondoka aliniangalia had napotelea.
 
Umenikumbusha mi nlienda kwenye mpesa nimening'iniza funguo ya gar kiunon alaf Niko smart nikamkuta dada mmoja mkali balaa alaf nkaomba namba yake ili nitoe pesa akanipa nikatoa buku tu ,,
Daah yule sista aliniangalia Mara mbili mbili huku ananiuliza umetoa shingap? Nikamjibu buku akauliza "eeeeh?" Nikamjibu "buku" (ki gangster) huku nanyoodha mkono anipe hela yangu nlivyoondoka aliniangalia had napotelea.
Hahahaha
 
Siobww hata mm sema sku hizi hata sijali nikiLa kinjunga changu naenda kwenye mishe kama kawa atakaenihisi mwizimwizi atajua mwenyew ila uzur wanaonijua wananifahamu hainipi shda ila kuna muda inaniua nguvu kuna sku nlienda kumsaidia fundi mahali naskia mafundi wengne site wanajifanya kuongea kiingereza cha kuombea maji wakinipa madongo uku wanatoa simu zao na nguo daah hata skukaa sana pale site nikajifanya naumwa ili tu niondoke skuweza kukaa sehem na watu ambao hawana amani na mm aisee iliniuma kingese
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom