Nahisi naibiwa hapa sina amani kabisa

The End..

JF-Expert Member
Aug 13, 2013
4,364
3,801
Habari za mchana wana MMU imani ni wazima wa afya.

Leo mwenzenu nina majanga yaani majanga.

Nina mpenzi wangu ambaye nimemwelezea sana humu JF ila la leo ni tofauti.

Kwa sasa amesafiri kwenda kwao Arusha sasa kule amekutana na mdogo ambaye anadai wanapendana kiasi kwamba wanachangia hadi vitu.

Nilikubaliana na yote ila hapa kwenye simu naona linanishinda muda mwingi nikimpigia simu yake inatumika hadi usiku na nitakapompata anadai alikuwa anatumia mdogo wake coz yeye hana simu.

Japo sio kawaida yake ila mwenzenu kiroho paaaa..

Hebu nisaidieni hapa siibiwi kweli.

cc miss chaga , watu8 ,Matola,Heave n on the earth, Tabibumtaratibu na wengineo
 
Inawezekana alichokwambia ni kweli, wewe usiwaze mabaya yoyote kwa sasa. Endelea kumuamini ila mwambie kuwa mawasiliano na wewe ni muhimu sana kwa sasa kwa kuwa yuko mbali na wewe hivyo apatikane mara kwa mara ili muongee. Kubali kuwa huna ushahidi wowote wa kumtuhumu kwa lolote na udumishe imani kwake hadi utakapoona dalili zingine kama kutokukuchangamkia tena unapoongea naye kwa simu. Ni hayo tu.
 
kama kweli hana simu, usiogope sana mkuu
ila kumbuka
'fimbo ya mbali haiuwi nyoka'
'sanda ya mbali haiziki maiti'
'dalili ya mvua mawingu'
ila pia 'zimwi likujualo halikuli likakumaliza'
halafu 'tahadhari kabla ya hatari'
 
we bora nidanganye danganye tu
ukiniambia ukweli nitaumia
we si unajua kwako Mi sijiwezi
ukiniacha nitalia
 
Hapo unaibiwa mkuu. Inamaana yeye hana hamu ya kuwasiliana na wewe mpaka ampe mdogo wake simu usiku kucha anaongea? Tafakari halafu chukua hatua
 
Tatzo wewe unahisi alafu hauongei.... Mwambie kwamba huna imani nae kutokana na kuongea usiku sana...
 
Kwa kiasi fulani hofu yako ina mantiki. Kikubwa jaribu kufuatiria ili ujilizishe kama ni kweli au si kweli. Binafsi huwa ninaamini kwenye mapenzi kina mama/dada ni weledi na wana hila. Yakupasa utumie akili nyingi kubaini ukweli.
 
Kama kaibiwa simu si umtumie hela anunue nyingne apo unajistukia tu wala uibiwi
 
kama kweli hana simu, usiogope sana mkuu
ila kumbuka
'fimbo ya mbali haiuwi nyoka'
'sanda ya mbali haiziki maiti'
'dalili ya mvua mawingu'
ila pia 'zimwi likujualo halikuli likakumaliza'
halafu 'tahadhari kabla ya hatari'

Na bandu bandu humaliza gogo......
Mgaaga na upwa.....hali wali mkavu.......
Ganda la mua la jana........
Ukiona zinduna........
 
kama kweli hana simu, usiogope sana mkuu
ila kumbuka
1. 'fimbo ya mbali haiuwi nyoka'
2. 'sanda ya mbali haiziki maiti'
3. 'dalili ya mvua mawingu'
4. ila pia 'zimwi likujualo halikuli likakumaliza'
5. halafu 'tahadhari kabla ya hatari'

hebu kidogo unaniacha mbali mkuu!!!
namba 1,2,3 zinaonyesha kabisa kuna tatizo ila namba 4,5 zinanipa matumaini fafanua japo kidogo!!!
 
Kwa kiasi fulani hofu yako ina mantiki. Kikubwa jaribu kufuatiria ili ujilizishe kama ni kweli au si kweli. Binafsi huwa ninaamini kwenye mapenzi kina mama/dada ni weledi na wana hila. Yakupasa utumie akili nyingi kubaini ukweli.

ni kweli mkuu ila naanzaje nataka nijue kabla hajarudi..........!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom