Nahisi kukata tamaa msaada wenu jamani

Vidonge vya vitamin C nimetoka kumaliza weekend iliyopita tu, machungwa nimekula sana mkuu kwa siku si chini ya matano
Basi muone daktari wa magonjwa ya koo.
By the way, hujawahi kuzama chumvini kweli? Isijekuwa umepata fungus wa mdomo.
 
Habari wakuu.
Nimekuwa nikisumbuliwa na hili tatizo yapata mwaka sasa bila mafanikio, ulimi wangu umekuwa unalika na kupona wenyewe upande mmoja, kuna kipindi nahisi kama kuna kitu mafano wa chakula kimekwama kooni na maumivu kwa mbali sana kooni, kifua na koo kuwaka moto, natokwa na vipele vidogo mkononi tumboni na kifuani, mwili kuchoma choma nimeenda hospital nyingi tu tangu mwaka jana naishiwa kupewa dawa tu bila kufanikiwa, nimekuwa na mawazo hadi nakosa raha kabisa naombeni ushauri wenu wakuu. Naambatanisha na picha hapo chini
Pole sana mkuu,hakuna tatizo lisilo na ufumbuzi amini hilo,usikate tamaa
Ipo siku utapona na itabaki historia tu kuwa ulikuwa na tatizo hilo

Jaribu kuonana na daktari wa magonjwa ya ngozi huku ukiendelea kufatilia ushauri ulopewa na wadau wa kutumia vitamin c,au malt vitamin,pamoja na kula matunda yenye njano mf machungwa,nanasi n.k

Naamini utapona.

Na kama ni mwanaume na kwa wanaume wengine wote muepuke sana kuzama chumvini,inaweza waletea matatizo kama mwanamke ana fangas au hajisafishi vizuri,sijamaanisha mtoa Uzi anafanya hivyo ila ni ushauri tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Assante sana ndugu ubarikiwe nafurah kwa kunipa moyo niko kwenye mchakato wa kufuata ushauri wenu
 
Kuwa na ugonjwa ni jambo moja, lakini hakuna kitu kinaumiza kama kutokuambiwa unasumbuliwa na kitu gani hospital.
Unapewa dawa na tiba mbalimbali lakini hauponi, hii inasababisha msongo wa mawazo kuliko hata ugonjwa wenyewe.

Jambo la kwanza, iambie nafsi/akili yako kwamba huo ugonjwa hata kama hospital hawajasema ni kitu gani lakini utapona.
Ukikata tamaa, hata utumie dawa gani, hautapona na hali inazidi kuwa ngumu zaidi.
 
Pole mkuu kwa mateso unayoyapata,Mungu akufanyie wepesi katika hali yako upate tiba stahiki kwa tatizo lako!Madaktari naomba mje huku huu ndio muda wenu wakujidai nakujionyesha mnachokijua msituachie siye kina yakhe wakukisia.Njooni please mtoe ushauri ndugu yetu anateseka,Huu uzi upo kwenye idara yenu njooni kwa wingi.Mkuu nimewaita nadhani wakipata nafasi watakuja tu vuta subra!
 
Assante mkuu
 
Back
Top Bottom