genious wa kijiji
Senior Member
- May 1, 2014
- 173
- 248
Wakuu
Nilikua nimepanga kwenye chumba kimoja kodi elfu thelathini kwa mwezi. Kodi inaisha kesho tarehe 1 agosti na ninatakiwa kuhama kwa kuwa nilishaongea na mwenye nyumba tukakubaliana kwamba kesho nihame hivo tayari alishatafuta mtu wa kumpangisha na huyo mtu anahamia kesho jioni hivo natakiwa kuondoka.
Mm sina kazi maalum isipokuwa naungaunga mtaani leo natembeza mitumba kesho nauza machungwa ili mradi mkono uende kinywani.
Sio kwamba sikuwa na taarifa ya kuhama, taarifa nilikua nayo ila mbaya zaidi takriban wiki nzima nilikua naumwa hivo sikuenda kutafuta. Jana na leo ndo nimeenda na nimebahatika kukusanya 20,000/=
Hii haitoshi kulipa kodi ya chumba kwani vyumba vingi mjini vinaanzia 30000 na unatakiwa kulipa kuanzia miezi mitatu.
Wakuu naomba ushauri nifanyaje ili hii elfu ishirini izalishe walau 90000 kwa siku ya kesho nikatafute chumba nilipie.
Niko tayari kufanya mishe yoyote halali nipate hela ya pango.naombeni mawazo yenu