Nina matatizo ya kifedha na sina msaada wowote. Nimepanga kuwatelekeza mke na watoto

Marashi

JF-Expert Member
Apr 14, 2018
2,774
4,269
Nimeshafanya booking, nitaondoka na bus la Kidia One kwenda mkoani Arusha nikatafute maisha. Ninasikitika kwakua nitaondoka bila kuaga na ninaiacha familia yangu katikati ya ukata mkubwa wa kifedha huku ikishindwa kumudu mahitaji yakila siku. Lakini kuliko nibaki tufe wote acha nijiendee Arusha nikabangaize maisha.

Januari hii mwanangu mkubwa Zawadi alitakiwa kwenda shule tar 7 na ada mkononi Sh.680,000 tasilimu. Hata mahitaji mengine madogomadogo kama sweta la shule na viatu navyo vimeshindikana. Kodi ya nyumba itaisha tar 23 na mwenyenyumba amedai nihame kwakua nyumba yake anabadili matumizi, hapangishi.

Mimi na mke wangu wote tulikua tunafanya kazi. Mimi kwenye kiwanda cha Gypsum na mke wangu kampuni kubwa ya Vinywaji. Lakini kama mnavojua kikiri na kakara za kampuni binafsi hasa uzalishaji unapopungua, alianza mke wangu kufukuzwa nikafuata mimi.

NSSF wananipa elfu 24,500 kila mwezi fao la kukosa ajira, huu ni mwezi wa 4 na watalipa ndani ya miezi 6 tu. Mke wangu yeye hakua anachangia.

Nimejaribu kumshauri mke wangu tu-downgrade maisha hataki. Kodi kwa mwezi tunalipa 180,000 chumba masta, sebule na jiko Mburahati. Mtoto anasoma darasa la tatu ada kwa mwaka jumla 1,550,000. Nimeshakopa sana, nimejaribu vibarua lakn kazi nzito siwezi nina matatizo ya kifua.

Ninamuacha mke wangu mama zawadi, zawadi na Taia mtoto wetu wa mwisho kwenye nyumba ya kupanga na hali mbaya ya kiuchumi. Lakini sina namna. Mimi na mke wangu tulishapitia matatizo na migogoro mingi sana lakini kwa sasa imeisha na tulishasameheana. Ugumu wa maisha ndio unanifanya nikimbie Dsm

Kama kuna msamaria anaweza kunipokea na kunipa hifadhi ya siku mbilitatu Arusha tafadhali sana aje PM na nitashukuru sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejaribu kumshauri mke wangu tu-downgrade maisha hataki
Hapo ndipo kwenye tatizo. Kabla hujaondoka, kama una chochote, kodi chumba cha elfu 20, acha kilo kumi za mchele na maharage. Andika kinote kuhusu haya maelekezo ukiweke mahali mkeo akipate. Uache na funguo ( na namba ya dalali anayejua chumba kilipo) Siku wakifukuzwa hapo, utamkuta keshahamia chumba kimoja yeye na watoto wako. Acha maelekezo mtoto akasome shule za serikali, ada ni bure.
Ukirudi toka Arusha, utawakuta 'wamesha settle'.
 
Daah nataman nimlaumu JIWE kwa kuyaleta haya ila nawaza siye anaeleta fedha nyumbani ila nafikiria zaidi labda anahusika namna moja au nyingine(nadhani nimepatia hapa)

Real JF sa hivi imekuwa sehem ya watu kueleza shida kuliko habari.
pole mkuu kila la heri
 
Hapo ndipo kwenye tatizo. Kabla hujaondoka, kama una chochote, kodi chumba cha elfu 20, acha kilo kumi za mchele na maharage. Andika kinote kuhusu haya maelekezo ukiweke mahali mkeo akipate. Uache na funguo. Siku wakifukuzwa hapo, utamkuta keshahamia chumba kimoja yeye na watoto wako. Acha maelekezo mtoto akasome shule za serikali, ada ni bure.
Ukirudi toka Arusha, utawakuta 'wamesha settle'.
naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia..
 
Kaa chini na mkeo umuelezee uamuzi wako wa kwenda Arusha na sio kuwakimbia kimyakimya bila taarifa yyte. Acha ubinafsi...Mfikirie mkeo utamuacha kwenye hali gn ukimtelekeza yy na watoto na kodi ya nyumba ndo inaisha. atleast mueke wazi km unaondoka
 
Back
Top Bottom