Nahisi kuchanganyikiwa: Kodi ya chumba imeisha natakiwa kuhama na sina hela

Pole sana mkuu ila siku nyingine hakikisha unaweka kodi au unajua pa kupata kodi mapema.
Niko radhi nisile ila niweke hela ya kodi aisee.
 
Yakupasa umueleze mwenye nyumba hali iliyokukuta na kama inakuwa ngumu nenda kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa na umueleze shida iliyokukuta.

Hiyo shida yako sio ya kujitakia ni shida inayoweza kumpata mtu yeyote, uliugua na ukashindwa kuzalisha matokeo yake umeshindwa kutimiza malengo uliyoyakusudia---- hao wote, mwenyekiti na mwenye nyumba ni binadamu watakaa wafikirie kitu cha kufanya (wakupe muda mchache wa kuendelea kukaa hapo ili uzalishe kipato).

Hiyo ni miongoni mwa kazi za mwenyekiti wa serikali za mitaa.
Pata pepis
 
Kama ulipaji wako wa kodi kwa mwenye nyumba ulikuwa mzuri kabla ya kupata shida, ukimweleza mwenye nyumba atakuelewa, tatizo ni pale ambapo kama utakuwa ni msumbufu wa kulipa kodi kwa mwenye nyumba, mwenye nyumba ataitumia shida yako kama fimbo ya kumuondolea shetani aliyemvamia kwenye nyumba yake.
 
Tatizo ni kwamba hiki chumba kuna mtu ashalipia tayari na anategemea kuhamia leo jioni tarehe moja.

Back
Top Bottom