Nahisi mtoto sio wangu

Duh, kazi kweli kweli! Mkuu ulivyoanza kuhadithia ulitaka kufanana na mimi lakini ulipofikia kwenye kubadilis wanawake kama nguo hapo nikajiondoa. Hapa mkuu unaumizwa roho tu bila upige kimya usonge mbele na maisha. Kwa vile umeamua kuzaa naye piga mimba ya Pili fasta, wataosema mtoto siyo wako ni wapuuzi wewe lea hicho kiumbe kwa ajili ya watoto wako watakaofuata. Mimi dogo sikumtupa niliamua kumkea hivyo hivyo tu kwa kfumba macho sasa hivi kumaliza chuo na ajira juu! Wala simdai na mimi hanidai, nimefanya hivyo kwa ajili ya wadogo zake, najua hawezi kuwatupa hata iweje!
 
But every weekend nskuaga kwa mke wangu, na week days nskuwa kwa mke mdogo
Ila mkuu katika hili mmekubaliana na mke mkubwa kwamba uwe na mke mdogo? Tukitumia ubabe wa kiume huwa tunawaumiza sana wenza wetu. Mkuu ungeikubali hiyo hali ya kuwa na watoto hao wawili ungekaa maisha ya raha sana. Ukisikiliza pressure za ndugu hutatoboza. Mama mdogo nilimtoa mbio alitaka kuleta ujinga eti ananicheka kuwa na watoto watatu (wawili wa kwangu na mmoja wa wife), analinganisha na watoto wake kwamba wamepata watoto wengi. Nikampeleka darasa eeeeh, hao wajukuu zako lundo wamefanikiwa katika nini? Nikamwambia wa kwako wanazidiwa thamani na hao wa kwangu watatu maana wote wako chuo kikuu na mkubwa wao kamaliza na ana kazi yake! Wa kwake ni wavuta bangi mtaani, hiyo inaitwa SROI. Kwa hiyo kuwa na watoto wachache hujapoteza pambano, ni wewe tu ndiye unajipa pressure!
 
Kwa hiyoo watoto wiwili umeona hawatoshii unahangaika kupata watatu wa nje??? una matatizo ya akili kijana miaka 45 ila bado akili za balehee zimekujaa.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Watoto wawili hawatoshi jomba ? Huyo wa 17yrs kama ni wa kike kesho Kesho atakuletea mjukuu, huku bado unahangaika tena kuzaa n vibinti
Unanipangia ukibwa wa, familiayangu kwan inakuhusu
 
Wewe ni mtu mzima sana. Halafu hapa duniani sio kila hitaji la moyo wako lazma litimie kwa asilimia miamoja.

Watoto umepata lakn bado unahangaika kutafuta wengne. Sasa hapo mzee mwenzangu umri wako unaikaribia 50 ndio kwanza unamtoto ana miezi.
Huyo mtoto utamlea kwa pensions???

Na huko kwenye DNA utajisumbua tu. Watakupa majibu ya kukuridhisha wewe. DNA watakupa majibu ya kweli endapo mtoto anagombaniwa na wanaume wawili tofauti.

Hii ya kupima DNA kwa kutaka kujua kama ni wako au sio wako watakupa majibu kuwa huyo ni wako maana endapo wakikwambia sio wako inamaana tayari wewe utamkataa na je mtoto atalelewa na nani?

Acha ujinga tulia na watoto wako uliobahatika kupata lea watoto wako
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…